Serikali ya awamu ya tano inatumia cash budget, kuna baadhi ya taasisi ya serikali zinahitaji wafanyakazi wake kusafiri mfano wakaguzi ili kutekeleza majukum yao . Mfano unakuta kuna taasisi inatumiwa hela kwa kila mwezi ambazo hazifiki hata nusu ya mahitaji yake kwa mwezi huo na unakuta hakuna hela za matumizi ya kila siku kama mafuta na wafanyakazi wanaenda kufanya kazi za serikali kwa kukopwa per diem!? Mipango kazi yenye tija inashindwa kutekelezeka. Je hii ndiyo maana ya kubana matumizi?