Hivi CAG hakuomba majibu ya zilipo trilioni 1.5 kabla ya kuandika ripoti yake?

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,526
Hili ndilo swali ambalo tunapaswa kujiuliza wote, mpaka CAG kutoa ripoti yake aliomba majibu ya fedha hizo na huenda hakuridhika nayo ndio maana akaliweka hili katika ripoti yake.

Inakuwaje pesa ya serikali isijulikane ilipo? Fikria umetunza pesa yako sehemu salama baadae usiikute pale, uulize kila mtu aseme hajui, moja kwa moja utajua umeibiwa.

Hivyo basi majibu tunayopewa sasa hivi alipaswa apewe CAG ambae ndie mtaalamu, na kama alipewa na hakuridhika nayo kwanini na sisi wengine turidhike nayo?

Sidhani kama ofisi ya CAG yenye wataalamu lukuki wanaweza kukurupuka kuandika kitu ambacho hakipo na hawajajiridhisha nacho, hoja ya msingi ni kwamba zip wapi trilioni 1.5 hayo mengine ni kujaribu kujikosha tu na kujifanya wakali ili kufunika mambo, na hili tulilitegemea.
 
Kwani jana CAG ikulu alienda kufanya nn...maana hausiki kabisa na tukio la jana....bila shaka kaambiwa akiendelea atapotezwa na akapewa mfano mdogo wa risasi 38 za risu
 
Inaumiza sana.. hoja ya 1.5 trillion inajibiwa hivi.. 'Hakuna kitu kama hicho. Hazina tupo vizuri' alafu jiwe anachekelea tu...
 
Hili ndilo swali ambalo tunapaswa kujiuliza wote, mpaka CAG kutoa ripoti yake aliomba majibu ya fedha hizo na huenda hakuridhika nayo ndio maana akaliweka hili katika ripoti yake.

Inakuwaje pesa ya serikali isijulikane ilipo? Fikria umetunza pesa yako sehemu salama baadae usiikute pale, uulize kila mtu aseme hajui, moja kwa moja utajua umeibiwa.

Hivyo basi majibu tunayopewa sasa hivi alipaswa apewe CAG ambae ndie mtaalamu, na kama alipewa na hakuridhika nayo kwanini na sisi wengine turidhike nayo?

Sidhani kama ofisi ya CAG yenye wataalamu lukuki wanaweza kukurupuka kuandika kitu ambacho hakipo na hawajajiridhisha nacho, hoja ya msingi ni kwamba zip wapi trilioni 1.5 hayo mengine ni kujaribu kujikosha tu na kujifanya wakali ili kufunika mambo, na hili tulilitegemea.

Kwenye ukaguzi wowote kuna kitu kinaitwa " clarification of issues". Mkaguzi anapokutana na jambo lenye utata kabla ya kuliandika kama kasoro huwapa nafasi taasisi inayokaguliwa kutoa ufafanuzi. Kama taasisi inayokaguliwa haikutoa ushirikiano inabidi mkaguzi aiandike hoja hiyo kama kasoro, na hata ikitoa maelezo siyo lazima mkaguzi aifute hoja hiyo kwa sababu maelezo lazima yajitosheleze kulingana na viwango vya ukaguizi
 
CAG hana uwezo wa kulazimisha mtu kutoa majibu,ameandika na anazo nyaraka za mawasiliano kuomba majibu. Kazi ya kulazimisha majibu wameachiwa wabunge. Sikiliza clip akihojiwa Azam
 
Tupate nakala ya CAG ukurasa wa 33-34 ndio itakuwa mwisho wa figisu.
 
Majibu yapo kwenye speech ya mwenyekiti wa kamati.Ifatilie vizuri,ila kama wewe ni shabiki wa majani wala usiisikilize maana itakuchefua.Tuache mapokeo,bali tufate uyakinifu wa mambo.
 
Kwanini watu mnakuwa wagumu kuelewa, hakuna mahali CAG kasema pesa imeibiwa ila alisema haijulikani matumizi yake, kwa swali ambalo aliuliza maghufuli kuwa pesa zimeibiwa CAG yupo sahihi kabisa kujibu kuwa hakuna pesa iliyoibiwa Kama angesema ndiyo pesa imeibiwa angeulizwa ameiba nani Na aliiba vipi?, Wakati CAG Hana majibu yake wenye mamlaka wa kugundua Hilo Ni polisi Na takukuru
 
Kwani jana CAG ikulu alienda kufanya nn...maana hausiki kabisa na tukio la jana....bila shaka kaambiwa akiendelea atapotezwa na akapewa mfano mdogo wa risasi 38 za risu
Ikulu jana aliitwa ili jiwe lijisafishe.
 
Back
Top Bottom