Uchaguzi 2020 Hivi Bunge lina kazi gani kama kila anapokwenda kwenye kampeni, Rais Magufuli ndiye anayeahidi kujenga miradi mbalimbali?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,221
2,000
Tunavyofahamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. inaeleza wazi majukumu ya kila mhimili wa Dola, ikiwa Bunge ndilo lililopewa jukumu la kupanga bajeti na kupanga miradi hiyo ipelekwe wapi.

Lakini nashangazwa mno na namna Katiba ya nchi inavyosiginwa siginwa, kwa Rais Magufuli kutwaa madaraka ya Bunge, kwa yeye kila anapokwenda kwenye kampeni zake, kuagiza miradi mbalimbali, ianze kutekelezwa katika maeneo hayo.

Mbaya zaidi ni pale mgombea huyo wa kiti cha Urais wa CCM, John Magufuli, anapowadanganya wananchi kwenye maeneo yao kuwa, wabunge wa upinzani, hawawasemei wananchi hao wanapokuwa Bungeni na hivyo kuwaomba wananchi hao, eti wawachague wabunge wa CCM, ambao kwa madai yake ndiyo wanaoweza kuwasemea wananchi hao.

Hivi nchi hii Katiba ya nchi inaweza kusiginwa kwa kiasi hiki, huku Tume ya uchaguzi ikiwa inaangalia hivi hivi bila kuchukua hatua zozote?

Hivi Rais Magufuli kuwatangazia kwenye mikutano ya kampeni, siyo tu kunavunja Katiba ya nchi, kwa kuwa anaamua kuyapora mamlaka ya Bunge, bali pia anatoa rushwa kwenye hayo maeneo, kwa kuwa tayari kipindi hiki cha kampeni, Bunge la nchi yetu lishavunjwa.

Ninachowauliza NEC, hivi kwa haya anayoyafanya mgombea Urais wa CCM, John Magufuli, siyo kuvunja kanuni zao wenyewe NEC za kutotaka mgombea yeyote wa kiti cha Urais, wakati wa kampeni kutoa ahadi zozote za miradi, wakati wewe ni mgombea kama walivyo wagombea wengine?
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,352
2,000
Mbali na hayo yote pia idadi ya wabunge nikubwa sana baadhi yao nimipasho na zomeazomea. Kazi kubwa kwao imekua vyamavyao kwanza halafu watanzania baadae.

Wanajizungushatu kwenye viti,vitolewe wawekewe mabenchi au madawati na maslahi yao yapunguzwe ndio itakua rahisi kuwasemea watanzania wanyonge
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
11,262
2,000
Sijui kwanini imefikia hapa!
budget yote ya nchi ipo mikononi kwa mtu mmoja!
Ndie anaamua kodi za watu ziende wapi na sio Bunge tena!
halafu kuna mtu anajiita spika na kujidai eti bunge lake ni imara!
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
37,471
2,000
Sijui kwanini imefikia hapa!
budget yote ya nchi ipo mikononi kwa mtu mmoja!
Ndie anaamua kodi za watu ziende wapi na sio Bunge tena!
halafu kuna mtu anajiita spika na kujidai eti bunge lake ni imara!
Hakuna wasomi wa kupaza sauti wapo tu kazi ni kujipendekeza.
 

maalon

JF-Expert Member
Feb 14, 2015
428
500
"Mkichagua mbunge kutoka upinzani sitaleta maendeleo kwenye maeneo yenu"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom