Wanajukwaa habari, nimekuwa nikijiuliza, hizi taasisi za serikali mbona ziko kimya sana, wakati.ndizo.zenye jukumu la kumlinda mlaji wa mikopo hii ya kwenye simu kutoka tigo na airtel ambao kiukweli wanamwibia mteja. Tigo ukikopa shilingi 120,000/= kwa siku 21 unatakiwa urudishe shilingi 144,600/= ambayo hii ni sawa na riba ya 27.3% kwa mwezi au 328% kwa mwaka, jamani huu ni wizi, hata kama hii mikopo risk yake ipo juu.
Airtel wao ukikopa shilingi 136,000/= utatakiwa urudishe shilingi 161,092/= baada ya siku 21 ambayo ni sawa na riba ya 24.6% kwa mwezi au 320% kwa mwaka.
Kidogo afadhali ni voda ambao wao wanakopesha kwa mwezi, ukikopa shilingi 46,000/= utalipa shilingi 50,140/= baada ya mwezi mmoja, hii ni sawa na riba ya 9% kwa mwezi au 108% kwa mwaka. Japo hii iko juu ila ni nafuu ukilinganisha na mitandao mingine.
Kwa hili naomba BOT na TCRA waingilie kati kulinda haki ya mteja, badala ya kuyaacha haya makampuni ya simu yakiwaibia wateja
Nawasilisha.