Hivi biko sports mna tatizo gani ?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,399
Habari wadau
Kwa wale wapenzi wenzangu wa kubet matokeo ya soka mtakubaliana na mimi kwamba kwa sasa kumekuwa na kampuni nyingi za kubetisha on line.
Utaratibu unafahamika kwamba ukishabet na kushinda malipi hutolewa siku hiyohiyo au kesho yake.
Cha ajabu kumejitokeza kampuni ya kitanzania ya biko sports ambayo nayo imeingia ktk kubetisha lakini ikiwa haijajipanga ipasavyo.
Pamoja na odds nzuri na option nyingi za kubet walizonazo hawa jamaa ni wasumbufu ktk kulipa ukishashinda mkeka,binafsi mara nyingi wananilipa baada ya wiki tena baada ya kupiga sana simu ofisini kwao,nimeshawah pia kulipwa baada ya wiki nne toka nishinde mkeka.
Najiuliza hivi usipowapigia kudai pesa yako si wanaweza kukausha wakakutapeli jumla ? Kupitia uzi huu naomba niwashauri wajipange ipasavyo kama wanataka kufanikiwa ktk suala la betting maana biashara za pesa zinataka ujenge kuaminika kwa wateja ndipo utafanikiwa kinyume cha hapo hawatafika mbali watu watawakwepa.
Naomba kuwasilisha,
Nb:aione mmiliki wa biko sports au watendaji wa biko sports.
 
Yaani kampuni kibao na nzuri za kubetia zipo na malipo ni rightaway unaenda kubetia biko?
 
Kwahiyo ndo umetuanzishia na uzi kabisa? Sasa tutakudhulumu kabisa ndo utujue sisi ni biko
 
Back
Top Bottom