Hivi Barça(bunge) wamejiandaa kweli kupambana bila uwepo wa Messi (CAG) kwenye timu yao?

Makambovich

JF-Expert Member
Oct 27, 2018
207
200
Jana taarifa ya CAG iliwasilishwa bungeni Kama sheria inavyotaka!
Kabla taarifa hiyo haijawasilishwa kila mtu anajua Barça(bunge) liliamua kuvunja mkataba na mchezaji wake mahiri Messi (CAG).
Kwa miaka mingi uwepo wa Messi (CAG) uliwang'arisha wachezaji wengi wa Barça(bunge) kutokana na pasi zake za mwisho kutumiwa vizuri kwenye mechi mbalimbali (Mfano hoja mbalimbali za mikataba mibovu) ambazo kwa namna moja ama nyingine zilifanya baadhi ya wachezaji wa Barça(bunge) kuonekana mahiri.
Kwa sisi wadau wa michezo tunajiuliza kama Barça(Bunge ) wakiachana na Messi (CAG) wataweza kweli kuchangia hoja zao kwa data zilizochakatwa au itakua ni kutumia hisia na tetesi za mtaani.
Kumbuka kwa sasa upatikanaji wa habari zile muhimu/nyeti sio kama kipindi cha awamu ya 4 ambapo watumishi wasio waaminifu walikua wananyofoa docs muhimu na kuwapasia ndugu zetu.
Najaribu kuwaza jinsi ambavyo Barça (bunge) itakavyo tumia muda mwingi kupaki basi kutokana na kukosa makali.
 
Back
Top Bottom