Elections 2010 Hivi Baraza la Mawaziri la Kikwete kama akishinda litakuwaje?

Innolee

Member
Oct 6, 2010
9
0
Tumeona ....Hawaaminiki,Lkini hatujui kama mheshimiwa ataamua kuwajaza tena ktk uwaziri..or kwakuwa amepiga kazi mwenyewe ..basi hatajali kulipa fadhila...??
 
Atamteu Waziri mkuu toka mkoa wa Mbeya kurudisha imani ya CCM kwa wana Mbeya
 
JK atajaza mafisadi wenzie lakini vijana atawapooza na Unaibu kibao....tegemea baraza la mawaziri nene kama hili la sasa.......lengo ni kufurahisha walaji wa mali za umma ili wasimnyanyapae....................
 
Tumeona ....Hawaaminiki,Lkini hatujui kama mheshimiwa ataamua kuwajaza tena ktk uwaziri..or kwakuwa amepiga kazi mwenyewe ..basi hatajali kulipa fadhila...??

Bora liende, hayuko serious kiasi hicho hivyo hategemei Baraza la Mawaziri serious. Matokeo yake wataning'inizwa Bungeni mpaka macho yawatoke kama panya aliyekamwatwa na mtego.

 
Tegemea lowasa kurudi maana kwenye kampeni alimnadi kuwa hakuna kama yeye, na kipenzi chetu mwakyembe usishangae akaachwaa
 
spika - Lowasa, Akina mama - Salma kikwete, Vijana - Riziwani, fedha - Rostam, Waziri Mkuu- MAsha
 
Usitegemee jipya kutoka kwa JK,mawaziri 60 na zaidi kulipa fadhira,muendelezo wa Ukoloni mamboboleo.
 
Kikwete atashinda na baraza la mawaziri litakuwa nzuri sana

Baraza la mawaziri kama wakifanikiwa kuchakachua na wananchi kukubali basi litaundwa na Jakaya akisaidiwa na mkewe Salma na mwanae Ridhwani: ndio hasara ya kuifanya institution kama Presidency kuwa family business!! Watajaa vilaza wengi wanaovaa kininja!! I bet you Mwantumu Mahiza will be in!!
 
Nategemea mtu kama Masha kuwa kupata nafasi ya Uwaziri ingawa amedondoka..atapata uteuzi wa rais...Pia mamvii nae huenda akapambana kwenye U spika..Pinda atarejea kwenye nafasi yake ya U -PM..ila baraza la mawaziri linaweza kuwa na watu wale wale wakina kawambwa..ngeleja..mkulo etc mabadiliko madogo yatakuwa kwa mawaziri waliodondoka..Batilda..Kamara etc
 
hata kama ataweka mafisadi wake kuwa Mawaziri wananchi wakae wakijua sheria zote zinapitishwa bungeni kwahiyo hiyo mikataba fake na ufisadi wao utakuwa limited na Kikwete hana interest au kitu chochote atakachojali kwani 2015 ni mwisho wake. CCM yenyewe inajua Kikwete hana interest na hii nchi kwani makosa makubwa ni kutowakubalia walioshinda kura za maoni kugombea, CCM imekuwa na makundi ambayo yanamwumiza kichwa hata mabest zake wa karibu wanamtosa.
Kazi ni bungeni, na upinzani utahakikisha Katiba inafanyiwa marekebisho makubwa tena kuanzia kuteua majaji, kuteua tume za uchaguzi ziwe kwenye neutral ground kwani Rais pia ni mwanachama wa chama fulani kinachogombea kwanini ateue watu kama hao na nina uhakika 100% kiongozi yoyote wa upinzani akishinda issue ya katiba haitamsumbua kitu kwani anajua ameingia kwa nguvu za wananchi na katiba si tatizo ila kwa CCM especially JK hiyo inampa kiburi...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom