Hivi Bara la Africa ni laana au ni kitu gani?

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Africa ni bara ambalo ni zuri sana! Lina mimea mizuri ya asili,mito,bahari,madini kila aina,milima
mbuga mzuri za wanyama,wasomi na viongozi wa taasisi mbalimbali. Nadiriki kusema mungu ali
lipendelea bara hili kuliko bara lolote hapa Duniani!.

Lakini ukiiondoa South africa kidogo, Nchi zote zilizobaki ikiwemo Tanzania yetu ni matatizo kibao
kama si lukuki. Njaa Africa,vita Africa,malaria Africa,ukimwi Africa,matatizo ya umeme Africa,elimu
mbovu Africa, viongozi kung'ang'ania madarakani Africa na kadha wa kadha.Yaani yapo mengi sana
lakini hapo nimeolozesha machache tu!.

Hivi tatizo ni nini? Hebu angalia tulifurahi kuondoa ukoloni kwa kusema tujitawale na tuendeleze nchi
zetu wenyewe,lakini kiko wapi? Leo hii wale wakoloni wamerudi,japo hawatutawali kwa fimbo kama
zamani lakini wanatutawala kwa remote control [nguvu za kiuchumi na elimu] Haitoshi bado viongozi
wetu wanapanda ndege kila siku kuwafuata hukohuko ulaya na America waje kuwekeza kwenye secta
zote ndani ya nchi zetu kasolo IKULU. Yaani ni SHAME ON US kwakweli!

Na jinsi wageni hao 'hasa watu weupe'wanavyothaminiwa kwenye nchi zetu ni balaa tupu! viongozi wetu
wako teyari kukufunga au hata kukuuwa wewe mzawa kuliko kumpoteza huyo mwekezaji uchwara.
Kuhusu misaada toka kwenye hizo nchi tajiri ndio usiseme! lakini zinaishia mifukono mwa watawala.
Na ukithubutu kuhoji tu,MIAKA MIA JELA.

Hizo nchi zinazopigana vita kila kukicha ndio usiseme! ziko kibao! Somalia,Rwanda,Liberia,Sudani,Congo.Burundi,Sieralleon na sasa inanukia hapo Ivory coast tena.
Yaani kwa ufupi ni tafraani na wakhaaka tupu ndani ya bara hili teule la mwenyezi mungu!.

Toka Dunia imeanzishwa na mwenyezi mungu, hatujawahi kutengeneza magari yoyote ya maana
kwa kuitwa gari! achilia mbali Helcopitor,ndege,pikipiki,train,maboat ya kisasa na hata baiskeli.
Ilihali wasomi waliosoma mpaka kupindukia kwa ndani na nje ya nchi tunao! TATIZO NI NINI?

Nawasilisha wandugu
 
Tuliondoa wakoloni weupe tukaweka wakoloni weusi. Ni afadhali kuwa chini ya mkoloni mweupe kuliko kuwa chini ya mkoloni mweusi maana na roho yake ni nyeusi kweli sio uongo.
Hapa ndipo our grand fathers missed!
 
Back
Top Bottom