Hivi Bangi Huwa ina nini? Haya ni machache yaliyowahi kuniacha hoi

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Juzi jamaa mmoja wa Muleba kwenye TV anadai yeye akivuta anakuwa na nguvu ya kulima hekari kwa muda mfupi. Kuna jamaa yeye alienda kuogelea kwenye maji yaliyotuama barabarani akidhani ni ziwa.

Mwingine alikuwa anaona umati wa watu wanamkimbiza wakati yuko peke yake. Mwingine mtaro mfupi na mwembamba yeye anauona kama ziwa tanganyika

Mwingine ukimtengea ugali hata uwe mkubwa kiasi gani anaumaliza peke yake
Mwingine akuruka sarakasi bila kushika chini huku akiwa hajui lolote kuhusu sanaa hiyo akaishia kuvunjika

Mwingine ukimuangalia machoni anakuonea aibu, na kukuchukia..
Mwingine anachekacheka bila sababu...

........

Hivi huu mmea Haramu Kwa tanzania huwa una ingrediates gani hadi unahamisha bongo kiasi hiki.
4899069_delta_jpeg7750a516e434b4a718a9bbefe3112ec9


Ongezea zako....
 
Juzi jamaa mmoja wa Muleba kwenye TV anadai yeye akivuta anakuwa na nguvu ya kulima hekari kwa muda mfupi.

Kuna jamaa yeye alienda kuogelea kwenye maji yaliyotuama barabarani akidhani ni ziwa.

mwingine alikuwa anaona umati wa watu wanamkimbiza wakati yuko peke yake

Mwingine mtaro mfupi na mwembamba yeye anauona kama ziwa tanganyika

Mwingine ukimtengea ugali hata uwe mkubwa kiasi gani anaumaliza peke yake

Mwingine akuruka sarakasi bila kushika chini huku akiwa hajui lolote kuhusu sanaa hiyo akaishia kuvunjika

Mwingine ukimuangalia machoni anakuonea aibu, na kukuchukia..

Mwingine anachekacheka bila sababu...

........

Hivi huu mmea Haramu Kwa tanzania huwa una ingrediates gani hadi unahamisha bongo kiasi hiki.

Ongezea zako....
Mshana Jr. aje hapa mara moja... Alishazungumzia uhusiano wa bangi na jicho la tatu au sixth sense
 
Mbona dalili ulizojaja hata wagonjwa wa malaria wanazo. Hapo suala sio bangi tatizo ni uwezo wa ubongo wa mtumiaji kuhimili kiwango cha dozi ya bangi!
Kipimo,kipimo, kipimo........!
KWENYE DALILI ZA MARALIA HOSPITALI HAKUNA HAYO ISIPOKUWA ILE CEREBRAL MARALIA AMBAYO NI KESI CHACHE.
Mifano hiyo ni live ya watu waliokuwa wazima kabisa na kuvuta pafu moja tu kwa mara ya kwanza na mabadiliko yakatokea ndani ya muda mchache
 
Bangi ni kama pombe inategemea kichwa chako kikoje. Wako wanaokunywa bia mbili tu wanalewa na wako wanaokunywa kreti zima bila ya kulewa.
Na bangi iko hivyo hivyo,wako wanaovuta na kuwa hivyo wako wengine wakivuta ndio wanaweza kufanya kazi kiufasaha na mambo mengine kiufasaha.

Kiufupi kila kitu kina kipimo chake kutokana na uwezo wa kichwa chako.
 
Mara ya kwanza kuvuta bangi,nilivuta mbali kidogo na home mwendo wa kama 20 hivi kwa miguui nauli ya daladala ni mia NNE,sikumbuki ilikuaje ila nilijikuta nipo home chumbani nmelala!!
Wengine wakishapuliza hakuna hesabu inawashinda.
Hii ni kweli kabisa,kuna jamaa nmemaliza nae 4m 4 alipata div 1.7 asingeweza kusoma bila kuvuta bangi,hapo badae alikufa kwa kansa huko Italy alikokwenda kumalizia masomo yake ya upadri..jamaa alikua jiniasi sana!!
 
Hizo ni comedy tu

Na sio kweli stori za kwenye kahawa usituletee
hivi ni vitu vilivyotokea mubashara kabisa enzi hizo. kwa walioshi mitaa ya kuchangamana sio vitu vya kushangaza. kati ya hao karibu zaidi ya robo nimewashuhudia na wengine wanasema wenyewe
 
d55a90635c3313268729207197144299.jpg

Wengine wanasema Hizi ni bangi. Ukivuta unakuwa na ROHO nzuri Sana ambayo inakuhamasisha kumtafuta mpk MUNGU. Ukivuta ukatulia utajionea maajabu ya MUNGU kuumba universe vuta bangi usiku.. Hayo ni maoni ya mdau mmoja mtumiaji wa bangi.. Toa maoni yako
 
hivi ni vitu vilivyotokea mubashara kabisa enzi hizo. kwa walioshi mitaa ya kuchangamana sio vitu vya kushangaza. kati ya hao karibu zaidi ya robo nimewashuhudia na wengine wanasema wenyewe
Huku nilipo kuna watoto vichwa ngumu panya road ,watoto 14,15,16,17,18 wanavuta kama vile wanakunywa maji na wanasema kawaida hawasikii chochote

mie naona ni stori za kufurahisha baraza ,mtu anaweza kuwa high lakini fix nyingi huwekwa kwenye mastori
 
Back
Top Bottom