Hivi bajeti ya Wizara ya Elimu ina Mpya Kweli?


Mgoyangi

Mgoyangi

Senior Member
Joined
Feb 6, 2008
Messages
184
Likes
3
Points
35
Mgoyangi

Mgoyangi

Senior Member
Joined Feb 6, 2008
184 3 35
Katika masuala ya Elimu walianza mababu zetu na mfumo imara ya Elimu, ambayo baadaye tukaiita, Elimu katika mfumo usio rasmi, lakini ndiyo iliyozaa wazalendo.

Ikaja Elimu ya Mkoloni, iliyojenga kuzalisha maafisa uchwara, wenye roho mbaya dhidi ya wenzao wanaojalio zaidi maslahi binafsi dhidi ya yale ya umma.

Tukawa na Elimu ndani ya Tanzania huru, chini ya dhana ya Elimu ya KUjitegemea, pamoja na kutoeleweka kwake, lakini ilikuwa na malengo mazuri na ikafufua ari ya uzalendo.Hii tulifundishwa na Nyerere, uliza hata watoto wake walisomea wapi utaambiwa.

Lakini sasa tukawa na Elimu yetu vichwa ngumu, wenye madfaraka yao wakafyeka unono na Elimu ikakosa damu na kuwa mahututi, ikashindwa hada kumudu penseli na daftari za wanafunzi, wenzetu wakaona kuwa njia ni kukwepa watoto wao wasisomee hapa wakaenda nje.

Hapa tukabaki walala hai,na ndicho kinachoendelea hadi sasa, shule hoi wanadai tunasonga mbele, sasa wanafuta mtihani wa darasa la nne na Form two, watoto wao wanasoma Ulaya, wa kwetu wanaendelea kuwa mbu mbu mbu.

Na kwa kuwa kupata kazi kunahitaji sifa za Kilemu, Mtoto wa Mlala hoi hatakomboa kamwe katika mzunguko wa Kimaskini.

Hivi hii bajeti ya Elimu iliyosomwa jana inajaribu kuangalia haya aua ndiyo inaendeleza matabaka na mipango mingi ya kuwajaribia watoto wa walala hoi?
 
BadoNipo

BadoNipo

Senior Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
175
Likes
14
Points
0
BadoNipo

BadoNipo

Senior Member
Joined Jul 4, 2008
175 14 0
Budget ya elimu kidogo imenifurahisha kwa kuongeza posho kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. zaidi ya hapo sijaona lingine jipya.
 

Forum statistics

Threads 1,237,905
Members 475,774
Posts 29,305,724