Hivi Bajeti ya 2019/2020 imetekelezwa ipasavyo? Hii ndiyo iwe ajenda kuu

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Bunge linategemewa kuahahirishwa na kuvunjwa halafu tunaingia kwenye uchaguzi mwezi Octoba mwaka huu.

Swali na muhimu kipindi hiki ni: je, bajeti ya 2019/2020 imefikiwa. Ahadi za serikali zimetekelezwa, na wewe mwananchi huduma za kijamii kama elimu, maji, afya, miundombinu ya barabara na umeme hapo kwako ni kwa kiwango gani?

Kimsingi, bajeti ndiyo kigezo na utendaji wa serikali kama utekelezaji wake uko juu ya wastani au chini. Ni kipimo cha uongozi uliotukuka kama wananchi wsmeweza kupata huduma zote za msingi. Ni kipimo pia cha utawala bora kama mahitaji muhimu yanapatikana kwa raia uishi bila kubughudhiwa au kunyimwa haki zao za msingi kidemokrasia.

Tujikite kwenye mjadala wa Bunge badala ya kutunishiana misuli kwenye vyama. Hapa tulipo naona ukiingia baadhi ya magroup utaona wazi hivi sasa ajenda kuu ni kauli za kufutiana vyama na uanachama. Hata ajenda ya corona sasa hivi si gumzo tena. Jamani, turudi kwenye issue za kitaifa. Kuwa na bajeti imara hata hili corona tunaweza kulidhibiti kwa sababu uchumi utakuwa stable.

Corona lipo,tuchukue tahadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom