Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,142
- 18,769
Amani na umoja wa Watanzania, ni sifa ambayo ilijulikana juu ya Watanzania duniani kote. Kwa miaka mingi sana Tanzania ilikuwa haitajwi na vyombo vya habari kama BBC na CNN kwa kuwa hatukuwa na habarai mbaya ambazo vyombo vya magharibi hupenda kuzitangaza juu ya nchi zinazoendelea na masikini. Tanzania wakati fulani ilikuwa ndio kisiwa cha kukimbilia wananchi wa nchi jirani wanapokuwa na matatizo.
Lakini mambo yalianza kubadilika taratibu, na katika awamu hii ya tano chini ya Raisi Magufuli, tumefikia hatua mbaya ambayo hatujawahi kufikia katika historia yote ya siasa za Tanzania. Kwa sababu za kisiasa, watu wanatekwa, wanauwawa, ofisi za serikali na vyama zinachomwa moto, chuki kati ya watanzaia ambao tullitana ndugu huko nyuma inazidi kukua kwa sababu tu za ufuasi tofauti wa vyama, hata tumefikia kuitana "adui" na sio ndugu tena!
Tunakwenda wapi?
Hivi kweli, iwe wewe ni mfuasi wa CCM, au chama cha upinzani, unaona yanayotokea Tanzania ni sehemu tu ya ushindani wa kiasiasa? Ni wendawazimu na ulevi gani umetuingia hadi tumefikia kuruhusu wajinga wachache waamue kuharibu uhusiano na undugu na umoja wetu kwa sababu tu za uchu wao wa madaraka na kujiona wao ndio wanajua kuliko sisi wengine wote?
Watanzania tufike mahali tujiulize, tunataka kufikia mahali tuwe na vurugu ndani ya nchi kati yetu wenyewe kama ilivyokuwa DRC? Zimbabwe? South Sudan? Rwanda? Burundi? Hivi tunataka kuonja machungu ya kuvunjika kwa amani kati yetu weyewe, tumekinai amani yetu kiasi hicho?
Natoa wito kwa Watanzania wote, uwe CCM au vyama vya upinzani, wakati wa kuvumilia kutenganishwa umekwisha, na sasa tukatae kugawanywa na watu wachache ambao wanajifanya wapo kwa maslahi yetu kumbe wanataka tu kututumia. Kama ikibidi, tufikie mahali tuwakane hawa wanasiasa wote, iwe CCM, iwe vyama vya upinzani, na kuonyesha kwamba tunataka kuanza upya katika misingi ambayo inatuweka pamoja kama Watanzania bila kujali huu ushabiki wa kitoto wa kisiasa uliopo sasa, ambao hatima yake huko mbele ni mbaya tu. Tufikirie sana tunaandaa mazingira ya namna gani wa ajili ya watoto wetu. Tuachane na ushabiki wa kisiasa wa kilevi tu kama watu tusio na akili timamu.
Ifikie mahali tuone kwamba mfumo wa kisiasa uliopo sasa umefeli, si upande wa CCM, si upande wa upinzani, na sasa tunataka kuwa na mwanzo mpya wa mfumo wa kisiasa hapa nchini ambao utatuunganisha kama ndugu badala ya kututenganisha na kutugombanisha. Kama ikibidi kuviua CCM na vyama vingine vyote vilivyopo ili tuanza upya, basi acha hilo litokee. Tukubali ukweli kwamba kama nchi yetu kwa miaka mingi imeshindwa kuendelea kwa kuwa ilifunikwa na ufisadi wa kutisha - hao ni CCM waliosababisha, na bado tunafikiri leo watabadilika? Na kama CCM waliendelea kutawala nchi kwa kifisadi bila bugudha, basi vyama vya upinzani navyo vimeshindwa katika kuidhibiti CCM na kuhakikisha Tanzania inaongozwa kwa misingi ya utawala bora. Upinzani ifikie wakati wakiri kushindwa, na CCM wakiri kuwa wao ndio wameharibu nchi yetu.
Tusiwaone watu hawa kama wakombozi, wote wana damu ile ile ya ufisadi, ya kutudangnaya, ya kutugombanisha, ya kushindwa kutuletea maendelea, ya kushindwa kuwasaidia watanzania wengi wanaokosa huduma za msingi za afya, maji, elimu nk. Wote wamefeli vibaya. Wamepimwa na hawafai. Wote wanajifanya wana akili kutuzidi watanzania tusio viongozi.
Tuamke!!!!