Uchaguzi 2020 Hivi bado tunaamini nyomi kubwa kwenye mikutano ya kampeni ndio dalili za ushindi?

WanaJF

Nafikiri mnaona jinsi kampeni zinavyoendelea kila sehemu mgombea huyu akipita watu wanajaa na wakiulizwa mtanipa kura wanasema “tutakupaaaaaaaaaaaa”. Akija mwingine hivyohivyo “mtanipa kuraaaaaa?” Wanajibu “ndiyo tutakupaaaaaaaa”

Walewale waliomuahidi wa mwanzo sasa wanakuahidi nawe hivyo mgombea usijidanganye kuwa kundi lote ni lako. Watu ni walewale cha msingi na cha kujiuliza ni ‘Je, walio tayari kupiga kura wapo wangapi miongoni mwao? Kumbukeni kura ni siri ya mtu!

Tundu Lissu asione watu wengi, wengine wanaenda kumshangaa tu kwamba kumbe ndiyo huyu alipigwa na manati mawe 16? Siyo wapiga kura hao, asije siku yanatangazwa matokeo aone ameonewa
 
Back
Top Bottom