Hivi bado kuna haja ya kuwasha mitambo ya DOWANS na masika yote haya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi bado kuna haja ya kuwasha mitambo ya DOWANS na masika yote haya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Mar 12, 2011.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tunapolazimishwa kuwasha mitambo ya DOWANS tunaambiwa umeme uliopo hautoshi kwakuwa mabwawa yamekauka!

  Hata hivyo majuzi nilipita maeneo mbalimbali nikielekea DSM. katika mikoa ya mbeya, iringa na baadhi ya maeneo ya moro mvua zilikuwa zikendelea kunyesha na mito ilionesha kuwa huko inakotoka mvua zilikuwa zikiendelea kunyesha maana maji yalikuwa mekundu kweli! labda dar es salaam ndiyo nilikuta kukame, nikadhani ndiyo maana watu wa dar walikuwa wakikubali kwamba hakuna mvua na hivyo mabwawa yamekauka kama wanavyosema watu wa serikali na kwama nchi iko katika hatari mitambo ya DOWANS isipowashwa.

  Kwa bahati nzuri, kwa mujibu wa vyombo vya habari hata Dar na maeneo mengine ambako mvua zilikwa zimeacha kunyesha, tayari imeanza kunyesha na sasa masika yanakaribia, hadi tukaambiwa huko sumbawanga daraja la kuunganisha huko na nchi jirani ya zambia lilisombwa na maji ya mvua kali zilizokuwa zikendele akunyesha.

  Sasa swali ni je, bado kuna hofu ya mabwawa kukauka na hivyo kuwepo haja ya kusumbua vichwa vya watanzania na kamati ya bunge ya nishati na madini kuhusu, kuwashwa kwa mitambo ya dharura, au tuendelee na mipango yetu mingine ya muda mfupi na muda mrefu ya kutatua tatizo la umeme, bila ya DOWANS?

  ikiwa bado kuna wanaotaka mitambo hiyo iwashwe kwa kisingizio hicho, nitachelea kuamini mkwamba kumbe hakukuwa na ukaukaji uliosababisha uzalishaji wa nguvu ya umeme kupungua na hivyo kusababisha mgao wa umeme nchi nzima.

  bali mafisadi, watoto wao na wasuka njama wao waliingia tanesco na kusuka dili kwamba sasa itangaze kwamba maji yamepungua na hivyo kuanzisha mgao ili watanzania wakubali mitambo hiyo iwashwe waweze kujilipa fidia kwa mlango wa nyuma.

  na kama hivyo ndivyo mungu akisaidia mvua zikaendelea kunyesha, na hivyo kuona wameumbuka, kuna hatari wakazusha jingine kwamba kuna hitrafu katika mitambo ya ruvu chini/juu au mtambo huu au ule ili mradi wazime umeme mpaka watanzania wanyooke na kukubali mitambo iwashwe!

  vinginevyo, wataalamu waniambie kipindi cha kuelekea uchaguzi miezi ya septemba na oktoba na wakati huu ni wakati gani mabwawa yalipaswa kukauka, maana kipindi kile amacho nchi ilikuwa kame hakukuwa na mgao kama ulioshuhudiwa kipindi hiki kwa kisingizio cha mvua!

  S
   
Loading...