Hivi baba wa Taifa angekuwa kama vijana wa sasa wa CCM, Tanzania Tungepataje uhuru?

Mara ya Mwisho mimi kusikia kijana au kiongozi yeyote wa CCM kuihoji au kukosoa serikali ilikuwa ni mwaka Juzi. Na hiki kitendo kilifanywa na Mbunge Bashe kabla hajapewa unaibu waziri akituhumu kuwa kwenye list ya wanaotaftwa na wasiojulikana sababu ya kukosoa serikali. Baada ya yeye kuingia kwenye system ( ya kutokuongea ukiwa unakula) na yeye kawa muimba nyimbo za sifa na Utukufu.

Mifano ipo mingi sana ya namna hii ukiangalia apo nyuma hasa awamu ya JK. Vijana wengi walihoji na kukosoa mwenendo wa serikali yao. Wengi walihoji hasa juuu ya Ufisadi na Matumizi mabaya ya kodi za watanzania.

Cha kushangaza, baada ya hawa vijana Type ya " Polepole" kuingia kwnye system na wao wakafyata mkia.

Sasa swali ni hili.

Hivi Baba wetu wa taifa angekuwa kama hawa vijana wa sasa wa CCM ( kigogo anawaita MATAGA), je Tungepata uhuru au Tungepataje uhuru?

Mnafikiri mabeberu hawakutafta njia tofauti za kumdhuru au kumhonga Nyerere ili aache chokochoko za kupigania uhuru? Kumbuka Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na hawa Mabeberu mpaka wakamfadhili na kumsomesha chuo cha Edinburgh nchini Uingereza ( 1952) lakini hakuwa mnafiki alipigani uhuru wa Watanganyika na kuhakikisha wanatuachia nchi yetu.

Ukiangalia hata mandela naye ivyo ivyo. Alikuwa mwanasheria na maisha mazuri tu ila alipigania uhuru wa nchi yake ingawa aliteswa sana na Mabeberu.

Uzalendo wa Baba yetu wa Taifa ndyo uliotufanya tupate uhuru. Ila Tafsiri ya uzalendo wa baba wa Taifa sio huu wa vijana wa CCm wanaotaka kuaminisha Watanzania.

Uzalendo Sio Kuipenda CCM,
Uzalendo Sio Kusifia Serikali,
Uzalendo Sio Kubeba Ilani ya CCM,
Uzalendo Sio Kuvaa Bendera ya Taifa,
Uzalendo Sio Kunyamazia unyanyasaji.
Uzalendo sio kunyamazia Ufisadi.

Uzalendo ni kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yako kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia.

Ukiangalia hii Tafsiri ya Uzalendo, kupata kijana au Kiongozi CCM mwenye huu uzalendo utamtafta kwa Toshi.

Ndugu ‘Zero Hours’, kwa kweli nakushauri upate utulivu wa nafsi ili uielewe dunia na binadamu vizuri. Binadamu ana uwezo wa fikra, kwa Kiingereza unaitwa ‘theory of mind’. Huu ni uwezo wa akili kutambua kijamii (cognitive social skill) kwamba binadamu wengine wanaweza kuwa na mtazamo, matamanio, imani, nia na uelewa ambao ni tofauti na wako wewe. Kwa hiyo basi, hawa watu wa CCM wana haki na wako sahihi kuwa na mtazamo na mawazo yao tofauti na yako wewe; na hiyo haiwapunguzii heshima au utu wao kama binadamu. Hata enzi za Mwalimu Nyerere akidai uhuru walikuwapo watu waliofikiri na kusema kwamba anawapotosha na kuwatoa kwenye njia sahihi ya kuleta uhuru - kama unavyodai kuhusu CCM sasa. Katika mifumo ya binadamu kujiendesha ndiyo maana kuna demokrasia ya wengi wape na wachache wasikilize. Sasa unapong’ang’ania kwamba CCM wanaipeleka nchi pabaya, basi kubaliana tu na ‘theory of mind’ ili tusikuite mjivuni na mbinafsi (neno zuri kwa Kiingereza ni ‘narcissistic’) mtu anayefikiri kwamba yeye peke yake ndiyo anaweza kuwa na mawazo mazuri na sahihi. Vinginevyo, tafuta chama mbadala cha siasa, wape sera zako nzuri, halafu zinadi kwa Watanzania ifikapo mwezi wa saba mpaka Oktoba. Kama wakikubali sera zako basi watakupeni kura za ushindi muwang’oe hao CCM. Kila la heri kwenye jitihada hizo.
 
Kiongozi nafikiri na wewe pia unaenda nje ya point...mtoa mada haongelei mambo ya kufikirika kama unavyojaribu kusema....matendo mzee....matendo.....utofauti wa itikadi na vyama vya siasa hautoi dhana ya ukweli...Ukweli na haki vitabaki ukwelu tu....ukweli na haki hauna demokrasia au maoni binafsi.....UKWELI upo hivohivo..uwe CHADEMA,CCM,CUF,ACT etc.....Watu kupotea, kuuwawa bila majibu ya serikali, waty kujeruhiwa....na majibu yabakosekana...

Haya ndio mambo ya msingi....KILA MTU KUWA NA HAKI YA KUISHI na KUFANYA CHOCHOTE AMBACHO HAKIVUNJI.SHERIA
 
Nadhani tungekuwa wote tunakula tunda kimasikhara na kufanya ngono sehemu hatarishi.

Chanzo kikubwa ni mfumo mbovu wa elimu.
 
Back
Top Bottom