Hivi baba wa Taifa angekuwa kama vijana wa sasa wa CCM, Tanzania Tungepataje uhuru?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,696
2,000
Mara ya Mwisho mimi kusikia kijana au kiongozi yeyote wa CCM kuihoji au kukosoa serikali ilikuwa ni mwaka Juzi. Na hiki kitendo kilifanywa na Mbunge Bashe kabla hajapewa unaibu waziri akituhumu kuwa kwenye list ya wanaotaftwa na wasiojulikana sababu ya kukosoa serikali. Baada ya yeye kuingia kwenye system ( ya kutokuongea ukiwa unakula) na yeye kawa muimba nyimbo za sifa na Utukufu.

Mifano ipo mingi sana ya namna hii ukiangalia apo nyuma hasa awamu ya JK. Vijana wengi walihoji na kukosoa mwenendo wa serikali yao. Wengi walihoji hasa juuu ya Ufisadi na Matumizi mabaya ya kodi za watanzania.

Cha kushangaza, baada ya hawa vijana Type ya " Polepole" kuingia kwnye system na wao wakafyata mkia.

Sasa swali ni hili.

Hivi Baba wetu wa taifa angekuwa kama hawa vijana wa sasa wa CCM ( kigogo anawaita MATAGA), je Tungepata uhuru au Tungepataje uhuru?

Mnafikiri mabeberu hawakutafta njia tofauti za kumdhuru au kumhonga Nyerere ili aache chokochoko za kupigania uhuru? Kumbuka Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na hawa Mabeberu mpaka wakamfadhili na kumsomesha chuo cha Edinburgh nchini Uingereza ( 1952) lakini hakuwa mnafiki alipigani uhuru wa Watanganyika na kuhakikisha wanatuachia nchi yetu.

Ukiangalia hata mandela naye ivyo ivyo. Alikuwa mwanasheria na maisha mazuri tu ila alipigania uhuru wa nchi yake ingawa aliteswa sana na Mabeberu.

Uzalendo wa Baba yetu wa Taifa ndyo uliotufanya tupate uhuru. Ila Tafsiri ya uzalendo wa baba wa Taifa sio huu wa vijana wa CCm wanaotaka kuaminisha Watanzania.

Uzalendo Sio Kuipenda CCM,
Uzalendo Sio Kusifia Serikali,
Uzalendo Sio Kubeba Ilani ya CCM,
Uzalendo Sio Kuvaa Bendera ya Taifa,
Uzalendo Sio Kunyamazia unyanyasaji.
Uzalendo sio kunyamazia Ufisadi.

Uzalendo ni kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yako kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia.

Ukiangalia hii Tafsiri ya Uzalendo, kupata kijana au Kiongozi CCM mwenye huu uzalendo utamtafta kwa Toshi.
 
Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
291
1,000
Vijana wengi wetu ni wachumia tumbo tu.... Huku vyuoni unakuta mtu anawaza tu namna ya kupata upenyowa kuingia kwenye system tu basi ili aweze kula.....zama hizi uzalendo unautafuta kwa tochi ndugu
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,696
2,000
Vijana wengi wetu ni wachumia tumbo tu.... Huku vyuoni unakuta mtu anawaza tu namna ya kupata upenyowa kuingia kwenye system tu basi ili aweze kula.....zama hizi uzalendo unautafuta kwa tochi ndugu
Umasikini unapozidi watu wnazidi kuwa wanafiki ilimradi wapate chochote wasukume maisha
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,696
2,000
Kundi lililopo hatarini ni kundi hili la ujana ... Yaani tunapelkwa kama bendera fuata upepo yaani
Hii ndyo type ya vijana tunaoongelea.
Screenshot_20200607-203052.jpg
 
Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,820
2,000
Kuna mzee mmoja humu huwa anaandika sana historia za matukio ya zamani lakini watu wanaishia kumzodoa tu,hebu turejea nyuzi zake halafu tuanze kulinganisha na picha ya sasa.
ila mambo ni moto mambo ni faya,mradi siku ziende.
ndo kilichobaki.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,553
2,000
Umeandika kitu kizito sana. Katika taifa hili la waoga na watu wa kujipendekeza, Mungu alitupa watu wachache wasio na woga (akiwemo Nyerere) ili tu watuletee uhuru. Mungu ni mwema sana. Nyerere alikuwa na kazi yake pale Pugu, akifundisha. Hebu fikiria na yeye angewaza tu tumbo lake na familia yake, kama hawa wa leo, akachagua kuendelea na kazi yake ya kufundisha. Basi Waingereza wangekuwa bado wapo mpaka leo.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,508
2,000
Mimi huwa nawaza kama Nyerere angeongoza kizazi hiki cha wanachadema katika kudai uhuru hakika wangemgeuka wakakumbatia wazungu.

Wewe ona sasa hivi Magufuli akijaribu kwenda kinyume na sera mbovu za mabeberu utasikia chadema tangu chini hadi ngazi ya juu wanalia machozi kabisa kwamba tutakosa misaada.

Shame on them aisee
 
Toa mfano wa sera tofaut na za Mabeberu ambazo magufuli kaenda tofaut nazo na faida zake kwa mtz?
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,696
2,000
Kuna mzee mmoja humu huwa anaandika sana historia za matukio ya zamani lakini watu wanaishia kumzodoa tu,hebu turejea nyuzi zake halafu tuanze kulinganisha na picha ya sasa.
ila mambo ni moto mambo ni faya,mradi siku ziende.
ndo kilichobaki.
Mkuu heb mtag tumjue
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,582
2,000
Mkuu punguza pumba kichwani, Uhuru ungepatikana tu hata kama Nyerere asingelikuepo. Au kuna nchi inayoendelea kutawaliwa na mabeberu kimabavu officially?
Muda wa kupewa uhuru ulikwisha fika na nchi zote zilipata uhuru haijaalishi walikua wanaongozwa na nani
 
Wewe ni wa kupuuza tu umeonesha upumbavu wako jinsi ulivyo wa hali ya juu.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
6,490
2,000
Sio kweli,uhuru ungepatikana tu kwa mtu mwingine au njia nyingine.
Umeandika kitu kizito sana. Katika taifa hili la waoga na watu wa kujipendekeza, Mungu alitupa watu wachache wasio na woga (akiwemo Nyerere) ili tu watuletee uhuru. Mungu ni mwema sana. Nyerere alikuwa na kazi yake pale Pugu, akifundisha. Hebu fikiria na yeye angewaza tu tumbo lake na familia yake, kama hawa wa leo, akachagua kuendelea na kazi yake ya kufundisha. Basi Waingereza wangekuwa bado wapo mpaka leo.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Mara ya Mwisho mimi kusikia kijana au kiongozi yeyote wa CCM kuihoji au kukosoa serikali ilikuwa ni mwaka Juzi. Na hiki kitendo kilifanywa na Mbunge Bashe kabla hajapewa unaibu waziri akituhumu kuwa kwenye list ya wanaotaftwa na wasiojulikana sababu ya kukosoa serikali. Baada ya yeye kuingia kwenye system ( ya kutokuongea ukiwa unakula) na yeye kawa muimba nyimbo za sifa na Utukufu.

Mifano ipo mingi sana ya namna hii ukiangalia apo nyuma hasa awamu ya JK. Vijana wengi walihoji na kukosoa mwenendo wa serikali yao. Wengi walihoji hasa juuu ya Ufisadi na Matumizi mabaya ya kodi za watanzania.

Cha kushangaza, baada ya hawa vijana Type ya " Polepole" kuingia kwnye system na wao wakafyata mkia.

Sasa swali ni hili.

Hivi Baba wetu wa taifa angekuwa kama hawa vijana wa sasa wa CCM ( kigogo anawaita MATAGA), je Tungepata uhuru au Tungepataje uhuru?

Mnafikiri mabeberu hawakutafta njia tofauti za kumdhuru au kumhonga Nyerere ili aache chokochoko za kupigania uhuru? Kumbuka Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na hawa Mabeberu mpaka wakamfadhili na kumsomesha chuo cha Edinburgh nchini Uingereza ( 1952) lakini hakuwa mnafiki alipigani uhuru wa Watanganyika na kuhakikisha wanatuachia nchi yetu.

Ukiangalia hata mandela naye ivyo ivyo. Alikuwa mwanasheria na maisha mazuri tu ila alipigania uhuru wa nchi yake ingawa aliteswa sana na Mabeberu.

Uzalendo wa Baba yetu wa Taifa ndyo uliotufanya tupate uhuru. Ila Tafsiri ya uzalendo wa baba wa Taifa sio huu wa vijana wa CCm wanaotaka kuaminisha Watanzania.

Uzalendo Sio Kuipenda CCM,
Uzalendo Sio Kusifia Serikali,
Uzalendo Sio Kubeba Ilani ya CCM,
Uzalendo Sio Kuvaa Bendera ya Taifa,
Uzalendo Sio Kunyamazia unyanyasaji.
Uzalendo sio kunyamazia Ufisadi.

Uzalendo ni kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yako kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia.

Ukiangalia hii Tafsiri ya Uzalendo, kupata kijana au Kiongozi CCM mwenye huu uzalendo utamtafta kwa Toshi.
Ondoa dhana kumkichwa kuwa mpaka leo tungekua tunatawaliwa.

Ndio mwanzo huo wa kumwabudu binadamu mwenzio.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,553
2,000
Hiyo ni kweli kwa Kenya lakini siyo Tanzania. Nchi hii imejaa ndumilakuwili wengi. Wote hawa wangekuwa upande wa mkoloni. Wangebeba mikoba ya wakoloni ili tu wapate pesa ya kushibisha matumbo yao.
Sio kweli,uhuru ungepatikana tu kwa mtu mwingine au njia nyingine.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom