Hivi Awamu ya Tatu ya uongozi ilikua chini ya chama gani? naomba mnikumbushe rais alikua nani?

mangia22

JF-Expert Member
Mar 10, 2017
447
185
HIVI AWAMU YA TATU YA UONGOZI ILIKUWA CHINI YA CHAMA GANI NAOMBA MNIKUMBUSHE NA RAIS ALIKUWA NANI?

Na: Dotto Bulendu

Watanzania msishangae haya yaliyoanikwa leo na Kamati iliyoundwa na Mh Rais John Magufuli kuchunguza mchanga unaosafirishwa nje ambapo imebainika kuwa makontena 277 tu yaliyochunguzwa ,serikali imepoteza zaidi ya shilingi Trilion 1.3.

Haya ni matokeo ya sisi watanzania kutoibana serikali,wabunge wetu kupitisha kila jambo linaloletwa na serikali hata kama lina madhara!.

Serikali kukosa mapato kwenye madini ni matokeo wataalamu wetu serikalini kutunga sheria za hovyo,za ajabu utadhani hii nchi haina wasomi wala watu wenye uzalendo!.

Mwaka 1997,bunge letu likipotisha sheria sa hovyo kwa hatinya dharura ,tarehe 26.3.1997 serikali ilipeleka muswada wa sheria mbili na bunge kuzipitisha,serikali ilipeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya kodi iliyofuta kodi zote kwenye sekta ya madini.

Tarehe 26.3.1997 ,bunge letu lilitunga sheria nyingine kwa hati ya dharura,sheria hii ni ile ya uwekezaji ambayo nayo ilifuta kodi zote kwa wawekezaji na kuwaruhusu wawekezaji waje kuchota alta utajiri wetu!.

Mwaka 1998,bunge likatunga sheria ya madini kwa hati ya dharura,madini yote yaliyopo nchini tukaambiwa eti siyo mali yetu,yaaani serikali na bunge zikasema wewe kama unamiliki eneo kwako ni juu tu,huku chini siyo kwako!.

Serikali yetu ilipeleka mapendekezo ya kutunga sheria kwa kiburi na jeuri,wabunge wetu wakapitisha sheria hizi kwa kejeli na kuzomeana wakadhani haya mambo wanawakomoana,leo wamesababisha mamilioni ya watanzania kuwa masikini!.

Haya yaliyowasilishwa leo kwa Rais Magufuli ni kiduchu tu,huko Nyamongo,Buzwagi,Geita na Mererani watu wamekufa,wamepigwa risasi wamehamishwa kibabe na kinyama kisa dhahabu!.

Mh Rais Magufuli,nenda Nyamongo watu wamebaki na ulemavu wa kudumu,wamepigwa risasi na askari ambao wanalipwa mshahara kwa kodi zetu!.Yaani mtu anatoka nje anakwenda Nyamongo anawaondoa watu kwenye maeneo yao waliyozaliwa hapo,unawaambia eti wewe unamiliki maeneo ya juu juu,chini kwenye madini siyo kwako!.

Kuna machungu zaidi ya haya ya leo,miaka yote yalitetewa na serikali zetu,pale Geita watu walihamishwa kama wanyama kutoka kijiji cha Mtakuja,wakapelekwa kukaa eneo la jengo la mahakama pale Sofia Town!

Watanzania waliokuwa wakimiliki ardhi wakabwagwa kama wanyama,walinyanyapaliwa na wawekezaji mpaka mkuu wa mkoa,wengine wakapoteza maisha,watu hawa walihamishwa na askari wetu,kinyama na kibabe etu kuwapisha wanaoitwa wawekezaji wachimbe madini!.

Mwaka 2009,Mgodi huu huu wa Acacia ukitiririsha sumu huko Nyamongo,watu wakababuka ngozi,wengine wakafariki,viongozi wa serikali kuanzia kijiji mpaka mkoa wakawaita watanzania wale wanyonge eti wavamizi wa mgodi,Nyamongo watu wameunguzwa na sumu,wamekufa kwa sumu na wengine kupigwa risasi na walinzi wa mgodi!.

Leo unakwenda Nyamongo,Geita,Kahama,Nzega,Arusha kwenye migodi mikubwa yenye utajiri mkubwa lakini watu wake ni masikini wa kutupwa!.

Serikali iwashtaki wawekezaji wote walio ua watu,waliowafanya walemavu kwa kisingizio cha eti wamevamia mgodi,wao wanapora mali za watu halafu wanataka wenye mali waishi kwenye nyumba za tembe!.

Miaka hiyo ya tisini viongozi wakubwa wenye heshima zao wakajiuzia mgodi wa makaa ya mawe kwa bei ya kaptula,nakumbuka Marehemu Dr Mvungi alikuwa anaongea kwa uchungu jinsi utajiri wa nchi hii unavyouzwa kwa bei ya kaptula!

Kiongozi wetu mmoja akajiuzia mpaka mgodi tena kwa bei ya kaptula halafu watanzania walidhani angewaletea ahueni wakabaki masikini,baadhi ya wabunge walioibua hiyo hoja walizimwa na kuitwa wasio na adabu!.

Mawaziri wetu wakasafiri mpaka ulaya kusaini mikataba ya madini Hotelini,walipohojiwa na Wabunge wakiongozwa na Zitto Kabwe ,baadhi waliungana na kufikia azimio la kumfukuza aliyelalamika waziri kusafiri mpaka ulaya na kusaini mkataba hotelini,matokeo ndiyo haya ya leo tuliyoyasikia!.
 
Ndio maana mkapa alituita malofa pale jangwani
Kweli mzee sisi ni malofa squared kwa haya ccm mnayotufanyia waTZ ccm ni zaidi ya shetani hiki chama cha manyang'au
 
Umesahau kuuongelea mgodi wa Almas wa Williamson Petra Diamondi wa Mwadui. Huu mgodi hausemwi lakini watu waliouawa na mngiki wa mzungu ni wengi sana. Raia wazungukao mgodi wanaishi kama watumwa nenda maeneo ya UTEMINI, MWANZUGI, MAGANZO na mengine yanayozunguka ujionee uonevu wa hawa watu. Eneo ni kame hakuna mvua ni nusu jangwa mazingira yanaharibiwa na hewa chafu toka mgodini, maji ni shida dhiki ni kuu sana. Maji yanatoka bwawa la Songwe lakini watu huwa wanaliona bomba tuu na ukiingia mwadui watu wake wanaishi kama wako nchi nyingine wengine ni hawa hawa watanzania wenzetu ndo hao wanatumika kuwapiga risasi watanzania na kuwazamisha kwenye tope zito kutoka mgodini. Watu wamezamishwa na wamepotea mpaka leo kuna baadhi ya ndugu hawajui watu wao wako wapi washakufa hao!!
Sitosahau siku Rais wa awamu ya.... (Siyo hii) alipotembelea mgodini akiwa na waziri wa kipindi kile ndugu....... (Jina linahifadhiwa) alikuja akapewa zawadi ya KOLEO(Chepe) ya Almas yaani full WHITE DIAMOND!
Ilikuwa ni hongo fulani ivi maana kipindi kile ndege ilikuwaga kila alhamis inaingia mgodini kuchukua Mzigo sijui kama kulikuwa na ukaguzi toka serikalini mana hata STAMICO wenyewe sidhani kama wanaujua hata uliko huu mgodi.
Marais wetu wa kipindi kile walikuwa wanakula sahani moja na hawa ambao leo wanaitwa WEZI..... Aibu yetu wenyewe!

Wamekosea na adhabu inawahusu toka kwa watanzania. Wajitadhimi na watuambie wameshindwa maana hatuwezi kuwaelewa kabisa.
 
vita hatari duniani ni
1. Madawa ya kulevya
2. Madini
3.Mabank
hata kifo cha KENEDY ni alipoanza kuwachokonoa mafedhuri katika sekta hizi hasa hiyo ya Tatu.... Nimuombee maskini mwenzetu magufuli aliyekata utepe kuondoa mifumo ya kifedhuri iliyojikita nchini mwetu ila tutambue usalama wake ni mdogo
 
Back
Top Bottom