Hivi asili ya Wameru wa Tanzania ni wapi?

Huu uzi watu wa kaskazini hawachelewagi kujiita asili yao ni Ethiopia na Uyahudi.
Mimi sionagi shida kwa wao kujiita chochote kwani hali add value yoyote kwenye makabila yao. Wote ni Watanzania kwa sasa msije tufukuzia South mwe.
 
Msisahau Kenya Pia kuna wameru, tena wanafanana exactly na wameru wa Tz, hadi kafudhi, culture na Lugha kwa kiasi, pia asili yao ni milimani, na pia ni kabila dogo huku but lina ushawishi. Wameru wa huku pia hata akija Tanzania akasema ni mchaga hakuna mtu atakataa kwa muonekano ni wachaga kabisa, maybe lugha itawatofautisha.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
Hata Kenya kuna watu wana majina ya koo za kichaga hii ni fact sababu nimewaona na kuishi nao Mkuu
 
Wameru na wachagga ni niĺotes toka Ethiopia,ni warembo na wasomï wasio yumbishwa
Hawa ni wabantu. Nilotes ni Maasai, Wadatooga (Wabarbaig), Wataturu, Dinker (Sudan), Karamanjong (Kenya), kalenjin (Kenya) n.k.
Ila asili yao inaweza kuwa Mlima Meru ya Kenya. Siyo Usambara Mountain.
 
Acha ujinga kama jambo hulijui ni vyema ukauliza na kuambiwa na wajuzi wa jambo lenyewe.Kimeru ni kimachame 100%.Tena baadhi ya koo zipo kote kote eg Urio,Urassa,Massawe.....
Hamna Mmeru URASSA au MASAWE
 
Ethiopia na Wairaq au Wambulu...hawa hata ukiwaona sidhani kama utakua na haja ya kuleta ubishani.

Kimuonekano na lugha yao itakufanya tu utafakari asili yao.
kabisa. Wairaqw ni Wakushi ambao asili yao ni Ethiopia.
 
Hawa ni wabantu. Nilotes ni Maasai, Wadatooga (Wabarbaig), Wataturu, Dinker (Sudan), Karamanjong (Kenya), kalenjin (Kenya) n.k.
Ila asili yao inaweza kuwa Mlima Meru ya Kenya. Siyo Usambara Mountain.
WADATOGA hawa jamaa ni harari sana, wanaishi na wahazabe hapa lake Eyasi, ni wazuri sana na damu yao ni moto.
 
Baada ya kuchoshwa na matukio ya awamu ya tano ngoja leo tujifunze kidogo kuhusu kabila la Wameru

Mpaka sasa hivi haswa sijafahamu asili ya hawa jamaa wengine wanadai ni machame but wa karibu zaidi na Wameru ni Waarusha na Wamasai kwa Magharibi na jamii ya wasiha kwa Mashariki

Maswali yangu ni haya:

1. Ilikuaje wakafika Arusha wakahamia wotee na lugha yao? maana kiasili nimeambiwa Arusha walikuja tu.

2. Nini kiliwafanya wakimbilie Arusha

3. Kwanini hawajiiti Wachaga wakati wanatumia lugha ya Kichaga?

Karibuni wajuzi

Somalia, Kaka wawili, toka somalia, mmoja alipanda machame mwingine Meru!
 
Lakini mbona wachaga na wameru wanasikilizana? Mmeru akiongea namuelewa mbona
Ni sahihi. Ila umeshasema ni mmeru na mchaga. Inawezekana huko nyuma walikuwa watu wamoja waka split. Mbona hata wachagga wenyewe hatusikilizani mkuu.

Wewe najua ni wa Siha je Mrombo unamsikia? Au Mmarangu?
 

Attachments

  • Screenshot_20221001-100032.png
    Screenshot_20221001-100032.png
    114.5 KB · Views: 25
Back
Top Bottom