Hivi Arusha mkoje?

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,029
1,191
Mwanamume mmoja aitwae Mango Sarakikya anaefanya kazi ya kupandisha watalii mlima Kilimanjaro amemaliza hasira zake kwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa anaesoma darasa la pili mara baada ya kutokea mzozo kati yake na mkewe.kwakua alinyimwa unyumba. Tukio limeripotiwa kituoa cha polisi Tengeru.
Katika tukio jingine mkazi mmoja wa mtaa wa Kambi ya Fisi hapohapo Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumueka kinyumba mtoto wake wa kumzaa na kumfanya mke wake.

Laana hiyo,ARUSHA MNA MATATIZO GANI?
 
Ubakaji: Zanzibar usiyoijua.....kwako yakhe Makamee


Na Talib Ussi. “JAMANI kwa kweli mahakama zetu zinarudisha nyuma juhudi za kupiga vita udhalilisha wa kijinsia. Kesi 60 jamani eti moja tu kati ya hizo mara nyingi ndio yaweza kupatiwa hukumu aaa [??] jamiii. Polisi na mahakama tushirikianeni ili tuondoe hili tatizo ambalo linatugusa sote.” Hiyo ni kauli ya Waziri wa Zanzibar wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar. Bi Zainab alisema kwa kipindi cha takriban mwaka — Julai 2012 hadi April 2013 — zaidi ya watoto wa kike 480 wamebakwa na watoto wa kiume 53 wamelawitiwa Unguja na Pemba.
Ama kwa upande wa kukashifiwa wanawake 273 na wengine 22 wametoroshwa kutoka kwao kwa wazee wao na wamefichwa kinyume na sheria.
Hali ya sasa katika visiwa vya Zanzibar ni ya kutisha kuhusu masuala ya ubakaji na ukatili wa wanawake.
Baada ya kuonekana kuwa athari zake zitakuwa kubwa katika kizazi cha leo Baraza la Wawakilishi lililijadili kwa muda mrefu suala hilo wakati wa mjadala kukhusu Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa Fedha 2013/14.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakari alitumia muda mwingi kujibu maswali ya Wawakilishi.
Waziri Bakari aliliambia Baraza hilo kwamba mwaka 2011 hadi Machi 2012 kati ya jumla ya kesi 5,477 zilizofikishwa katika mahakama mbali mbali 4,070 zilikhusika na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ubakaji.
Jumuiya mbalimbali za kiraia pamoja na Serikali zimefanya utafiti ili kujua chanzo cha ubakaji ni nini.
Kati ya Jumuiya hizo zilizoshirikiana na Serikali kupiga vita udhalilishaji wa wanawake na watoto hapa Zanzibar ni Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Kwa mujibu wa utafiti wa TAMWA vitendo 900 vya udhalilishaji wa kijinsia viliripotiwa, vikiwa pamoja na matukio 400 ya ubakaji, kati ya 2012 hadi April 2013 katika wilaya kumi za Unguja na Pemba.
Katika mkoa wa kaskazini Unguja vitendo 103 vya udhalilishaji wa kijinsia viliripotiwa lakini kesi 10 tu zikifikishwa mahakamani.
Kisiwani Pemba kesi 23 za ubakaji zimeripotiwa katika Mahakama ya Mkoa ya Chake chake, kuanzia mwezi Juni hadi Julai mwaka huu, hali ambayo inawatia khofu kubwa wanajamii kwa vile matukio ya ubakaji yanazidi kutokea siku hadi siku.
Akizungumza na Zanzibar Daima Online ofisini kwake mjini Chake Chake karani wa ufunguaji kesi, Abass Mwinyi Mkuu, alisema kuwa kati ya kesi hizo 23, Wilaya ya Chake Chake inaongoza kwa kuwa na kesi 13, na Wilaya ya Mkoani ikifuatia na kesi 10 .
Mwinyi Mkuu alisema kuwa kati ya kesi hizo 23, tisa tayari zimeshafutwa katika Mahakama ya Mkoa, kupitia vifungu tafauti vya sheria.
Alieleza kuwa, kati ya hizo tisa zilizofutwa, kesi sita za ubakaji zimeondolewa chini ya kifungu cha sheria 100 (a), kwa vile ushahidi uliotolewa ulikuwa dhaifu.
Karani huyo wa ufunguaji kesi aliongeza kusema kwamba kesi nyingine mbili zimeondolewa chini ya kifungu cha sheria 207. Kwa mujibu wa kifungu hiki walalamikaji wana mamlaka ya kuweza kuiondoa kesi Mahakamani kutokana na sababu zao wenyewe .
Alisema kuwa kesi nyingine moja imeondolewa chini ya kifungu 209 (1) cha sheria kwa sababu ya kupitwa muda wa kipindi cha upelelezi. Muda wa upelelezi wa kesi kama hizo ni miezi minne. Endapo muda huo unapita Mahakama ina mamlaka ya kuifuta kesi.
Kati ya kesi hizo 23 zilizoripotiwa kesi 14 bado zinaendelea kusikilizwa Mahakamani, alisema Mwinyi Mkuu.
‘’Kati ya kesi hizo hakuna kesi hata moja ambayo imetolewa hukumu, katika kipindi hichi hii ni kutokana na wanajamii kuwa wazito wa kutoa ushahidi katika kesi hizi ‘’, alidokeza .
Akizungumzia suala la kutoa taarifa kuhusu matukio ya ubakaji, Mwinyi Mkuu alisema kuwa, bado jamii ina mwamko mdogo wa kuweza kutoa taarifa polisi kuhusu matukio ya aina hiyo, kwa sababu ya watu kuoneana muhali.
‘’Kwa kweli suala hili linaonekana bado kuwa zito, hivyo wanajamii hubakia nyumbani na kuzisuluhisha wenyewe kwa wenyewe, hali ambayo inasababisha kuendelea kutokea kwa kesi hizi siku hadi siku’’, alisema Mwinyi Mkuu.
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Chake Chake, Khamis Ramadhan Abdalla, alisema kuna changamoto kadhaa ambazo zinawakabili katika kusikiliza kesi za ubakaji, ikiwa ni pamoja na mashahidi kukataa kutoa ushahidi.
‘’Kucheleshwa kwa upelelezi kupitia upande wa mashtaka hali ambayo inapelekea kucheleshwa kwa kesi kusikilizwa na kupelekea kuondoshwa bila kupatiwa uamuzi unaofaa‘’, alisema Hakimu huyo.
Hata hivyo aliwataka wanajamii kuwa na ushirikiano ili kuweza kupata ushahidi madhubuti wa kuweza kuwatia washtakiwa hatiani na kuwapa adhabu inayostahiki ili kuweza kuondoka kwa matendo hayo ya udhalilishaji hasa ubakaji .
Uchunguzi unaonyesha kuwa kesi za kuwadhalilisha wanawake hazifuatiliwi kwa makini na huondolewa kiholela mahakamani na polisi.
Kadhi wa Wilaya ya Chake Chake Daud Khamis Salim, alisema suala hilo litaendelea kuwepo kwa vile baadhi ya wanaume hawaujui wajibu wao n hawaifuati misingi ya dini ya Kiislamu.
‘‘Dini yetu imeweka wazi kila jambo, mpaka jinsi ya kuishi na wanawake katika jamii, na hakuna hata eneo moja lililoruhusu kuwadhalilisha na kuwafanyia vitendo vya ukatili kama ilivyo sasa’’, alisema Kadhi huyo.
Alisema suala la vipigo na kuwadhalilisha wanawake hasa hujitokeza kwa kasi baada ya wanandoa kuachana.
‘’Mimi hapa nimeanza kazi kama miezi sita tu sasa, lakini nimekuwa nikishuhudia mambo makubwa wanayofanyiwa wanawake na utadhani kwamba wafanyaji hawana dini, na mengine hayafai hata kukuelezea’’, alisema.

hivi zanzibar kunani?
 
Last edited by a moderator:
Acheni kula mirungi Arusha utambakaje mtoto kisa mama yake kakunyima unyumba?
 
Hlo ni janga ambalo linaloweza kutokea hata mtaani na wilayan kwako na cyo Arusha tu,ni janga la kitaifa mkuu afu wanaofanya hvo vitendo cyo watu wote wanaokaa Arusha!kumbuka kwenye msafara wa mamba na kenge pia wamo!watu wa Arusha ni wazuri tuuu!polen waliokutwa na usodoma huu
 
Hlo ni janga ambalo linaloweza kutokea hata mtaani na wilayan kwako na cyo Arusha tu,ni janga la kitaifa mkuu afu wanaofanya hvo vitendo cyo watu wote wanaokaa Arusha!kumbuka kwenye msafara wa mamba na kenge pia wamo!watu wa Arusha ni wazuri tuuu!polen waliokutwa na usodoma huu

Huoni jina hapo juu SARAKIKYA NI MMERU kabisa huyo. Bangi tu +mirungi
 
Kuna uwezekano mkubwa kwa ajili ya ugomvi wa wazazi hawa, mama kaamua kumchafua baba,ni simple mother kum-feed information za uongo mtoto kwa ajili ya kummaliza baba.believe me kunauwezekano huyo mtoto hajabakwa!chezea mtoto wa kike weye!hasa mkitofautiana!
 
Arusha ni mkoa wa kwanza unaoongoza kwa kilimo cha bangi ukifuatiwa na mkoa wa mara.

nafikiri nimejibu chanzo
 
Kuna uwezekano mkubwa kwa ajili ya ugomvi wa wazazi hawa, mama kaamua kumchafua baba,ni simple mother kum-feed information za uongo mtoto kwa ajili ya kummaliza baba.believe me kunauwezekano huyo mtoto hajabakwa!chezea mtoto wa kike weye!hasa mkitofautiana!

Mkuu hii sio tamthilia mpaka muda huu mtoto amelazwa hospitali ya mkoa Mt.Meru. Kamgeuza mbele na nyuma
 
Inasikitisha kwa kweli ukatilili wa aina hii kwa watoto mpaka lini?
 
Back
Top Bottom