Hivi aliyeruhusu wanafunzi wa sekondari kuvaa hijabu alijua madhara yake?

Status
Not open for further replies.
Kaka mi huwa sikejeli dini ya mtu. Halafu ujue mnachokosea nyie Waislam ni kudhania mna hati miliki ya Uislam. Uislam haumilikiwi na yoyote. Mtu yoyote mwenye mawazo huru anaweza kuusoma na kuuelewa vizuri tu. Mi nina rafiki zangu waislam na wao wanasema hawaamini chochote zaidi ya Quran. Mimi nakubaliana nao. Sasa wao kuna vitu wanaona vinalazimishwa na havipo kwenye Quran mojawapo ni hii ya kuvaa hijab. Ndiyo maana nimeuliza kwa wema tu ni aya ipi katika Quran inataka wanawake wavae hijab badala ya kujibu nyie mnaleta kejeli. Mimi sipo huko.
Acha chuki zakishamba!!!

We hijabu kwako inakutatiza nini mpaka utafutiwe andiko, kwanini usiende kumuuliza Sista kule kanisani akakupa jibu, au yeye kavaa kimini.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la hijabu kuvaliwa shuleni sisi wanaoona mbali tulishajua litaleta matatizo,

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba, Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni, vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?

Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,



Britanicca


Hapa serikali lazima ipige stop hili jambo kwani kuna madhara gani wanafunzi kuvaa uniform kama siku za nyuma? Shule ni shule na kuna ulazima kuwe na utofauti wa hilo, anayetak kuvaa kitambaa kichwani au misalaba shingoni afanye vile akishatoka shule, yaani akiwa katika mazingira ya nyumbani. Serikali ya Tanzania fanyeni la maana hapa, tusiache wanafunzi wetu wanapotoka hivi hivi.
 
Kuna mafundisho yoyote yanayo wataka waumini wa kikristo wavae majoho
punguzeni chuki za kidini
Hivi mnaishi vipi na majirani zenu waislam
Munapandikizwa chuki badala ya upendo
Hayo ni mafundisho ya kibinaadam
Hakuna mungu anaefundisha kuchukia wengine
Hivi kila mwanafunzi akivaa uniform kulingana na dini yake patatosha kweli?? Wengine nao watataka kuja wamevaa majoho ya kipadre!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna. Sasa na wewe nipe jibu kama kuvaa hijabu ni hitaji la dini ya Islam. Nipe Aya.
Suala la hijabu mashuleni ni bomu kwa Taifa. Huwezi kuwaonyesha watoto/ wanafunzi kubaguana kwa misingi ya dini hali unagenga taifa lenye umoja. Tumsaidie Mama Ndalichako kupiga kelele.analijua lakini anaogopa kushambuliwa na waislamu kumbukeni alivyokuwa baraza la mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza fuatilia kwann MASISTA WANAVAA VILEMBA?ukishajuwa itakuwa rahisi KUELEWEKA,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
Na mm nimekwambia kama hauwezi kujibu swali langu potezea najua wapo Waislam wengi sanaa wako rational na wanajua dini yao watakuja hapa watanijibu sio kwa mihemko kama wewe ila kwa maandiko. Kwa hiyo kama ww hauna jibu pita kimya tu. Sio ugomvi.
 
Daaaah kwa mawazo finyu kama haya nawe unajiita muona mbali. Hakuna muona mbali ambaye anaweze kuandika jambo ambalo hajalifanyia utafiti/tafiti na kupata maarifa ya kina. Acha mawazo mgando mwanamke sharti ajisitili. Na kama haufahamu ungeomba ujuzwe na wataalamu sio kukimbilia kuandika tena ktk side ya negativity
Suala la hijabu kuvaliwa shuleni sisi wanaoona mbali tulishajua litaleta matatizo,

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba, Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni, vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?

Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,



Britanicca

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watakuja wengine nao watadai.. Maeneo wanayoishi ni mjumuiko, kuna watu wa dini tofauti.. Nao watakataza matumizi ya adhana, kutumia vyombo vinavyotoa sauti wakati wa ibada. Watasema ni kero kwao.

Huwa mambo mpaka unayaona yanaandikwa humu yanaanza taratibu taratibu. Mdomo/mkono ni njia tu inatumika kuelezea kile kilicho moyoni kwa mtu. Nchi iko huru na vyombo vya maamuzi vipo fikisheni ombi lenu.

Ili lifanyiwe kazi, wao ndio walilipitisha halafu tuone natija yake ni nini baada ya hapo?
 
Kaka mi huwa sikejeli dini ya mtu. Halafu ujue mnachokosea nyie Waislam ni kudhania mna hati miliki ya Uislam. Uislam haumilikiwi na yoyote. Mtu yoyote mwenye mawazo huru anaweza kuusoma na kuuelewa vizuri tu. Mi nina rafiki zangu waislam na wao wanasema hawaamini chochote zaidi ya Quran. Mimi nakubaliana nao. Sasa wao kuna vitu wanaona vinalazimishwa na havipo kwenye Quran mojawapo ni hii ya kuvaa hijab. Ndiyo maana nimeuliza kwa wema tu ni aya ipi katika Quran inataka wanawake wavae hijab badala ya kujibu nyie mnaleta kejeli. Mimi sipo huko.

Naomba unisamehe mkuu kwa hii post "Nyie ndio wale hata dada zenu wakivaa chupi wakatembea barabarani "sawa tu"


Umeuliza aya ipi katika Quran inataka wanawake wavae hijab👇


Kuvaa Hijabu.

Katika utangulizi tumetaja kwamba, Qur'an inahimiza sana sana kuvaa Hijabu, na katika Aya nyingi za Qur-an umetajwa mkazo wa jambo hili, nasi tutataja baadaye baadhi ya Aya nyingi zinazohusu suala hili na kuzifasiri kwa kifupi.
1. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا

"Ewe Nabii, waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio, wateremshe shungi zao. Kufanya hivyo kutapelekea wao kutambulikana (kwamba ni wanawake waungwana) hawatakerwa ( na watu waovu), na Allah ni Mwingi wakusamehe (tena) Mwenye huruma".1
Katika Aya hii tukufu, Mwenyezi Mungu anamuamuru Nabii wake Muhammad (s.a.w), awaamrishe wanawake wa kiislamu wakiwemo wakeze, binti zake na wake wa waaminio, wajisitiri kwa kuvaa Hijabu iliyokamilika. Katika zama za mwanzo wa kuja Uislamu wanawake walikuwa wakitoka majumbani mwao bila kujisitiri miili yao kikamilifu, kama vile walivyokuwa wakitoka wanawake wa zama za Jahiliya (kabla kuja Uislamu). Hali ya kutokujisitiri kikamilifu kwa wanawake, haikuridhiwa na sheria ya kiislamu, ndipo Mwenyezi Mungu alipomuamuru Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) awaambie wanawake waumini wajisitiri na wavae Hijabu, na awakataze kutoka majumbani mwao bila sitara iliyokamilika kisheria. Akasema Allah s.w.t kumwambia Mtume (s.a.w.w), "Ewe Nabii waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio wateremshe shungi zao." Tamko (Jalabib) ambalo limetumika kwenye Aya ya hamsini na tisa, maana yake kilugha ni ushungi ambao hufunika kichwa cha mwanamke na uso wake na kumkinga asionekane kwa watukwani kwa mujibu wa sheria haifai kuonesha mbele yao baadhi ya sehemu za mwili wake. Bali ilivyo ndivyo, ni mwanamke asitiri sawa maungo yake kama sheria inavyomtaka kuyasitiri.
Ama maana inayopatikana katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: "Kufanya hivyo kutapelekea wao kueleweka (kwamba ni wanawake waungwana)" Kauli hii inalenga kufahamisha kuwa, Hijabu humfanya mwanamke atajwe kwa utajo wa wema, na katika jamii hupambika kwa sifa ya Uchamungu.
Ni mara chache Wachamungu kukumbwa na mikasa itokanayo na watu waovu, ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaendelea kusema katika Aya hiyo ya hamsini na tisa kuwa: "Hawatakerwa na watu waovu".
Hii inamaanisha kwamba, macho ya watu waovu, wajeuri na wenye khiyana, hayamfikii mwanamke ambaye amejisitiri kikamilifu tena kisheria, kwa kuwa vazi la Hijabu humlinda dhidi ya aina mbali mbali za uovu, hata kumfanyia maskhara (utani) huwa ni vigumu. Hijabu huwa inasitiri mwili wa mwanamke na kuufanya uzuri wake na mapambo yake kutoonekana, kwani (awapo ndani ya Hijabu) hakuna kinachoonekana katika mwili wake, na mwanamke huyo huwa amesalimika kutokana na shari za aina tofauti. Salama hii hupatikana kwa kuwa, muovu amuonapo na kumtambua kwamba mwanamke huyo ni Mchamungu, tena ni mwenye kujihifadhi barabara hushindwa kumtendea ubaya. Kwa hiyo katika Aya hii tukufu, tuna dalili iliyo wazi inayotujulisha kwamba, kuvaa Hijabu ni lazima, pia inatujulisha kwamba, Hijabu inamhifadhi mwanamke kutokana na ufisadi na aina nyinginezo za uchafu.
2. Mwenyezi Mungu anasema tena kwamba: "Namnapowauliza (kitu wakeze Mtume), waulizeni nyuma ya pazia, kufanya hivyo kutatakasa nyoyozenu na nyoyo zao".
Aya hii inawaamuru Waislamu wanapouliza au kuomba kitu kutoka kwa wake wa Mtume (s.a.w.w) waulize hali ya kuwa wako nyuma ya pazia. Hapa wametajwa wake wa Mtume, lakini matumizi ya amri hii ni kwa wanawake wote ambao sheria ya kiislamu hairuhusu kuonana nao bila ya kuwepo kizuizi kwa ujumla.
Maana inayojitokeza katika Aya hii, ni kupatikana wajibu wa kuwepo sitara, yaani Hijabu baina ya wanaume na wanawake. Siyo sawa wanaume na wanawake kukosa mipaka ya mawasiliano, lazima papatikane muongozo utakaoeleza mipaka hiyo.
Ndani ya Aya hii ya hamsini na tatu, Mwenyezi Mungu aliposema: "Kufanya hivyo kutatakasa nyoyo zenu na nyoyo zao". Kilichokusudiwa ni kwamba, suala la Hijabu kwa maana yake halisi ni jambo jema kwa pande zote mbili yaani wanaume na wanawake. Hapana shaka kwamba mwanaume anapomuangalia mwanamke, jambo hilo huamsha hisia za kijinsia, na kumpa shetani nafasi ya kumsukumiza mwanaume huyo katika mambo ya haramu na ufisadi. Na kwa upande wa mwanamke, pindi anapokosa kuwa ndani ya mazingira ya Hijabu, tayari huwa anaiweka heshima yake na utu wake katika hatari ambapo wakati wowote ule anaweza kuvunjiwa heshima yake. Hivyo basi vazi la Hijabu ni utakaso kwa wanaume na wanawake, na ikiwa kizuizi cha wanawake na wanaume kuchanganyika kitaondolewa, hali hiyo inaweza kusababisha ufisadi na fitna ndani ya jamii, mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyakataza na
Hali hii ya uovu ndani ya jamii inajitokeza kwa wingi mno ndani ya maeneo yasiyozingatia kanuni hii ya Hijabu2 msamiati unaoitwa mfadhaiko. Yote haya hayakuja kwa bahati mbaya, bali ni kutokana na kupuuzwa kwa mafunzo ya Mwenyezi Mungu na kuyapa mgongo. Basi ni kwa nini
Wakati huo huo ni lazima tufahamu ya kwamba, Mwenyezi Mungu ameyakemea maovu na ufisadi kwa aina zake na vyanzo vyake vyote.
Baada ya maelezo haya yatupasa tujiulize, je ni kwa nini Mwenyezi wakati akilielezea suala la Hijabu tamko lake akalielekeza kwa wakeze Bwana Mtume (s.a.w)? Jawabu lake ni kwamba, wakeze Mtume wanayo daraja maalum ndani ya jamii ya kiislamu, kadhalika wao ni Mama wa Waumini wote, na kwa ajili hiyo wanatarajiwa mno kuwa na ziada katika utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwa sheria muhimu ni hii kanuni ya Hijabu. Kutokana na ukweli huu, mwanzoni tu mwa Aya hii Mwenyezi Mungu ameanza kwa kusema: "Enyi Wake wa Mtume, ninyi si kama yeyote miongoni mwa wanawake".3
Maana ya maneno haya ni sawa na kumwambia mtu mwenye elimu, "Wewe Bwana ni mwanachuoni usiseme uongo". Sasa basi, maneno kama haya huwa hayamaanishi kuruhusu kusema uongo kwa asiyekuwa Mwanachuoni, bali maana yake ni kuwa sifa ya kuwa mkweli inamsatahikia mno mtu huyo na uongo kwake ni jambo baya sana. Bali ukweli ulivyo ni kuwa, jambo lolote ambalo huwa ni sababu ya mwanaadamu kuingia ndani ya makosa, huwa ni haramu kwa mujibu wa sheria ya kiislamu. Ni wazi kabisa kwamba, wanawake wengi walikuwa wakienda kwa wake wa Mtume (s.a.w.w) na kujifunza mambo mengi waliliyokuwa wakiyaona kwao.
3. Mwenyezi Mungu anatoa maelekezo zaidi anasema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ

" Na kaeni majumbani mwenu (enyi wanawake) wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionesha (mapambo yao) wanawake wa zama za Jahiliyya (kabla kujaUislamu).4
Ndani ya Aya hii mnapatikana amri ya Mwenyezi Mungu inayomtaka mwanamke kutulizana nyumbani mwake, ili ashughulikie masuala ya ndani miongoni mwake ni kuhusu ndoa yake na familia, ikiwa ni pamoja na kuwalea wanawe kwa malezi ya kidini na tabia nzuri.
Hii ndiyo maana sahihi ya wanawake kutulizana majumbani mwao. Na iliposemwa katika Aya hii ya 33: "Na wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionesha mapambo yao wanawake wa zama za kijahiliya." Maana yake ni kuwataka wanawake wa kiislamu wasitoke majumbani mwao kila inapobidi kutoka, bila ya kujisitiri sawa sawa kama walivyokuwa na tabia hiyo wanawake wa zama za jahiliya. Si sawa mwanamke kuonesha mapambo yake hadharani. Na inapotajwa mapambo, lazima ieleweke wazi kwamba mapambo ni kama vile hereni, bangili, mikufu n.k. Istoshe kwa vitu hivyo kuwa ni mapambo, bali mwanamke yeye mwenyewe bila kuongeza hereni au mkufu ni pambo. Kwa hiyo basi mwili wake asiuache wazi na kuufanya uonekane kwa kila mtu.
Kitu kingine muhimu kinachojitokeza katika Aya hii ni kwamba, Mwenyezi Mungu anamtaka mwanamke wa kiislamu apambike kwa sifa tofauti na wanawake wasio Waislamu katika mavazi na Uchaji Mungu. Hali hii ni kwa sababu wanawake wa kiyahudi, kikristo na washirikina huwa hawajilazimishi kufuata hukmu hii ya sheria ambayo ndani yake mna hekima nyingi . Wao hutoka bila kujali kulinda heshima zao kama wanawake na mapambo yao huwa wazi mbele ya kila mtu.
Suala la kutojiheshimu kwa wanawake wa kiislamu, Mwenyezi Mungu hapendezwi nalo, ndiyo maana akawatakia utukufu na heshima kwa kuwachagulia vazi litakalowasitiri na kulinda hadhi yao. Kutokana na maelezo haya, linapatikana fundisho ambalo linamtaka kila mwanamke alizingatie kuhusu namna ya kuvaa. Na iwapo mwanamke wa kiislamu ataacha kuvaa Hijabu na akaamua kuuacha wazi mwili wake, basi atakuwa kajifanananisha na wanawake wa kiyahudi kikristo na washirikina. Pia huonekana kama mtu anayekataa heshima na utukufu ambao Uislamu unamtaka awe nao. Si hivyo tu bali huwa anajisogeza taratibu hadi kwenye mwelekeo mbaya unaomchukiza Mwenyezi Mungu. Kuna hadithi isemayo kwamba: Mwenyezi Mungu alimpelekea Wahyi (ufunuo) Mtume fulani miongoni mwa Mitume wake akamwambia, "Waambie Waumini: wasivae mavazi ya maadui zangu, na wala wasile vyakula vinavyoliwa na maadui zangu, na wala wasipite katika njia wanazopita maadui zangu, (ikiwa watayafanya haya niliyoyakataza) basi nao watakuwa miongonimwa maadui zangu kama walivyo hao ambao nimaadui zangu." 5
Aya hizi tatu zimekuja kuzungumzia maana ya Hijabu, na kuna Aya nyingine nyingi kuhusu suala hili ambazo hatujazitaja ili kufupisha maelezo.
.
 
Maneno mengi ya nini mkuu. Wewe niwekee aya inayowataka wanawake wa Kiislam kuvaa hijab. Vinginevyo huo ni ubunifu wenu tu wa kwenye hadith. Mimi ni Quranist. Sisikilizi chochote nje ya Quran Tukufu.

Kaka mi huwa sikejeli dini ya mtu. Halafu ujue mnachokosea nyie Waislam ni kudhania mna hati miliki ya Uislam. Uislam haumilikiwi na yoyote. Mtu yoyote mwenye mawazo huru anaweza kuusoma na kuuelewa vizuri tu. Mi nina rafiki zangu waislam na wao wanasema hawaamini chochote zaidi ya Quran. Mimi nakubaliana nao. Sasa wao kuna vitu wanaona vinalazimishwa na havipo kwenye Quran mojawapo ni hii ya kuvaa hijab. Ndiyo maana nimeuliza kwa wema tu ni aya ipi katika Quran inataka wanawake wavae hijab badala ya kujibu nyie mnaleta kejeli. Mimi sipo huko.
Ni matumaini yangu kwamba nia yako ni njema coz' sikuja hapa kubishana na watu, hususani wanaopenda kutumia kashifa kwenye mijadala kama hii wakati dini zenyewe tumeletewa tu! Dini tumeletewa lakini bado wapo tupo radhi kutoleana maneno machafu na ya kejeli bila sababu za msingi!

Back to the topic! Je, Hijab ni uzushi tu au Quran, imeagiza?! Jibu utapata kwenye Sura ya 24, Aya ya 31 ambayo inasema:-
Na waambie wanawake waaminio kwamba wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, na wasidhihirishe uzuri wa sura zao wala mapambo yao isipokuwa yale yaliyo bayana katika hayo, na kwamba washushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe uzuri wa sura zao wala mapambo yao
isipokuwa kwa waume zao, au.
.....
Hata uki-Google English Version, utakutana na hii hapa:-
And tell the believing women to reduce [some] of their vision and guard their private parts and not expose their adornment except that which [necessarily] appears thereof and to wrap [a portion of] their headcovers over their chests and not expose their adornment except to their husbands, their fathers, their husbands' fathers,....
In short, aya yenyewe ndo hiyo hapo, na imetaja mwanamke anaweza kuwa kichwa wazi mbele ya nani! Kimsingi anaruhusiwa kudhihirisha uzuri wake pamoja na kichwa chake ama mbele ya mumewe au mbele ya watu ambao sharia hairuhusu kuolewa nao!
 
Ni matumaini yangu kwamba nia yako ni njema coz' sikuja hapa kubishana na watu, hususani wanaopenda kutumia kashifa kwenye mijadala kama hii wakati dini zenyewe tumeletewa tu! Dini tumeletewa lakini bado wapo tupo radhi kutoleana maneno machafu na ya kejeli bila sababu za msingi!

Back to the topic! Je, Hijab ni uzushi tu au Quran, imeagiza?! Jibu utapata kwenye Sura ya 24, Aya ya 31 ambayo inasema:-
Hata uki-Google English Version, utakutana na hii hapa:-In short, aya yenyewe ndo hiyo hapo, na imetaja mwanamke anaweza kuwa kichwa wazi mbele ya nani! Kimsingi anaruhusiwa kudhihirisha uzuri wake pamoja na kichwa chake ama mbele ya mumewe au mbele ya watu ambao sharia hairuhusu kuolewa nao!
Shukrani sana kaka. Wengine wanadhani kila muuliza swali anatafuta kukashfu. Kaka asante sana.
 
Mkuu britanicca, mbona hufananii na kashifa za kidini?! Hii thread haina maana yoyote Zaidi tu ya kuchochea chuki za kidini!! Kwa mfano unadai:-

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba,
Hijabu inavaliwa kichwani, sasa inafichaje mimba inayokuwa tumboni?! Hivi unafahamu maana ya Hijab kweli wewe?!
Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Hivi kabisa unaamini kwenye picha hii hapa chini hakuna uniformity?
Hijab.png


Hivi mabinti kama hao waliovaa hijab mtu wanamkera kera vipi?! Seriously?! Hivi kwa hiyo dressing code inatosha kabisa kuleta mjadala ambao kila mwenye utimamu anafahamu ni mjadala unaoweza kuhemusha hisia kali za kidini?!

Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni,
Kama wewe ni Mkristo basi bila shaka unafahamu ni namna gani maandiko yanavyosisitiza kwa Mkristo kuwa mkweli! Je, unaweza kutamka kwa yakini kabisa kwamab Wakristo wamezuiliwa kuvaa rozali shuleni?!
vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?
Hivi utakana vipi ukiambiwa lengo la mada yako ilikuwa ni kukashifu tu?! Kama hilo halikuwa ndio lengo lako, umetumia vigezo gani hadi kuweka hijab daraja moja na tunguli?! Tunguli ni ushirikina; ina maana kutokana na mafundisho yako unaamini kabisa hijab ni ushirikina?! Btw, suala la wapagani na tunguli linahusiana vipi?! Au sio tu hufahamu nini maana ya ajabu, inawezekana hufahamu hata Pagani ni mtu wa aina gani? Si ndio?!
Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,
Kwa kumbukumbu zangu, shule za serikali ziliruhusu kuvaa hijabu awamu ya Ali Hassan Mwinyi! Now tell me:-
1. Ni kwa kiasi gani Hijab zimeongeza ZERO kwenye shule za serikali?
2. Ni kwa kiasi gani na namna gani Hijab zimepunguza ufaulu kwenye shule za serikali?
3. Ni kwa kiasi gani na namna gani ufundishaji umekuwa mgumu kwenye shule za serikali simply because kuna wanafunzi wanavaa hijab?
4. Ni kwa kiasi gani na kwa namna gani shule za serikali zinakosa vyumba vya madarasa, madawati, vitabu, walimu wenye sifa na vitendea kazi vingine kwa sababu tu kuna mabinti wanavaa hijabu?
5. Hivi leo hii ukiambiwa utaje na uelezee matatizo ya elimu ya Tanzania, suala la Hijab utaliweka namba ngapi na utaeleza linakwaza vipi Elimu yetu?
6. Ni kwa kiasi gani na namna gani wanafunzi wasio Waislamu wanaathirika kwa baadhi ya wanafunzi wa Kiislamu kuvaa hijab?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom