Hivi Afrika wanaotaka mabadiliko ni Waarabu tu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Afrika wanaotaka mabadiliko ni Waarabu tu ?

Discussion in 'International Forum' started by uporoto01, Feb 12, 2011.

 1. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baada ya kuona harakati kubwa iliofanyika Tunisia,Misri na sasa Algeria kuna swali najiuliza hivi sisi watu weusi wa Somalia,Zimbabwe na nchi zingine raia wetu hawataki mabadiliko ? hivi raia wa Somalia hawawezi kusema vita sasa basi ? Hivi Mugabe hawezi kuambiwa mzee ulitukomboa lakini sasa pumzika tunahitaji mtu mwingine mwenye mawazo tofauti ? Museveni hawezi kuambiwa mzee hebu pumzika aje mtu mwenye mawazo mapya ?
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Tunakuja Mpwa, tunakuja, subiri, tumeshajifunza, utaniambia, I can even predict nchi ya weusi itakayoanza hili vuguvugu, and am convinced itakua ni nchi fulani ya ukanda fulani unaosifiwa kwa kitu fulani cha kijinga sana ambacho in reality hakipo..., We are coming, we are coming the sons and daughters of the Oppressed we are coming, yes we are coming with a common determination, we are coming, we gona shed no more tears, we gona fear no more,

  wanakuja, Wamachinga, wakulima kwa wafanyakazi, wanakuja, sichochei bali wanakuja, subiri uone, Kama jua angavu wakati wa asubuhi, ili kuleta nuru ya matumaini, wanakuja, si kizazi tena cha uongo na manyanyaso, hawatamwaga damu tena, bali vilio vyao na sauti zao ndio silaha yao kubwa, Wanakuja, wakubwa kwa wadogo, wale waliorundikwa kwenye madarasa kama kuku, wasiijue kesho yo itakuaje, wanakuja, wameshaunda na bomu, wanakuja, wasio na elimu, wasio na imani, wanakuja.

  lakini, wakati wakija, Mimi na wewe tutakua wapi? je si wakati wa sisi kujiunga nao, tusimwage damu, tumwage chozi, chozi litakaloijaza bahari, bahari itakayounda mawimbi, mawimbi yatakayokuja kwa nguvu kuliko Tsunami, Yes, Tsunami itakayondoa uonevu wote, Tunakuja, Na Jina langu likiitwa, na MIMI nitakuwepo. Karibu twende wote.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  At the moment, ndo walio onyesha kuhitaji mabadiliko! Nyie hata kwenye kura tu mnambwela mbwela!
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Moto ulionza Tunis na Misri hakuna wa kuuzima. Karibuni vijana wetu watatoka woga kwani wanajua kuwa hawana cha kupoteza. Karibu hata askari wetu walamba buti wataamka na kuona kuwa wao pia ni wahanga wa viongozi wasiotosheka, viongozi walio tayari kutawala mafuvu halimradi watawale tu. Hata huko Tunis na Misri askari walianza kwa kuua na kutesa, lakini punde wakagundua kuwa familia zao, watoto wao, majirani zao, marafiki zao, ni wananchi wanaodai haki zao. Karibuni umma utasimama, kwa sauti moja utasema: MPAKA HAPA BASI. INATOSHA! Hakutakuwa tena cha Mgabe wala Museveni, Gagbo wala Kabila, Kikwete wala nani na nani. Karibuni, si Afrika tu, bali popote ulimwenguni ambako kuna ukandamizaji, vijana watasema basi. Vijana ndio Taifa la leo, na wala sio la kesho kama wanavyokuwa wakituambia kila siku. Vijana watasimama imara. Wazee watajiunga. Wanawake, wanaume, wakubwa, wadogo, bega kwa bega. Nyuso za mashaka, matumbo yenye njaa, vichwa visivyo elimu, familia zilizogawanywa kiitikadi za kisiasa na kidini, kwa hasira lakini kwa dhamiri, wote watasema basi. KIla uwanja, kila kipembe, kila barabara, kijiji, mji, wilaya, mkoa...nchi nzima itajazwa na sauti moja tu: INATOSHA! TUMECHOKA! MMETUCHOSHA! Karibuni! Karibuni!

  Tusiogope mabadiliko. Mwanzo mgumu. Askari watauwa, lakini wanapouwa kumi watajazana laki; vibaka watapora, lakini wengine watasimamia maduka na mali za watu. Punde WOTE, SOTE, tutafahamu tunapigania niniKaribuni! Karibuni! Karibuni! Ole wao viongozi wasiotaka kubadilika. Vitawatokea puani. Karibuni! Karibuni! Tutaikomboa Afrika.
   
 5. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo letu sisi nikuwa kuna watu ambao wanafaidika na mambo yalivyo watakaa mbali na tutaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe. Sijui kama tunaweza kukaa pamoja mahali bila ya fujo na uhalifu bila ya sisi wenyewe kwa wenyewe kufarakana. Halafu pia kuna watu ambao japo wanataka mabadiliko wanaona kuwa kwa nini tuingie sasa miaka mitano ijayo tutajitahidi kubadilisha mambo. ( najua neno kuchakachua litaingia hapa) Lakini ndivyo wenzetu wengine wenye the so called democracy wanavyofanya) Wanasema tu in 4 years we gonna elect the person we like, hatumpendi huyu jamaa lakini tunaipenda nchi yetu hatutaki kuingia katika kuivuruga sasa mpe miaka minne tutachagua mtu tumtakaye.
   
 6. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili ni wimbi la mabadiliko...na limeanzia huko juu....linakuja huku chini...taratibu.....litafika tu...
   
 7. F

  Fahari omarsaid Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati huo mlala hoi ambaye anavaa fulana iliyochanika kwa miaka 4 halafu wa5 anapewa fulana mpya ya YANGA ataamka na kuingia kundini mwenyeki watawi shina ataamka na kuona kiwanja cha mpira alichokua anachezea mwanae kauziwa DENGU ajenge GODOWN hapo hapo mkaazi wa DAR atajiramba baada ya kuoga nakuhisi ladha ya chumvi mwili inayotokana na kuoga maji ya kisima na akidai maji ya RUVU ambayo yamekuwa history wakaazi wa uswahili watamtaka waziri wa afya awajibu 7bu ya kuwapa neti baada ya kuwapa ushauri nyenzo za kuuwa mazalio ya mbu
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  watu wanapenda mabadiliko uporoto lakini hawaanzi kujibadilisha wao.
  Bado wana uoga, matendo na tabia ni zile zile. Hakuna kitakachobadilika kwa dizaini hiyo.
  Tunataka vitu fulani lakini hatufanyi chochote kitakachopelekea tupate tunayoyataka.
  Tunawaza mabadiliko, tunayaongea na tukilala tunayaota ila yatakujaje yenyewe!
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nili tutafanya mambo haya na sisi muda unazidi kwenda na Fisadi Kikwete anazidisha madudu na ujinga wake
   
 10. s

  shosti JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  thubutu roho zetu nyeusi kama ngozi zetu:sick:
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ni kazi saana ku-mobilize UMA juu ya kufanya kitokee kama kilichojiri kaskazini mwa afrika. Viongozi wa upinzani wengi wao ni pandikizi za wanausalama, nadhani mnajua nini maana ya taasisi hiyo ya usalama. Hivyo kwa kila kitakahokuwa kikiendelea hakitofikia muafaka zaidi ya kusalitiana baina ya viongozi kwa viongozi waandaaji, ni jambo gumu saana kutekelezeka hapa kwetu.
  Mfano mzuri, rejeeni mchango bungeni wa mh.Mbowe katika mjadala wa khotuba ya rais jana,, tazameni historia ya mrema,, mrejeeni Dovutwa,, turejee siku matokeo ya uraisi kutangazwa...ambapo mh.Lipumba alitoa khotuba ya kukubali matokeo.
  Kuna yaliyo mengi ambayo ni aghalabu ku-mobilize jamii ya kitanzania kushawishika, na hata jamii ikishawishika bado itabakia ....aaah HATUWEZI KUMSALITI HUYO ALIYE JUU SI MWENZETU KIIMANI?
  Go east...go west, bado Tanzania haitowezekana katika wimbi hili.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  This is by far the word of inspiration and courage.Yes the time is coming where by all oppressed will raise and say enough is enough.
   
 13. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  inategemeana unaongelea nchi gani aisee, kama unaongelea misri, wale mabadiliko yao yamelalia zaidi kwenye muslim brotherhood wanaotaka kuing'oa selikali inayofanya urafiki na israel ili wao wakalie madaraka waungane na iran kuimaliza israel, kitu ambacho watajilaumu sana kwasababu si muda tutaona misri ikiharibika kabisa uchumi na utalii wake kwasababu ya kuingia vita na israel, kiti kitakachofuata muda si mrefu. ni kwasababu watapigwa kama watoto na uchumi wao utalegea sana. ukija algeria na tunisia, they are not sensible, huwezi kuilaumu selikali kwasababu ya maisha magumu, maisha magumu si sababu, sababu ingekuwa labda kuna viongozi waliotumia pesa kama hapa kwetu epa, na ufisadi, ila si maisha magumu....ukifanya kazi kwa bidii maisha magumu utayasikia tu. ciao!
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tutaishia kupelekwa hivihivi kama gari bovu, hakuna akayesimama wala atakayesema ikizidi ni lipservice ya humu humu. No one really has a gut for changes or taking that risk.
   
 15. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  waarabu wako tayari kwa mabadiliko na ushahidi ndio huo kule Tunisia na Egypt. Wabantu bado tuna akili mgando na ni waoga. Mfano Bongo, Zimbabwe na kwengineko
   
Loading...