Hitimisho: CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Angalia revolution za akina Mao ze dong , vradimir ilych Lenin.

Walikuwa na misimamo juu ya kile wanachokipigania.

Hata ukiwasima akina Karl max wanasisitiza juu ya falsafa inayeleweka.
Hizo falsafa za hao watu bado zinatenda kazi hadi sasa duniani. Nenda China kaangalie kama zaidi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa kingine nini cha Mao ze Dong kilichobakia. Hizo nadharia za Karl Max na Lenin zinafanya kazi kwenye nchi gani kama hata huko Urusi kwenyewe wameshazitupilia mbali?

Unawezaje kutoa mifano ya falsafa zilizoshindwa kuwa mfano wa kuigwa na CHADEMA?
 
It is time you mind your own business.Issue za CHADEMA tuachie wenyewe ,tutamjudge mtu kulingana na performance yake.

Hata huko Bungeni wewe mweneywe zaidi ya kutukana wabunge wa Upinzani,hujafanya chochote kinachoonyesha kwa watanzania wengine.

Ukiufunga mdomo wako utatusaidia sana wengi wetu.

Usituamulie mambo kutokana na mawazo yako.Badala ya kufanya kazi iliyokupeleka Bungeni uko Busy kupigana na watu wazima waliokuzidi umri kisa ni wapinzani.Shame upon you.Disgusting member of parliament

Msimamo wa watanzania walio wengi ni kwamba mpaka sasa hatujaona alichofanya JPM zaidi ya kuweka wapinzani wake ndani,na adui zake kuwafungulia mashtaka,kuajiri ndugu na jamaa zake hiki ndicho alichoweza kufanikiwa nacho.

Poor you
 
Utakuwa na utaahira mkubwa sana wewe. Mwinyi, Butiku, Kinana, Warioba na Kinana wote wamemzodoa dikteta uchwara hadharani kwa kuingiza nchi kwenye mkenge.

Pole pole anajua fika kama uchaguzi huru na wa haki basi Chadema inatwaa nchi lakini taahira wewe unakuja humu na akili yako ya kusadikika!

 
Juliana hivi tangu uingie bungeni zaidi ya kutaka alima mdee aongezewe adhabu na kuwafungulia wabunge wa chadema kesi ya kukudhuru kuna cha maana ulichowafanyia wananchi wa songwe Jitathimini na Mungu akusaidie hizi siasa za chuki azitakufikisha mbali muulize mwenzako machange yupo wapi leo
 
Hatari sana hii, Mbunge unakuja kwenye mitandao kupambana na Chadema kila kukicha huku Taifa lako likiwa moja ya nchi masikini kabisa duniani. Kifupi toka Tanzania imepata uhuru mpaka leo 2017 ni moja ya nchi masikini duniani, katika hili Chadema haituhusu.

Hiyo Elimu yako na madaraka yako uliyokuwa nayo ungekuwa bize kuanzisha mijadala itakayoweza kuisaidia Tanzania kuondoka na umasikini na watu wengi wakachangia kwa kutoa mawazo ungedhihirisha ukomavu wako kama kijana unayejielewa, sio kila mpinga CCM/Serikali ni chadema lahasha wengine ni wapiga kura tunaishi kwa ukweli na uhalisia.

Chadema hawana dola mama, wenye dola ni CCM na ndio wanaokusanya kodi za watanzania toka 1961..
Tuna muda wakupambana na mkusanya kodi na msimamizi wa kila kitu zikiwemo rasirimali zetu toka 1961.
 
Hizo falsafa za hao watu bado zinatenda kazi hadi sasa duniani. Nenda China kaangalie kama zaidi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa kingine nini cha Mao ze Dong kilichobakia. Hizo nadharia za Karl Max na Lenin zinafanya kazi kwenye nchi gani kama hata huko Urusi kwenyewe wameshazitupilia mbali?

Unawezaje kutoa mifano ya falsafa zilizoshindwa kuwa mfano wa kuigwa na CHADEMA?
Hakikisha umeelewa vzr ndio ujibu hoja. Mpaka mwaka 1945 china ilikuwa na uchumi mbovu kuliko hata Tanzania.
Lakn baada ya vita ya dunia ndio wakajitokeza wanaharakati kuanza kupigania mapinduzi. Msimamo wao ukikuwa ni kutokomeza unyonyaji na kuimarisha ujamaa.

Kutokana na mao kusisitiza mapinduzi ya kijamaa huku akiungwa mkono vzr na wakulima na wafanyakazi ndio iliyopelekea kufanikishwa mapinduzi yake.


Umeniuliza kuhusu chadema je Leo hii chadema wanazungmzia tena ufisadi?
Je zile casestud zake za ufisadi ambazo ambazo zilikuwa zikizungumzwa hazarani Leo anazingumzia tena?

Ukiwa mwlm unavyomfundisha mwanafunzi kuwa herufi A inasifa hizi akakuelewa na kesho tena ukaja kumbadlishia sifa za hyo herufi hataweza kukuelewa.
 
Miundombinu mibovu, Elimu bado duni, Huduma mbovu za Afya, Uchafu uliokithiri kwenye miji yetu, Umeme usiotoshereza, kushindwa kuutilize resources tulizonazo wenyewe, Ukosefu wa maji safi na salama, Shule za msingi za serikali hazina vyoo, Rushwa na wizi wa mali za umma umekithiri, Bajeti ya nchi haitosherezi, Nchi bado tegmezi kwa wahisani, Uwiano mdogo wa kuishi kwa mtanzania, kilimo duni, nk, nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk,nk..

Hayo yoooote hapo juu tukishirikiana kwa pamoja kupambana na watawala yataisha, ila tukiendeleza unafiki kama ulivyokuwa toka 1961 basi hayo matatizo yataendelea kuwepo milele na milele na yataendelea kutumika kama mtaji..

Ukiwa kama mbunge unayejielewa hayo kwenye paragraph ya kwanza ndio ingekuwa vita yako kila kukicha dhidi ya serikali kuanzia bungeni mpaka huku kwenye mitandao..

Kuendelea kupoteza muda na rasimali kupambana na chadema hakuwezi kumaliza matatizo ya watanzania, kama yale yoote kwenye paragraph ya kwanza yangekuwa hayapo basi tungekuwa na muda wa kupambana na Chadema, Chadema silaha yao kubwa na msingi wao mkubwa ni kwa CCM kushindwa kutekeleza yale kwenye paragraph ya kwanza..

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hili Dada lilimponda sana Dr. Slaa, Leo eti mbowe alimfukuza , uliyefukuzwa chadema ni wewe , Dr. Slaa hakuwahi kufukuzwa chadema alijitoa kwa hiyari yake. Kaa na Sana ccm wenzako wakufundishe siasa na uongozi la sivyo 2020 hiyo nafasi ya upendeleo utaisikia tu. Ukitaka upotee kwenye siasa basi sema hovyo upinzani , utadharaulika na jamii na itakupuuza kweli kweli. Mambo yamebadilika sana hakuna Mwananchi asiyejua nini kipo ndani ya vyama vya siasa , siasa za uongo wa kuwadanganya watu zimepitwa na wakati Dada.
Kama unaona chadema kuna shida , jiulize baba yenu amezuia mikutano ya hadhara kwa sababu zipi? Kwa nini ccm wanahofu chadema kuzunguka kufanya siasa?
 
Ukiwa mwlm unavyomfundisha mwanafunzi kuwa herufi A inasifa hizi akakuelewa na kesho tena ukaja kumbadlishia sifa za hyo herufi hataweza kukuelewa.
Mfano wa herufi na misimamo ya kisiasa haviendani hata kidogo. "A" ni "A" iwe leo ama kesho lakini kwenye siasa mtizamo unaweza kubakia ule ule lakini jinsi ya kushughulika nao kukabadilika. Kwa mfano China hadi leo bado wanajiita wajamaa. Unadhani Mao akifufuka leo atawaona hao wenzake ni wajamaa kwa tafsiri yake ile ya ujamaa aliyokuwa nayo wakati anaanzisha "Cultural revolution"?

CHADEMA bado wanazungumza kuhusu ufisadi na CCM bado wanasema kwamba ufisadi unaosemwa na CHADEMA si ufisadi. Huo unaosema ulikuwa unasemwa na CHADEMA kama ni ufisadi zama zile ndiyo ulikuwa unasemwa si ufisadi na CCM.

Leo CHADEMA wanasema ujenzi wa uwanja wa ndege Chato ni ufisadi, CCM wanasema si ufisadi. CHADEMA wanasema Rais anatumia hela nje ya bajeti iliyopitishwa na bunge na nje ya mifumo ya bajeti za serikali kwa ivo ni ufisadi, CCM wanasema si Ufisadi. hakuna siku CCM wanakubali kwamba wanafanya ufisadi mpaka ufisadi ufanyike na kuwafaidisha ndipo hutafuta mbuzi wa kafara na kusema kwama kulikuwa na ufisadi.
 
Kama kuchagua kusimama na vyama vya upinzani nikutokuwa na akili kwa mujibu wa Juliana Shonza, kama wenye akili ni wale tu wanaoiunga mkono CCM kwa kila kitu, kama viongozi wa nchi hii wanafikra kama zako, then sio CHADEMA yenye ombwe la uongozi bali nchi inaombwe la uongozi.. Sidhani na siamini kama kuna kiongozi duniani anae weza beza upinzani kama kweli anaitakia mema nchi yake..
 
Hivi Juliana Shonza ombwe la uongozi CHADEMA kwa nini linakuuma sana kama vile mtakatifu anavyowaona watu wakitenda dhambi? Ina maana Uongozi ni Mwenyekiti tu ama uongozi ni mfumo wa taasisi unaosimamiwa na watu?
Kama nia yako ni kutaka kuelewa naomba nikujibu kama ifuatavyo, kwa taasisi hasa taasisi ya kisiasa uimara wake na ubora unategemea maono na fikra za kiongozi wake wa juu kabisa kwa maana ya Mwenyekiti. Ndio maana wakati fulani msemo maarufu wa "Zidumu fikra za Mwenyekiti" ulitamalaki, unareflect ukweli halisi kuwa Mwenyekiti ndio moyo wa Chama cha siasa, akiyumba na Chama kinayumba na akiwa madhubuti na chama kitakuwa madhubuti.

Kuhusu kuumia, naomba nikujibu honestly CHADEMA kuna jasho langu, zipo nguvu zangu nyingi nilitumia kuhakikisha kinasimama na kinakuwa chama cha maana, nasikitika kuona wapo manyang'au wamevamia na kujitwalia chama iko wanajitangaza ugombea wa milele na hakuna wa kuwauliza jambo wala kusema kitu, naumia zaidi ninapoona mtu ambaye tulimuamini ameendelea kupotoka na kuwa wa hovyo. CHADEMA ni zaidi ya Mbowe, ni kubwa mno kuliko maslahi ya mtu na familia yake ndivyo tulivyokuwa tukiamini na kuaminisha wengine lakini manyumbu wamegeuza imani hiyo, wanaitumia CHADEMA kwa maslahi yao, wao ndio CHADEMA na CHADEMA ndio wao, hakuna nafasi kwa mawazo mengine, ama mtu mwingine kuleta mtazamo ama maono yanayokinzana na ya kwao. Hawa ni watu wanaopaswa kukemewa, na ndio maana nawakemea.
 
Blah blah blah...

Mnaacha kudiscuss matatizo ya nchi kama kufifia kwa democrasia nchini,viashiria vya udikteta,kupuuzwa kwa katiba,mihimili ya serikali kuingiliana kwenye kutimiza wajibu wake etc

Mnakazana na mambo ya chadema hivi, chadema vile.
Kwani kua chama kingine ndio tiketi ya kujitoa ufahamu, ifike kipindi hata kama hamna uwezo wa kufikiri basi walau mpretend mnaweza kufikiri.

Sasa umeandika nini hapa! mbaya zaidi unamhushisha Mungu na mambo ya mipasho,seriously!?!?

Jifunzeni kujenga hoja ili hata huko mjengoni muwe mnasupport mambo ya maana.
Huwa najifikiria sana inakuaje mtu kama kibajaji kila akiongea upuuzi watu wanagonga meza na kushangilia?

Leo nigundua tatizo hamna ma think tank...hamna watu wenye uwezo wa kuja na mada zenye maana na mantiki.
ukosefu wa uwezo wakujenga hoja zenye mashiko, outcome ndio andiko kama hili.
Wahenga wanao msemo wao maarufu, "nyani haoni kundule" Vijana wa ufipa mnazungumzia kukosa think tank..seriously..???
 
Siasa sio ajira, ukiingia kwenye siasa baada ya kukosa ajira basi athari zake huwa ni kubwa saana.

Kila mtu ana sababu yake iliyomfanya kuwa Mbunge, na kila mtu ananjia alizotumia kuwa mbunge. kuna wengine wametumia mbinu chafu sana zinazomchukiza Mungu kuwa Wabunge na kuna wengine pia wametumia njia halali zisizomchukiza Mungu, Nafsi yako ndio inayojua mtoa maada ulitumia mbinu gani kuwa mbunge na sababu ipi imekufanya kuwa mbunge...

Kila unachoonyesha kichwani ukiwa kiongozi ndio kinachotoa taswira ni sababu na mbinu ipi ilimfanya mhusika kuwa kiongozi, Dhamira na mbinu zilizotumia na mhusika kuwa kiongozi ndio chanzo cha matokeo chanya au hasi. Waliotumia mbinu chafu siku zote kuwa viongozi huwa hawana dhamira nzuri kwa ajili ya Taifa husika..

CCM inaongoza watu mil50+ leo 2017, na pia iliongoza idadi tofauti tofauti toka 1961, CCM ndio yenye deni kwa kushindwa kutatua kero za hawa mil50+. Kutatua kero za watu 50+ kunahitajika akili na mbinu zilizoshiba na si vinginevyo, Kupambana na Chadema ni kupoteza muda na kuonyesha udhaifu wa CCM kwa kutojua ni nini majukumu yake haswa kwa wananchi..
 
Mleta mada kuna mtu jana aliwataka wanachama na wanazi wa ccm waseme wanamaanisha nini wanaposema wapinzani hawana hoja. Je ww unaweza ukatuambia hoja ni nini, na ipi ni tofauti kati ya hoja na sera? Ukiweza kujibu hilo utatusaidia sana.

Halafu Juliana Shonza huwa tunakushangaa, huwa huchangii mada za wengine hapa jukwaani lakini ww hupenda kuleta mada ndefu zinazokufurahisha ww tu, bila kuingia kwenye mada za wengine. Je umegeuza hili jukwaa ni jalala la ww kuja kumwaga takataka zako kisha usichangie lolote mpaka pale unapokutana na neno linalokuuma ndio ujibu tena kwa jazba? Jitafakari.
Ndugu yangu, kama ni mtu mstaarabu utaelewa kwanini nimeanza thread yangu kwa kuomba msamaha na kuwataka radhi wanajamvi, ninayo majukumu mengi. Wakati mwingine majukumu hayo yananinyima fursa hii muhimu ya kuungana nanyi kwenye jukwaa hili.

MUNGU akiniwezesha kumaliza shule yangu vizuri na kukamilisha majukumu yangu ya ubunge, nitapata fursa ya kutosha ya kujadili hapa. Lakini kwa wito huo huo naomba uwaambie pia akina LEMA, LISU na wengine ambao nao huwa wanaandika na kupotea mpaka wapate wasaa mwingine wa kuandika upupu wao tena, tuwakumbushe pia.
 
Kuhusu kuumia, naomba nikujibu honestly CHADEMA kuna jasho langu, zipo nguvu zangu nyingi nilitumia kuhakikisha kinasimama na kinakuwa chama cha maana
Lakini sina hakika kama chama chako cha sasa (CCM) kinajua unaumia kiasi hicho kwa CHADEMA. Kwa maana nyingine kwa kuwa CCM hukuijenga basi hauna uchungu nayo kama CHADEMA ambayo una jasho na nguvu zako kwenye kuijenga!
 
Back
Top Bottom