Hitimisho bila utafiti ni uvivu wa kufikiri!-Dk slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hitimisho bila utafiti ni uvivu wa kufikiri!-Dk slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TONGINDI, Dec 14, 2011.

 1. T

  TONGINDI Senior Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hitimisho bila utafiti ni uvivu wa kufikiri!


  Wilbroad Slaa


  Ndugu Mhariri ni imani yangu kuwa utanipa nafasi nijibu baadhi ya hoja za Mayage zenye sura ya upotoshaji kwa manufaa ya wasomaji wako na Watanzania wenye nia ya kujua ukweli kwa ujumla. Ni imani yangu utachapisha majibu hayo kikamilifu ili upande wa pili wa shilling ufahamike kwa wasomaji wako na wananchi kwa ujumla..

  Mimi ni msomaji wa Gazeti letu la Raia Mwema na magazeti na mitandao mbalimbali hivyo kufuatilia mijadala mbalimbali. Kila nilipoona dalili ya upotoshaji nimekuwa nikijaribu kuweka kumbukumbu sawa. Siku za karibuni nimekuwa nikifuatilia makala zilizokuwa zikitolewa na Mayage S. Mayage kwenye Raia Mwema.

  Makala ya mwisho ilitoka katika Raia Mwema la Desemba 7 hadi 13, 2011, ukurasa wa 22. Baada ya kusoma makala yake ya kwanza nilimwandikia ujumbe mfupi wa sms. Kimsingi nikimshauri asipende kufanya mahitimisho kwenye mambo mazito na hasa yanayohusu jamii na taifa kwa ujumla bila kufanya utafiti.

  Kabla hata toleo la gazeti lililofuata halijatoka nikaanza kupokea simu na sms kutoka kwa watu waliojiita wapenzi wa CHADEMA, wakilalamikia ujumbe wangu wa sms kwa Mayage.

  Nilistuka sana na kujiuliza maswali yafuatayo; mosi, kama ni kweli waliokuwa wakiniandikia sms na kunipigia simu ni wapenzi wa CHADEMA walijuaje majibu yangu ya sms kwa Mayage, kabla gazeti linalofuata halijatoka? Je, walipewa na Mayage na kama ni hivyo, kwa lengo gani?

  Pili, lugha iliyotumika kwa wote japo walijitambulisha kuwa sehemu mbalimbali za Tanzania ilifanana na hakuna hata mmoja aliyejielekeza kwenye hoja ya msingi kuwa, Mayage ametoa hitimisho bila kufanya utafiti.

  Iweje wote wana lugha inayofanana walikaa wapi kujadiliana na kupanga ujumbe wa kunitumia? Iweje wote hakuna anayezungumzia hoja yangu ya msingi, bali msisitizo ni katika walichokiita "kumtukana Mayage? Hili nalo liliashiria upungufu mkubwa kwa kuwa hitimisho lisilotokana na utafiti wa kina daima lina upungufu mkubwa, hasa katika jambo zito kama mikakati ya chama.

  Je, watu hao walitarajia mikakati ya chama ingeliwekwa hadharani? Ni jeshi la ajabu linaloweka mikakati yake hadharani? Ni kwa msingi huo, nilitarajia Mayage kama ni mtu makini na mwenye nia njema kama anavyoonekana kutaka kutushauri, angelifanya utafiti aghalab angegundua mikakati au hatua kadhaa zinazochukuliwa na CHADEMA kujiimarisha na kujikita katika ngazi mbalimbali kwa lengo la kuchukua dola 2015.

  Je, Mayage anajua kuwa hakuna kanuni moja na inayofanana katika siasa kwa kuwa siasa "is a game of dynamics" yaani ni mchezo wa mbinu na mikakati.

  Hata hivyo, hata hao waliosema kuwa nimemtukana au kumdhalilisha Mayage, hawakueleza ni tusi gani ametukanwa. Kutokana na mazingira hayo, nimeona nitoe ufafanuzi ufuatao.

  Si mara ya kwanza
  Si mara ya kwanza tunajibishana na Mayage, baada ya makala au nyaraka zake. Kwa wale wanaokumbuka alikuwa akiandikia gazeti la Rai. Mayage aliwahi kuandika "Waraka wa wazi kwa Dakta Slaa" katika makala tatu mfululizo na zote zilikuwa za upotoshaji. Makala hizo zilikoma pale nilipomjibu kupitia gazeti hilo hilo.

  Katika barua zake hizo niliamini tatizo lilikuwa kutokufanya utafiti, lakini baadaye niligundua kuwa licha ya kutofanya utafiti Mayage alikuwa "kuwadi" wa waliomtuma kwa malengo waliyokuwa wakijua wenyewe.

  Jambo hilo alilikiri kwangu kwa sms Mayage mwenyewe, baada ya kuondoka Gazeti la Rai. Nami nikampongeza kwa unyofu na uwazi wake. Kama ni mkweli na mnyofu atatoka hadharani na kukiri mawasiliano kati yetu.

  Kwa nini niliandika sms
  Niliposoma makala ya Mayage katika Gazeti la Raia Mwema, kwa kutumia saikolojia tu ya kawaida nilijua alikokuwa akielekea ndiyo maana nikamtumia sms bila kutaka kumjibu kwenye gazeti ili ajirekebishe kabla hajafika mbali.

  Kwa bahati mbaya, nia yangu njema kwa Mayage ikaanguka kwenye jiwe gumu, badala ya kuanguka kwenye udongo wenye rutuba. Hii haikuwa kwa bahati mbaya, kwani wakati anaanzisha safari ndefu ya makala zake alikuwa anajua alitaka kuhitimisha vipi.

  Hii imeonekana dhahiri katika makala yake ya sasa "Ombwe….mbadala wa CCM ni chama kipya". Mengine yote ni kisingizio tu.

  Hoja anazotoa kwetu
  Hoja zake ni kwanza, CHADEMA ijikite zaidi katika "kufanya siasa badala ya uanaharakati wa maandamano". Pili, wabunge wa CHADEMA wanatakiwa kuja na programu za maendeleo kwa wananchi wa majimbo yao "ili yasije yakakikuta yaliyokikuta chama cha NCCR-Mageuzi.."

  Tatu, katika makala yake ya wiki iliyopita yenye kichwa cha habari "Sababu tunayo, tuwang'oe 2015", alitoa sababu mbalimbali na hatimaye alitoa "ushauri kwa wazalendo wenye uchungu wa kweli ….kuanzisha chama cha siasa makini sasa, si kusubiri kesho na Watanzania wakiunge mkono kwa nguvu zote…"

  Majibu kwa hoja zake
  Mimi sina tatizo na ushauri wa kuanzishwa kwa chama kipya kwa kuwa ni haki ya kikatiba ya Watanzania. Msingi wa kumtaka Mayage kufanya utafiti ni katika upotoshwaji dhahiri wa Mayage, ambaye kwa ufundi mkubwa amejenga hoja kinzani (fallacy) inayoonyesha kuwa CHADEMA si chama makini, hakifanyi siasa makini bali kinafanya tu uanaharakati. Huu ndio msingi na kiini cha kumtaka bwana Mayage afanye utafiti kuhusiana na hoja zake.

  Kama hoja za Mayage kutaka kianzishwe chama kipya inatokana na hoja za Richmond, ufisadi na sasa Jairo, na kama angelikuwa makini kidogo na kufanya utafiti kidogo tu angeligundua ni kiasi gani CHADEMA ni ‘chama makini' hadi kujitosa MwembeYanga, Septemba 15, mwaka 2007 na kuibua hadharani (baada ya jitihada za kutumia Bunge kushindikana), hoja za ufisadi wa Benki Kuu, EPA kwa ujumla wake, Twin Tower ya Benki Kuu, Kagoda, Ufisadi kupitia Commodity Import Support (CIS) na nyingine nyingi.

  Inatosha kufungua kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) za mwaka 2007/2008/2009/2010. Msomaji na mfuatiliaji makini anaona wazi kupitia hansard jinsi Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alivyokuwa akipigwa "point of order" kutakiwa kufuta sehemu ya hotuba yake na Spika, bila shaka kwa lengo la kuuficha ukweli usijadiliwe bungeni.

  Mayage atakumbuka jinsi Spika wa Bunge, Samuel Sitta alivyokimbilia TBC1 na kutangaza kuwa "Nyaraka alizokuwa nazo Dokta Slaa (kuhusu ufisadi) ni feki na kuwa anaziwakilisha polisi ashitakiwe".

  CHADEMA hatukutetereka
  CHADEMA ilishikia bango bila kutetereka, pamoja na vitisho na matusi yote hoja hizi sasa zinajulikana, taifa zima leo linajua ufisadi mkubwa unaokumba nchi yetu katika nyanja mbalimbali.

  Leo taifa nzima linaimba na kupinga ufisadi. Hii iliwezekana tu, kwa kuwa baada ya jitihada za bungeni kushindikana CHADEMA, kwa kukodi helkopta ilipita kwenye makao ya mikoa 12 ya Tanzania Bara na kupeleka hoja hizo kwa wananchi, kama Mahakama Kuu kuliko zote kwa wanasiasa. Mzunguko huo ulihitimishwa MwembeYanga kwa kutaja hadharani majina ya mafisadi 11.

  Mafisadi wengine wako kortini
  Hakuna anayebisha, na hata Mayage atakubali kuwa wengine kati ya watuhumiwa hao wa ufisadi leo wako mahakamani kwa kesi zinazohusiana na ufisadi huo.

  Mayage anasema CHADEMA kinafanya kazi "ki uanaharakati" angelifanya utafiti kidogo tu angelijua matokeo ya uanaharakati huo kwa siasa za CHADEMA na kwa siasa za Tanzania baada ya MwembeYanga.

  Kwenye sms niliyomtumia nilitumia neno kwa mtu yeyote anayefikia hitimisho (conclusion) bila utafiti ni ‘uvivu wa kufikiri' na bado nitasimamia hapo kwa kuwa kuacha hoja ya Mayage bila kupata majibu ya kina tutaruhusu upotoshaji unaozidi viwango vyote.

  Aidha, Mayage ameshindwa kutoa tafsiri ya neno ‘siasa' badala yake anaona kinachofanywa na CHADEMA ni ‘uanaharakati' tu, na hivyo anawashawishi "Watanzania kuanzisha chama cha siasa makini".

  Waanzishe chama makini siyo kwa kuwa chama hicho kipya kina ajenda mpya bali kwa vile tu CHADEMA si makini na kinafanya kazi "ki-uanaharakati".

  Mayage anashindwa kuchambua kwa kina uhusiano wa karibu sana kati ya uanaharakati na siasa. Anashindwa kuona kuwa uanaharakati inaweza kuwa mbinu mojawapo (wakati mwingine ya lazima) ya kufikia malengo ya kisiasa.

  Hoja ya Mayage ingekuwa na mashiko angelikuwa amepitia mikoa yote 12 ambako CHADEMA ilifanya mikutano ya hadhara (uanaharakati) na kulishitaki Bunge kuhusiana na ufisadi wa Buzwagi, hoja ya Kabwe Zitto iliyolifanya Bunge kumfukuza Zitto, bungeni kwa miezi takriban mine, na kuwaeleza kinagaubaga Watanzania ni nini matokeo ya mikutano hiyo kwa Watanzania na matokeo yake (impact) kwa siasa za Tanzania leo. Bwana Mayage alipaswa kukumbuka msemo kuwa bila "utafiti hakuna haki ya kuzungumza"(No Research no right to speak).

  Itaendelea
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,506
  Trophy Points: 280
  Tongindi, mbona hii issue tayari ipo?. Mode iunganishe kule.
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nakuheshimu sana Dk na nisingependa nami nihitimishe kabla wewe hujafanya hivyo lakini kumbuka ''ANAYEJISIFU KWA ALIYO YAFANYA JANA, LEO HAJAFANYA CHOCHOTE''
   
Loading...