:Hitaji La Tax Clearance Kikwazo Maendeleo ya Wafanyabiashara/Wajasiliamali

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Nchi yetu bado ipo nyuma sana kiuchumi hivyo bado ni moja kati ya nchi maskini zaidi duniani.
Tatizo la ajira limetoa fulsa ya wengi kujiajiri katika sekta rasmi na zisizo rasmi kama biashara na ujasiliamali.

Elimu ya ulipaji kodi,mfumo wa ulipaji kodi hasa kwa wanaoanza biashara au kujiajiri na kuwa tayari kurasimisha biashara bado una mapungufu makubwa na ni kigingi katika maendeleo ya wananchi maskini.mathalani:Hitaji la kulipa kodi ya mapato katika hatua ya usajiri wa biashara husika kupitia makadirio ya mapato.

Kumekuwepo na hitaji la wafanyabiashara/wajasiliamali {wapya,wa zamani,wakubwa,wadogo} kutakiwa kupata TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili waweze kupatiwa leseni mpya waanzapo biashara au mwaka mpya wa kibiashara unapowadia.. Hili ni tatizo linalonyong'onyesha wafanyabiashara wengi hasa wadogo na wa kati kutokana na ufinyu wa ufahamu katika masuala ya usimamiaji mapato,mahesabu,matumizi na biashara kwa ujumla .lakini pia mara nyingi figisufigisu za baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato {TRA} kuwafanyia makadirio makubwa yakiambatana na vitisho ili kushawishi rushwa kutolewa.

Maendeleo ya kiuchumi ya taifa lolote msingi wake ni wafanyabiashara/wajasiliamali/wenye viwanda wadogo,wa kati..Taifa letu haliwezi kuendelea kwa viongozi wa kisiasa/serikali/TRA kutunga,kusimamia,kutekeleza sera /sheria kandamizi ama zisizo rafiki kwa wadau..yatupasa kulitazama hili kwa jicho la saba tukiiga nchi kama China,Thailand,Brazil,India ambako kutengemaa kwa uchumi kumesababishwa na mchango endelevu wa sekta ya wafanyabiashara/wajasiliamali katika viwanda vidogo na kati.

Mapato mengi ya muda mfupi yasiwe chachu ya kuua kiu,nia,dhamira,malengo,ndoto,jitihada,ubinifu ambavyo vingeweza kulelewa na kuwa na manufaa makubwa kwa vizazi na vizazi kama kina Mercides benz,Tata,Hitachi,Sony,Toyota,Boeing,Bell,Ipp,Cocacola,Pepsi,....

Urasimishaji wa biashara nchini Tanzania ni zoezi linaloendelea na lenye tija katika ukuaji wa uchumi na maongezeko ya makusanyo ya mapato kama kodi,ushuru,na malipo mbalimbali.Elimu zaidi inatakiwa ili kuwaelimisha wengi,kuwawezesha wengi na kuwasaidia wafanyabiashara wadogo-kati,wajasiliamali kukua na kuchangia pato la serikali na ustawi wa taifa sasa na baadae.
 
Mbona tax clearance unapata tu ndani siku moja kama unalila kodi? Cha msingi ni kujua utaratibu tu.
 
Kwani tatizo li wapi ukilipa kodi na hudaiwi unapata hiyo TAX CLEARANCE CERTIFICATE bila shida.ipa kodi kwa maendeleo ya Taifa,bila hivyo tuache kusema ''serikali isaidie''itasaidia na nini kama hatupendi kulipa kodi kwa kutoa visingizio lukuki?
 
Mfanyabiashara mdogo makadirio huwa hayazidi 3000000 kwa Mwaka na hiyo unalipa kwa Awamu Nne
Ukishalipa ya awamu ya Kwanza unapewa Tax C yako ukaendelee na mengine
Wamefanya hivo maana watu walikuwa hawalipi kodi
 
Back
Top Bottom