Hitaji la kufufua uchumi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hitaji la kufufua uchumi wa Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Jan 27, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF,

  Natumaini kila mtu anajua uchumi wa Marekani na wa dunia umekumbwa na Misukosuko.

  Mataifa makubwa yamepata madhara makubwa ikuwepo viwanda kufungwa kutokana na kukosa wateja, nakadhalika.

  Raia wengi wamepoteza ajira.

  Mataifa mengi ikiwepo Japan, Marekani, Uingereza na nchi nyingine wameanza mkakati maalum wa kufufua uchumi unaitwa 'Economic Stimulus'.

  Bila Shaka Tanzania kwa ujumla tutapata madhara makubwa ikiwepo kupungua kwa utalii.

  Moja wapo ya hatua zinazochukuliwa na Serikali za nje ni (1) Kupunguza matumizi ya Serikali (2) Kukata mishahara ya wafanyakazi angalau kwa asilimia 15.

  (3) Kupunguza kodi kwenye sekta za uzalishaji hasa viwanda vidogo ili watu wengi zaidi wazalishe.

  Kwa hapa Tanzania nini kifanyike???? Changia tafadhali.

  - Kupunguza manunuzi ya vitu ambavyo si muhimu kwa kukua kwa uchumi kama Mashangingi.
  -Kupunguza kodi ya mafuta (Petroli na Diseli) Hapa serikali itakosa mapato, kiasi ambacho serikali itakosa mapato itafidiwa na hela zilizopatikana kutokana na kuepuka manunuzi yasio na umuhimu,

  -Kuweka vivutio katika uwekezaji. Mfano Ndege za Kimataifa hazitui Kilimanjaro Airport kutokana na Landing fee kuwa kubwa.
  Tujiulize kwa nini ndege nyingi zinatua Jommo Kenyatta International Airport - Nairobi na Moi Airport (mombasa), kwanini sisi tushindwe wao waweze
  -Kupunguza viingilio katika mbuga za wanyama kwa muda huu
  -Kupunguza bei za vyumba kwenye Hotel za Kitalii, mfano Sopa Lodge na Serena Lodge Masai Mara Kenya bei ni Rahisi sana ukilinganisha na Sopa Lodge na Serena Lodge Serengeti na Ngorongoro????

  -Kuokoa pesa zinazoliwa na mafisadi??

  - Kutunza mazingira kwa kupanda miti na Kutunza vyanzo vya maji. Hivyo mito na chemichem zitakuwepo kama miaka ya 1980 hadi 1990 ambapo kutakuwa hakuna ukame. Pia kilimo cha umwagiliaji kitawezekana.

  -Pia katika kupanda miti ajira nyingi itapatikana kwa form four leavers, darasa la saba. Pia wanavyuo watapata ajira za kweli. Ukiangalia katika miji yeyote machangudoa wameongezeka, wezi, vibaka, majambazi wameongezeka. KWa sababu hakuna ajira mpya kwa Grass root level (la saba na kidato cha nne). Katika kuwekeza katika kilimo na kupanda miti.

  Ili CCM ipunguzie wananchi makali ya maisha inabidi kuchukua hatua hizo hapo juu. Hasa kupunguza kodi katika mafuta ya diesel na petrol.

  Pia kupunguza kodi katika Simu na mtandao 'internet'.

  Kuwekeza katika kilimo.

  hatua hapo juu zikichukuliwa maana yake ni kuwa serikali itapata vyanzo vipya vya kodi.

  Naomba pia kama kuna Mbunge au mtu anayemjua mbunge ampe habari hizo hapo juu.

  Au naomba unipe email ya mhariri wa magazeti ya Raia Mwema, Au Mwananchi Papers Au Habarileo au Daily News au Mwanahalisi Au Nipashe/Guardian Au Tanzania Daima.

  Nataka hii habari ifike mbali zaidi na ijadiliwe bungeni.

  Asanteni
   
 2. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Tangu JK kuingia madarakani Shilingi imepanda thamani au imeshuka thamani??

  Uchumi umekuwa au umeshuka?

  Bei za vitu zimeongezeka sambamba na ongezeko la kipato cha mtanzania?

  Jk afanye nini uchumi ukue?
   
Loading...