History: Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Tshala Muana

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Leo ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanamama Tshala Muana, mmoja kati ya wanamuziki nguli na nguzo muhimu kwa muziki wa rhumba barani Afrika. Jina lake halisi ni Elizabeth Tshala Amedeus Muana Muidikay, alizaliwa May 13 mwaka 1958 huko Lubumbashi, DRC.

Baba yake alikua mwanajeshi na mama yake mama wa nyumbani. Kepteni Amadeus Muana Muidikayi aliuawa mwaka 1964 wakati huo Tshala Muana akiwa na umri wa miaka 6 tu. Ilimlazimu mama yake kuhangaika ili kuweza kumlelea Tshala pamoja na ndugu zake 9 walioachwa na baba yao.

Kutokana na ugumu wa maisha alipohitimu elimu ya msingi hakuendelea na masomo na badala yake alianza kujishughulisha na shughuli za kumuingizia kipato ili kujikimu kimaisha. Mihangaiko ya maisha ilimpeleka hadi jijini Kinshasa na akafanikiwa kuajiriwa kama mnenguaji katika bendi ya Tsheke Tsheke Love.

Baadae alionekana kuwa na kipaji cha uimbaji na akaanza kupewa nafasi ya kuimba. Katikati ya miaka ya 1980's akaondoka kwenye bendi hiyo na kusimama kama mwanamuziki wa kujitegemea (solo artist). Alisaini mkataba na kampuni kubwa ya muziki nchini Uingereza ya Charly Records na kutoa album yake ya kwanza yenye jina "Biduaya" yenye nyimbo kama Benga nga Respect, Mobali ya famile na Africa mokili mobimba.

Aliendelea kung'ara na kutoa album zingine kama Sokous Siren (1991), Mutuashi (1996) na The best of Tshala Muana (1997) iliyokua na vibao maarufu kama Karibu yangu na Dezodezo ambacho ni 'cover' ya wimbo wa Ndala Kasheba.

Kupitia muziki wake amepata tuzo nyingi za kitaifa na kimataifa. Amewahi mara kadhaa kualikwa ikulu na Rais Laurent Kabila (marehemu) kwa ajili ya kutumbuiza. Amewahi kutuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Laurent Kabila lakini amekua akikanusha uvumi huo. Yeye na Mbilia Bel hutajwa kama Malkia wa muziki wa rhumba nchini DRC.

Mwaka 2000 alifunga ndoa na aliyekua Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Congo cha PPRD Bw.Claude Mashala. Mwaka 2005 mama yake alifariki dunia, na akasema hilo ndilo tukio lililomuumiza zaidi kutokana na alivyowalea yeye na ndugu zake 9 kwa taabu. Mwaka 2007 alitangaza kustaafu rasmi muziki.

Happy 62nd birthday Elizabeth Tshala Amedeus Muana Muidikay. Asante kwa muziki mzuri.!

FB_IMG_1589344862379.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom