Historia ya Wilaya ya Ngara, utamaduni wa wakazi wa Ngara na chanzo cha jina la kabila la Wahangaza

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
HISTORIA YA WILAYA YA NGARA, ASILI YA MAJINA MBALIMBALI, UTAMADUNI WA WAKAZI WA NGARA NA CHANZO CHA JINA LA KABILA LA WAHANGAZA WANAOKAA WILAYANI NGARA.
ngara1.jpg

ASILI YA NGARA

Wilaya ya Ngara ni wilaya inayopatikana Mkoa wa Kagera kasikazini magharibi mwa Tanzania, wilaya hiyo inakaliwa na wahangaza na washubi ambapo wilaya hiyo inapakana na nchi za Rwanda na Burundi na lugha ya watu hao ni kihangaza na kishubi ambapo lugha hizo zinaingiliana na lugha za nchi hizo mbili na kuwafanya wenyeji kuelewana kilugha na wakazi wa mataifa hayo jirani.
ngara2.jpg

Mti aina ya Umunyinya uliopandwa Halmashauri ya wilaya ya Ngara
Jina la asili la wilaya ya Ngara kabla ya kuitwa Ngara iliitwa Kibimba (yaani pori). Chanzo cha jinna hilo la Ngara lilitokana na sehemu iliyokuwa maalumu kwa mikutanao ambayo ilifanyika chini ya miti mikubwa inayoitwa iminyinya yingara( ilikuwa miti mikubwa yenye matawi yaliyosambaa) ambapo kwa sasa eneo hilo ndipo ilipo halmashauri ya wilaya ya Ngara na mti wa kumbukumbu upo mpaka sasa.

ngara3.jpg

Mti wa Umunyinya uliopandwa halmashauri ya wilaya ya Ngara ambao asili yake imebeba jina la Ngara.

Wilaya ya Ngara ilikuwa na watawala wa kichifu ambapo kulikuwa na machifu wa pande mbili yaani chifu wa Bugufi na Chifu wa Bushubi. Machifu waliotawala Bugufi walikuwa Balamba wa kwanza, Rusengo, Ruvubi, Mpanda, Kanyamazinge na Balamba motto waKayamazinge. Machifu hao wa Bugufi walikuwa wakikutana eneo la Nyamilama ili kupeana maadili na mbinu za kiutawala mfano lilivyo bunge la Dodoma kwa sasa. Na Bushubi alikuwepo chifu Nsoro.

Baadhi ya asili ya majina ya maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ngara

Murgwanza awali iliitwa Mugwanza ikiwa na maana eneo lisilokuwa na kitu hivyo hali yake ilikuwa na upepo uliowavutia wamisionari kujenga eneo hilo kanisa, hospitali na makazi yao na kushindwa kutamka jina hilo la asili ndipo wakawa wanatamka Murgwanza na mpaka sasa panaitwa hivyo.

Nyamiaga ilitokana na upepo mkali ambapo wakazi wa eneo hilo walipanda miti na migomba kupunguza upepo huo.

Kabanga ilitokana na sehemu iliyotumika kutengeneza zana za vita kama upinde na mshale sababu eneo hilo lilikuwa na miti ya kutengeneza zana hizo iliyojulikana kama imibanga. Hayo ni baadhi ya maaeneo tu ya wilaya ya Ngara na ni ngumu kuchambua maeneo yote.

UTAMADUNI

Mila na desturi ya wahangaza na washubi, mtoto alikuwa haruhusiwa kukaria kiti cha baba yake wala kula sahani moja na wazazi wake hivyo walitengwa pembeni na kula peke yao.

Wahangaza walikuwa hawaruhusiwi kula kondoo na mbuzi bali kondoo na mbuzi waliliwa na kabila duni lijulikanalo kama watwa ( mbuzi aliitwa impene kwa kilugha kwa sababu waliichukulia kama ipo uchi na ndio sababu ya kutoliwa na kabila hilo enzi hizo.

ngara4.jpg

picha ya mbuzi aliyekuwa haramu kuliwa enzi hizo lakini kwa sasa ni nyama safi
Imani ya wahangaza na washubi (dini) ilikuwa ni kuabudu chini ya miti ya Milumba (ikivumu) waliabudu mungu aliyeitwa kilanga kilumwelu (mungu wa amani) na pia kutambikia kwenye vijumba vidogo vilivyoitwa Indalo. Aidha wakazi hao waliamini kinga za asili za chale na hirizi.

ngara5.jpg

Picha ya mti wa mulumba (ikivumu)

Msichana akibeba mimba nje ya ndoa adhabu yake ilikuwa ni kufungwa jiwe la kusagia ana kutupwa mto Ruvubu eneo lililojulikana kama Mmasangano (Nyaburumbi). Na adhabu nyingine ilikuwa ni kumfungia sagio (jiwe la kusaga) na kuwekwa njiapanda (amayilabili) ili aliwe na wanyama mpaka kufa.

ngara6.jpg

Picha ya jiwe la kusagia

Wahangaza walitumia tiba ya asili yaani miti shamba kwa magonjwa. Pia kuondoa mizimu iliyokuwa inawasumbua watu alikuwa anatafutwa mbuzi au kuku mweupe wa kafara na mgonjwa kuruka kafara hiyo kasha kutupwa porini kwenye miti iitwayo imilinzi.

ngara7.jpg

wazee wa asili na waliochangia kuandaa historia hii

Utamaduni wa kuoana ilikuwa ni kwamba kijana hakuruhusiwa kutafuta mchumba bali wazazi wake walimchagulia mchumba kwa kuangalia historia ya ukoo au familia anakotoka mchumba husika. Wazazi wa pande zote mbili walikubaliana kwa kupeana mahari (posa) ya jembe la mkia (jembe la asili) au nguo zilizotengenezwa kutokana na magome ya miti (ikibugu). Binti alipelekwa usiku kuolewa.

ngara8.jpg

Mahusiano ya watu yalidumishwa kwa kutembeleana baada ya kuandaa pombe ya asili yaani impeke na gwagwa. Kulikuwa na aina mbili ya unywaji wa pombe hii, aina ya kwanza watu walialikwa na kujumuika sehemu moja walipoitwa na familia iliyoandaa pombe hiyo hasa hasa msimu wa mavuno (kiangazi) kwa kilugha illiitwa gutumila na pia njia nyingine ilikuwa ya kwenda na mitungi ya pombe kutembelea familia Fulani( kwa kilugha kugemula). Wanawake na watoto walizuiliwa kunywa aina za pombe isipokuwa walikunywa pombe ya ndimasi au iliyochakachuliwa (umushalulo).

ngara9.jpg

mitungi ya pombe

Burudani ya kabila hizo ni miaeleko yaani ngoma ya asili ya wilaya ya Ngara.
ngara10.jpg

Ngoma ya mieleko kama burudani asilia ya Ngara

Shughuli kuu ya kabila hili ilikuwa kilimo, ufugaji kwa kiasi na uwindaji wa wanyama.

Watoto walirithishwa mila na wazazi wao kwa kupewa elimu ya vitendo na hasa kugawa kazi kwa kuzingatia mgawanyiko wa kazi kijinsia.

MAJINA YA ASILI YA KIHANGAZA

Majina yalitokana na matukio mbalimbali yaliyozikumba familia husika mfano Nduhiye, Luchamumikani, Semagogwa na Nyantuntu. Hayo majina na mengineyo yalitokana na wanafamilia kukubwa na balaa Fulani kwa kipindi kirefu mfano kuzaa watoto na kufariki bila kukua.

Majina ya mungu (kilanga)
Gwankuba
Mhindakazi
Mlengela
Kashana
Mahobeka
Ruboha
Ndundagi
Na mengineyo

Majina ya kihangaza (majina ya asili)

Kwa mtoto wa kwanza hadi wa tano hawakupewa majina hayo ya kimila. ( hii inaonesha wazee wetu walitambua uzazi wa mpango tangu mwanzo maana walitakiwa kuzaa watoto wasiozidi watano.) kuanzia mtoto wa sita na kuendelea walipewa majina yafuatayo:-
Wa sita aliitwa Miburo
Wa saba aliitwa Gwasa
Wa nane aliitwa Minani
Wa tisa aliitwa Nyabenda
Wa kumi aliitwa Machumi
Wa kumi na moja aliitwa Misago
Wa kumi na mbili aliitwa Kalenzo
Wa kumi na tatu aliitwa Kasongero
Wa kumi na nne aliitwa Ndululutse
Wa kumi na tano aliitwa Myandagalo
Wa kumi na sita aliitwa Misezero
Wa kumi na saba aliitwa Nkunkumuye
Wa kumi na nane aliitwa Ntiboye
Wa kumi na tisa aliitwa Choniki
Wa ishirini aliitwa Bujana
Wa ishirini na moja aliitwa Sebilele
Wa ishirini na mbili aliitwa Bisakumbwa
Wa ishirini na tatu aliitwa Bifutso
Wa ishirini na nne aliitwa Semyavu
Wa ishirini na tano aliitwa Ntamazina

Hapo mzazi alikuwa anafunga kizazi hivyo akiendelea kuzaa alikuwa anaanza upya kwa jina la Butanguye kwa mtoto wa kike na Ndatagunye kwa mtoto wa kiume.
ngara11.jpg

Mzee Essau Hosea (kulia) akiwa na Jeremia Nduhiye Bunamiye (yupo hai mpaka sasa) (wazee waliochangia kuelezea historia hii ya Ngara)

HISTORIA YA JINA LA HANGAZA
Kabila la hangaza au wahangaza ni kabila lililopo wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera nchini Tanzania, ni kabila la watu wapole, wastaarabu na wakarimu kwa wageni. Ila si vema leo tukajua asili ya neno au jina hangaza lilitokana na nini au wapi lilitokea.

ngara12.jpg

Mzee Essau Hosea (kulia) akiwa na Mzee Singirankabo Sugwigano( alifariki 2012 akiwa na miaka 120) (wazee waliochangia kuelezea historia hii ya Ngara)

Kwa historia ya mababu zetu ni kwamba hapo zamani kulikuwa na watemi wawili wa nchi mbili tofauti yaani Burundi na Rwandakwa sasa , watemi hao walikuwa mtemi Mwambutsa wa Burundi na mtemi Kigeri wa Rwanda. Watemi hao wawili walikuja kupigana na mtemi Kinyamazinge wa Ngara.

Watu wa Ngara walibuni vita ya kupigania mpakani(boarder defensive) ambapo mababu zeetu walishinda mchana kutwa wakikata miti na usiku ambao ndo ulikuwa muda wa vita walikoka moto mkubwa, sasa wale warundi na wanyarwanda walipokuja kupigana vita vya ana kwa ana( full force attack) walishangaa kuona Moto wakati muda huo wapiganaji wa ngara yaani mababu zetu wakiwa tazama vizuri na kuwapiga mishale kwa urahisi sababu ya mwanga wa moto ndipo neno hangaaza likiwa na maana ya tazama kwa umakini kwa lugha ya Kiswahili lilianzia pale maana warundi na wanyarwanda hawakuweza kuwaona vizuri wapiganaji wetu maana walikuwa kando kidogo na moto huo hivyo wakawa wanaambiza hangaaza neza ulibe yo bali yaani angalia kwa makini uone walipo kwa kiswahili .

Na pia kipindi hicho lilitumika zaidi kumaanisha mwanga wa vita kuanzia hapo wenzetu wa Burundi na Rwanda baada ya kushindwa vita hiyo ndipo walipoanza kutuita wahangaza. Na ndipo msemo wa kilugha unasema utazi umhangaza amuhanga amaso ulipoanzia.

ngara13.jpg

Mzee Essau Hosea (kulia) akiwa na Mzee Benjamini Sigaye(wazee waliochangia kuelezea historia hii ya Ngara)

ngara14.jpg

Wazee wengine wa Mubinyange waliochangia kuelezea historia hii baadhi yao walishaaga dunia

Imechapishwa na Ezra Essau kwa usaidizi wa historia kutoka kwa Essau Hosea Chiza.

NB: Salamu za Wahangaza;

1. Asubuhi
Unasema "Mwalaye"- Unajibiwa "Mwalaye"

2. Mchana/Jioni
Unasema Mwiliwe - Unajibiwa "Mwiliwe" pia

Salamu nyingine

Unasema Namaki(habari gani) - Unajibiwa "Ni meeza"(Nzuri)

Kuaga

Nagasaga(Kwaheri) - Unajibiwa Nagasaga(kwaheri)

Ijoro Jizia(Usiku mwema) - Unajibu hivo hivo.
 
Tazama Picha mbalimbali za Mitaa ya Wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-07+16.43.56.jpg

Muonekano kwa mbali wa Barabara kuu inayounganisha Nchi ya Burundi na wilaya ya -Ngara mkoani Kagera - na Mjini wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo imekuwa ni msaada mkubwa sana kwa Wananchi wa nchi za Tanzania,Rwanda na Burundi kuitumia katika shughuli za usafirishaji.
2013-07-07+16.43.10.jpg

Kwa mbali ni muonekano wa Majengo ya Shule ya Sekondari ya Mchungaji Mwema na Makao makuu ya Ofisi za Baba Askofu Severin Niwemugizi,Askofu wa Jimbo kuu Katoliki la Rulenge-Ngara, Mkoani Kagera.
2013-07-07+16.39.23.jpg

Hili ni Eneo la Kojifa ambako Wananchi wa Wilaya ya Ngara waliobahatika kupata uhalali wa kumiliki ardhi wameanza kuliendeleza eneo hilo kwa Ujenzi wa Nyumba bora.
2013-07-07+16.38.05.jpg

Ni muonekano wa baadhi ya Nyumba za Kojifa ,ambazo licha ya kuchakaa na kuchoka kutokana na kutofanyiwa marekebisho na maboresha lakini zimekuwa ni msaada mkubwa wa Watumishi na Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi nyingine kuishi.
2013-07-07+16.37.56.jpg

Ni muonekano wa baadhi ya Nyumba za Kojifa ,ambazo licha ya kuchakaa na kuchoka kutokana na kutofanyiwa marekebisho na maboresha lakini zimekuwa ni msaada mkubwa wa Watumishi na Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi nyingine kuishi.
2013-07-07+16.44.19.jpg

Kwa mbali ni muonekano wa Majengo ya Shule ya Sekondari ya Mchungaji Mwema na Makao makuu ya Ofisi za Baba Askofu Severin Niwemugizi,Askofu wa Jimbo kuu Katoliki la Rulenge-Ngara, Mkoani Kagera.
2013-07-31+13.48.48.jpg


2013-07-31+13.49.06.jpg
2013-07-31+13.45.48.jpg

Kwa chini ya Mlima ni Eneo kuu la Machinjio ya Nyama mjini Ngara.
2013-07-31+13.52.28.jpg

Ni muonekano wa Majengo ya Ofisi ya Idara ya Ukaguzi wa Shule wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-31+13.52.53.jpg

Ni muonekano wa Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-31+13.54.47.jpg

Ni muonekano wa Majengo ya Ofisi ya Idara ya Elimu wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-31+14.00.15.jpg

Hapa ni Ofisi ya Idara ya Kilimo na Mifugo wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-31+14.00.57.jpg

Ni makutano ya Barabara ya kuelekea Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ngara ,Benki ya NMB mjini Ngara na Mahakama ya wilaya na Kituo cha Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera.
2013-07-31+14.05.31.jpg

Ni muonekano wa Wanafunzi na Majengo ya Shule ya Msingi Ngara mjini .
2013-07-31+14.06.14.jpg

Hii ni mitaa ya kwa Mboya Guest jirani na Duka la Dawa Muhimu za Binadamu la Mama Clara Mjini Ngara.
2013-07-31+14.06.55.jpg

Hapa ni makutano ya barabara inayokutanisha eneo la mitaa ya Mzee Merichioly na Lango kuu la Kuingia soko kuu Mjini Ngara Ni muonekano wa Majengo ya Idara ya Elimu wilaya Ngara Mkoani Kagera.
2013-07-07+19.47.57.jpg

Moja ya kivutio kikubwa na Kituo cha huduma ya Mafuta cha Ngara Oil kilichopo makutano(Eneo la Janction) Mjini Ngara,Kituo hicho hutoa huduma zake saa 24 kila siku za wiki.
2013-07-31+13.47.23.jpg

CREDIT:MWANAWAMAKONDA
 
Daraja la R$usumo Mpakani mwa Tanzania na Rwanda

MAPOROMOKO ya Rusumo ni moja ya maporomoko yanayomvutia mgeni yeyote anayefika katika eneo la maporomoko hayo yaliyopo katika eneo la Rusumo wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Uwepo wa maporomoko hayo unatokana na mto Kagera au Ruvubu uliopo katika mpaka wa Tanzania na Rwanda na ni moja ya eneo ambalo ni kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali wanaofika katika ene hilo lililopo nje kidogo ya mji wa Ngara.

Maporomoko hayo huonekana kwa chini ukiwa juu ya daraja linalotengaisha nchi ya Tanzania na Rwanda na yamekuwa kivutio kikubwa kutokana na maji yake kuporomoka kwa kasi sana.

Ukiwa katika eneo hilo si rahisi sana kuona mpaka chini kutokana na mvuke wa maji wenye muonekano wa ukungu unaotokana na kasi ya maji yanayoporomoka kutoka mto Kagera upande wa Ngara.

Wageni wanaovuka mpaka huo wa Rusumo ni kawaida kukuta wakishangaa maporomoko hayo ya aina yake ambayo ni kivutio kikubwa cha kitalii.

Mbali ya maporomoko hayo kuwa maonyesho ya kuvuti ya kitalii,Kwa mjibu wa watafiti ni kuwa maporomoko hayo ambayo chanzo chake ni mto Kagera au Ruvubu yana uwezo wa kuzalisha megawati 90 za umeme.

Tangu mwaka 2013 serikali za Tanzania, Burundi na Rwanda zitiliana saini mkataba wa maridhiano ya pamoja katika kusimamia mradi mpya na mkubwa wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko hayo ya maji katika Mto Kagera uliopo wilaya ya Ngara.

Mradi huo uliopo chini ya Uratibu wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC), umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kwa kiasi cha dora Milioni 340, na nchi hizo wananchama zinatarajia kunufaika na nishati hiyo ya umeme na kila nchi itapata mgao sawa wa nishati hiyo.

Ikumbukwe kuwa kabla ya malidhiano hayo, mradi huo uliwahi kuwa katika mipango ya kuendeleza umeme katika miaka ya 1980 hadi 1990, mipango hiyo iliingiliwa na kile kilichotajwa kuwa ni matumizi ya maji ya Mto Nile hivyo kukosa ufadhili na kisha baadae vita vya wenye kwa wenyewe katika nchi za Burundi na Rwanda zikadhorojesha jitihada hizo.

Imeandaliwa na Ng’oko Innocent
 
MTAA KWA MTAA:-MV RUVUBU …Ukivuka tu umeingia Mpakani mwa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.
IMG_20140907_163504.jpg

Ni muonekano wa maji ya Mto Ruvubu ndani ya Kivuko cha MV RUVUBU napenda sana kukitumia kuvuka kama naenda mpaka wa Rusumo kutalii au kufatilia mambo mbalimbali yaliyopo,yapo na yajayo hasa ukizingatia ni Mpakani mwa Tanzania na Rwanda.
IMG_20140907_163428.jpg

IMG_20140907_163044.jpg

IMG_20140907_163119.jpg

IMG_20140907_163125.jpg

IMG_20140907_163136.jpg

Kivuko hiki cha MV RUVUBU huwa hakina sana watu wengi wanaokitumia kuvuka pengine sababu ya wengi wetu hupenda kupitia Benaco hadi Rusumo lakini ukipitia barabara ya Ngara-Murukulazo ni kwepesi sana kufika kwa Haraka Rusumo.
IMG_20140907_163144.jpg

 
Kuna mambo mengi kwakweli ya kujifunza, wazee starehe yao kubwa ni pombe aina aina kama mgoli goli, msharulo,gwagwa Na ndimasi vijana nao starehe yao ni mramba Na kabago au kabalagala. Kuna MTO mkubwa wenywe wanauita ruvuvu
 
Asante sana nlikua nkiskia kwmba wahangaza ni jamii ya wahaya kama ilivyo kwa wahaya wa kyeka...
Kuna ukweli wowote hapa mkuu
 
Nataman sana kuvisit pande izo mkuu
Swal la kizushi: naskia wajeda weng wanaotoka ilo eneo wanatuuza sana kwa nchi jiran kintejensia ni kwel ?
 
Karibu kwetu
Asante kutukaribisha. Kwa picha hizi hakika KWENU NI PAZURI. Namkumbuka Mbunge wenu mmoja wa miaka ya 1980. Alikuwa pia Waziri Mdogo wa Afya. Gwassa Angasi Sebabili. Yu wapi Mzee huyu? Je, ni kina nani wengine waepata kuwa wabunge wa Ngara tangu 1961? Wa wapi? Nimeipenda Ngara!
 
Ok, asante kwa taarifa. Swali jingine rafiki yangu. Hivi Wahangaza, Warundi, Waha na Wanya Rwanda mbona Lugha ZAO zinafanana? Sasa mbona ni Makabila tofauti? Zamani walikuwa wa moja?
Mkuu kwa ufahamu wangu ni kwamba waha na warundi wameoana na kufanya mwingiliano wao uwe rahisi hata lugha zao kufanana.kwa mfano ukienda kakonko hasa kijiji kinaitwa Malenga unaweza kuvuka kwa mguu kwenda Burundi .hata soko huwa wanaingiliana.Kwa upande wa waha kufanana na wahangaza katika lugha zao ukweli ni kwamba kugha zao zinafanana sana na utofauti upo kwenye utamkaji kwani wahangaza hutamka neno kwa kuvuta lkn neno hilohilo waha hulitamka kwa kawaida ila maana huwa ileile.Pia wanafanana lugha kwasababu ya mwingiliano.
 
Back
Top Bottom