Chimbuko la kabila la Wakurya

Tatigha

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
1,957
2,012
Kabila la Wakurya

Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya.

Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria.

Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji. Hasa Abakuria walio katika wilaya ya Serengeti wanatambulika kama wafugaji.

Abakuria wanafanana na Wakisii wa nchini Kenya kwa lugha na umbile.

Wanadhaniwa walikuwa kundi moja hadi waliposhambuliwa vikali na Wamasai mnamo karne ya 19 na kusambaratishwa katika maeneo tofautitofauti.

Utengano huo ulisababisha kuweko kwa lahaja mbili ambazo zinaeleweka na kila kundi.

Abakuria wamegawanyika katika "makabila madogo" au koo kumi na sita, nazo ni: Nyabasi, Bakira, Bairege, Bagumbe (wanaoishi katika wilaya za nchini Kenya na Tanzania), Batimbaru, Banyamongo, Bakenye,Basimbiti, Basweta,Barenchoka, Baikoma, Bamerani na mengineyo. Makabila haya madogo yote yapo pia katika kabila la Wakisii nchini Kenya.

Kabila la Abakuria pia linakaribiana na kabila la Wazanaki katika Mkoa wa Mara nchini Tanzania. Itikadi zao kadhaa zinafanana.

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK.

Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.

Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.
 
Aiseee,
Nilichoelewa hapa ni kuwa "wakurya siyo watanzania"

Msaada jamani!!
 
Naomba usiishie hapo hebu tusaidie kuelewa tofauti kati ya Nyumba Ntobu na (ambayo inatia dosari kabila hili kutokana a tafsiri potofu) na Nyumba Mbooke, tafadhali.
 
africa_17_18_cent.jpg
 
Washari sana hawa watu! wana mkono mwepesi wa kupiga: yaani hata kutongoza kwao mmmmh! kuna mmoja eti aliniambia jana nimeota tuko wote tuna...., sasa naomba basi hii ndoto yangu iwe kweli!!!!
 
Back
Top Bottom