Historia ya Wachagga: Koo, Kabila na Falme-Mangi

Historia ya wachaga ni pana sana waheshimiwa kwa mfano mnafahamu ni kwanini wakibosho hawapatani na wamachame?

hapa sio chumba cha majaribio mkuu.
Kama unajua ni kwanini hao uliowataja hawapatani, tupe ushahidi hapa jamvini, tukiridhika nao tutauhalalisha.
Sawasawa?
 
mbona unaruka hoja za msingi Maqupper?
Suala la kuwa makabila tofauti kati ya hao uliowataja haliumi na wala halina sababu ya kuuma, FYI. Nimekupa vigezo vya utamaduni, ambavyo ndio likely kufanya mfanano wa kijamii, hence KABILA, nikakuomba uvimwage kimoja kwa kingine, ili tutazame kwa ujumla wake kisha tufike hitimisho kama Warombo, Wamachame na Wakibosho ni wachaga au la? Badala yake umekuja na kigezo kimoja cha matambiko, halafu ukadai kuwa waVunjo hawafanyi matambiko (madai ambayo hayajathibitishwa), na hapo juu ukaja na mipasho ya ukweli unauma, ambayo hata sielewi msingi wake. By the way, wewe unaona kuwa na ethnic tie na watu fulani ni ishu eh? Leo hii Wizara ya Utamaduni ikitangaza kuwa Warombo, Wamachame na Wakibosho si Wachaga unafikiri kuna mtu ataandamana?
Poor!

umeshaanza kulalama baada ya kujua kuwa wewe unajiita mchagga kumbe sio mbona wenzetu.wa musoma wamekubaliana na hali halisi na ndio maana kuna makabila zaidi ya kumi lakini kwa watu ambao hawajatoka musoma wanajua ya kwamba kila mwenyeji wa musoma ni mkurya kumbe siyo, kwa hiyo basi si kila.anaetoka karibu na mt kilimanjaro ni mchagga kwa ujumla wake wanajiita wachagga lakini kwa uhalisia kuna tofauti kubwa mno na ndio maana kuna wakibosho,wamachame, warombo, na wavunjo
 
Historia ya wachaga ni pana sana waheshimiwa kwa mfano mnafahamu ni kwanini wakibosho hawapatani na wamachame?
Mkuu msome mchangiaji anayeenda kwa jina la Jones, amejaribu kuelezea kwa kiasi kikubwa licha ya kwamba bado tunamsubiri aje kujibu some questions kama akiweza.
 
umeshaanza kulalama baada ya kujua kuwa wewe unajiita mchagga kumbe sio mbona wenzetu.wa musoma wamekubaliana na hali halisi na ndio maana kuna makabila zaidi ya kumi lakini kwa watu ambao hawajatoka musoma wanajua ya kwamba kila mwenyeji wa musoma ni mkurya kumbe siyo, kwa hiyo basi si kila.anaetoka karibu na mt kilimanjaro ni mchagga kwa ujumla wake wanajiita wachagga lakini kwa uhalisia kuna tofauti kubwa mno na ndio maana kuna wakibosho,wamachame, warombo, na wavunjo

huwa sina tabia ya kulalamikia upuuzi ambao hauathiri maendeleo yangu. Sijasema kuwa mimi ni Mchagga, ila nimekuambia kuwa nina asili ya huko, jua kutofautisha vitu viwili,
sawasawa?
Hilo la kuwa kila anaetoka Musoma ni Mkurya si kweli, tangu nikiwa mdogo najua kuwa kuna Wazanaki, Wajita, Warianchoka, Wajaluo, Waruuri n.k n.k. Na hakuna siku ambayo Wazanaki wali-claim kuwa wao ni Wakurya kabla ya kuja kuenguliwa kwenye Ukurya baadaye, kama unavyotaka kutuaminisha hapa. Ama kuhusu Mt. Kilimanjaro, so far kuna makabila mawili ya kudumu yanayopatikana arround, Wachagga na Wataita kwa upande wa Kenya, unaweza kuwaongeza na Wapare, ingawa wako mbali kidogo na mlima, pia kuna makabila ya kifugaji, hawa huwa siwapi sana nafasi kwa kuwa si wakaazi wa kudumu.
Back to topic: Bado hujanipa vigezo vya kiutamaduni ambavyo vinachambulika, ili tuweze kuyachambua hayo makundi matatu, tujiridhishe kuwa si Wachagga.
Patiently waiting...
 
mkuu dwight mangi horombo alikuwepo na alikua mangi wa eneo la rombo miaka hiyo na aliaminika kuwa ni m2 mrefu kupita kiasi na kaburi lake lipo eneo la keni rombo.

Kwa kuongeza tu jina Rombo limetokana na jina la mangi Horombo
 
Mchungaji amani iwe nawe...!

Kiuna kitabu niliwahi kkukisoma zamani, kinaitwa "Maisha Ya Mchaga Duniani Na Ahera"

Sina kumbukumbu vizuri na jina la mwandishi (Nadhani ni Malealle) ila ni kitabu kizuri kukisoma.
Humo unaweza kupata mambo mengi kuhusu Kabila la Wachaga, Mila na tamaduni zao, uchawi na uganga wa Kichaga na mambo mengine mengi.

Pia kuan kingine kinaitwa People of Kilimanjaro, hiki sijawahi kukisoma ila nasikia nacho ni kizuri kuwa nacho, mwandishi wa kitabu iki ni Muingereza kama sikosei.

kimeandikwa na charles dundas.
Kipo cha kiingereza na kiswahili.
Cha kiswahili kinaitwa ASILI NA HABARI ZA WACHAGGA.
kina maelezo ya kutosha kuhusu wamangi wote kuanzia.
Kilema na marangu.
Vunjo
mamba.
Keni
machame
kibosho
moshi.

na maisha ya watawala mbalimbali kama mashina,horombo,rongoma na hata rengwa mangi wa machame.
 
huwa sina tabia ya kulalamikia upuuzi ambao hauathiri maendeleo yangu. Sijasema kuwa mimi ni Mchagga, ila nimekuambia kuwa nina asili ya huko, jua kutofautisha vitu viwili,
sawasawa?
Hilo la kuwa kila anaetoka Musoma ni Mkurya si kweli, tangu nikiwa mdogo najua kuwa kuna Wazanaki, Wajita, Warianchoka, Wajaluo, Waruuri n.k n.k. Na hakuna siku ambayo Wazanaki wali-claim kuwa wao ni Wakurya kabla ya kuja kuenguliwa kwenye Ukurya baadaye, kama unavyotaka kutuaminisha hapa. Ama kuhusu Mt. Kilimanjaro, so far kuna makabila mawili ya kudumu yanayopatikana arround, Wachagga na Wataita kwa upande wa Kenya, unaweza kuwaongeza na Wapare, ingawa wako mbali kidogo na mlima, pia kuna makabila ya kifugaji, hawa huwa siwapi sana nafasi kwa kuwa si wakaazi wa kudumu.
Back to topic: Bado hujanipa vigezo vya kiutamaduni ambavyo vinachambulika, ili tuweze kuyachambua hayo makundi matatu, tujiridhishe kuwa si Wachagga.
Patiently waiting...

Sitaki kurudia ila kama ambavyo nilikwishasema tangu mwanzo ni kwamba kigezo kikuu cha utambulisho wakabila ni LUGHa
 
Kuna kitabu kiandikwa na Petro Itosi Mareale (Marehemu) -mabaye alikuwa mangi Mwitori Wa Vunjo Uchagga Moshi District , kinaitwa
" MAISHA YA WACHAGGA HAPA DUNIANI NA AHERA" Kimechapishwa na Mkuki Na Nyota Publishers . Get your copy . Bila shaka mambo mengi yamo humo.
 
kumbe ushahitimisha?
Umeshindwa kujenga hoja unakuja na sera za '...kama hutaki piga mbizi',
leta ushahidi wa kupinga nondo nilizokupa hapo juu, au uje kuthibitisha madai yako humu. Kususa hakukujengi wewe wala hakumfaidi mtu.
He mrimu!
 
Kuna kitabu kiandikwa na Petro Itosi Mareale (Marehemu) -mabaye alikuwa mangi Mwitori Wa Vunjo Uchagga Moshi District , kinaitwa
" MAISHA YA WACHAGGA HAPA DUNIANI NA AHERA" Kimechapishwa na Mkuki Na Nyota Publishers . Get your copy . Bila shaka mambo mengi yamo humo.

tajipatia nakala inshaalah!
 
kule Moshi hasa sehemu za vijijini kuna ile kitu tunaita mreshe-yaani mahandaki. Haya mashimo yametapakaa sana chini ya ardhi ya uchaga na yalitumika sana kipindi cha vita huko. Kama mahandaki haya yangepata promotion tungekuwa na jambo fulani la kuzungumza
 
Sitaki kurudia ila kama ambavyo nilikwishasema tangu mwanzo ni kwamba kigezo kikuu cha utambulisho wakabila ni LUGHa

Nadhani Makupa unaweza kuwa na ukweli fulani unaoueleza. Hata hivyo sidhani kama huo ni aina ya ukweli ambao utamuuma mtu kwa sababu nadhani jamvini hapa watu wanaweza kuwa na mdahalo kwa nia ya kuelimishana na siyo katika mtindo wa kupashana ambapo ndipo mtu anaweza kudhani amedhiliwa. Kuna tovuti ambazo zinaweza kukupa mwanga zaidi na wale wengine kwa kile ambacho kinaleta utata, yaani uwepo wa kabila linaloitwa 'wachaga'. Mfano wa hizo tovuti ni Machame - Wikipedia, the free encyclopedia. Pia vitabu vilivyokwisha kutajwa kama vile cha 'history of the chagga people of Kilimanjaro' cha Mary Kathleen Stahl, na kile cha 'Kilimanjaro and its people' cha Sir Charles Dundas. Kama unafahamu kiingereza unaweza kuvitafuta ukivipata vitakusaidia kukupa mwanga. Tatizo tu ni kwamba vimeandikwa na wazungu ambao hawana ufahamu sana wa mambo ya kiasili na tofauti na kile cha Dundas, cha Mary Kathleen Stahl ingawa kimekwenda ndani zaidi katika habari za uchagani, kina makosa mengi, hasa ya miaka na ya mtazamo wake binafsi ambao ni wa kigeni usio na asili ya kizawa.

Katika ile tovuti ya historia ya Machame kwenye 'wikipedia' utakuta kwamba hili neno chagga kwa asili si la wachaga wenyewe. Ni neno ambalo waswahili kutoka pwani waliwaita watu waliokuwa wakiishi kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro. Mwanzoni kabisa inaonekana lilikuwa neno la nchi yenyewe, yaani lile eneo liliitwa chagga na waswahili. Haionekani kabisa kama watu wa asili kule mlimani walijiita kuwa wao ni kabila gani. Walijitambulisha zaidi kimaeneo, kwa mfano, wa-Uru, wa-Kilema, wa-Machame, n.k. Wale wa kule Rombo waliitwa kwa jina la mtawala mwenye nguvu sana aliyeunganisha maeneo mengi mashariki kabisa ya Kilimanjaro yakawa chini ya himaya yake, kwa hiyo yakaitwa kwa jina lake, Rombo (kumbuka kichaga huwa wanaitwa wa-orombo). Ukisoma ile tovuti ya wikipedia itakusaidia nadhani kukupa mwanga juu ya neno hili chagga.

Hata hivyo, hii nchi ya chagga inaonekana baadaye watu wa lile eneo walikuja kuitwa wachagga, yaani watu wa nchi ya chagga. Kwa mfano, unaposema watanzania, haumaanishi kwamba wote ni kabila moja fulani linaitwa watanzania. Kwa hiyo walipoitwa wachagga (ama na wazungu baadaye au waswahili) hawakumaanisha kabila fulani linalokaa kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro, bali walimaanisha watu wanaoishi kwenye nchi inayoitwa chagga. Kwa nini ile nchi iliitwa chagga na waswahili, ile wikipedia inaeleza (sitarudia hapa kwa ajili ya nafasi). Nadhani Makupa na wengine kama mnaelewa vizuri kiingereza mkishasoma ile wikipedia rudini jamvini humu halafu tueleweshane kama bado kuna utata.

Kwa hiyo hakuna utata kwa nini waitwe wachagga. Lakini pia kuna ukweli kwamba hawa watu hawana asili moja. Hata hivyo kwa kuishi kwao pamoja kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro kuliwafanya kuchangamana kwa kiasi fulani, kuoleana, kufundishana mambo mengi ya asili zao na hata tamaduni, na ndiyo maana pamoja na lugha zao kuwa tofauti lakini zina fanana fanana.
 
story ya kweli
kulikuwa na vita iliyosumbua kati ya mangi wa kibosho na mangi wa machame.Mangi wa kibosho akatuma ujumbe kwa mangi wa machame kwamba aende na watu wake wote ilio waweke upatanisho.
basi mangi wa kibosho akachimba shimo kubwa kubwa sana wakaweka majani juu
mangi wa machame akaja na watu wake kwa amani kumbe mangi wa kibosho alikuwa hajawaita kwa amani wala nini
wamachame walivofika pale wakibosho wakawakimbiza usawa wa lile shimo sasa wamachame kukimbia wakaanguka kwenye lile shimo .inasemekana walikufa watu wengi mno siku iyo
toka hapo uadui ukatangazwa kati ya machame na kobosho
amri ikawekwa
1.ni marufuku kuoa/kuolewa kibosho-ndoa ni chache saaaana za jamii hii kama unabisha taja kama utafika 10 katika ndoa 1000
2.ni marufuku kujenga nyumba kuelekea kibosho-hadi kesho hii ipo
3.hii ni siri siwezi andika hapa
 
Hapana. Hii siyo story ya kweli. Nakubali kwamba kuna masimulizi mengi mengi tu yanayotaka kuelezea kilichotokea kwenye mauaji yale ya wamachame kule Kibosho. Kwa mfano, ukienda Moshi utasikia wanasema kwamba wamachame walipatwa na mtego kule Kibosho kwa sababu wanapenda sana kula. Kwa hiyo, waliitwa kwenye sherehe ya kula nyama na pombe, wakala mpaka wakalewa halafu wakibosho wakawageuka wakawamaliza. Ukienda Marangu, Uru, n.k. utasikia masimulizi ya aina aina tofauti. Hizi zote ni nadharia zinazotokana na habari za kusikia na zisizo na uhakika wa uhalisia wa tukio lenyewe.

Kwanza ujue kwamba mangi wa Kibosho asingeweza kuwaita wamachame kwa sababu mpaka wakati huo Machame ilionekana ndiyo uliyokuwa inatawala mpaka Kibosho yenyewe (kumbuka hata mangi Sina aliwekwa na wamachame). Kiutawala, mdogo hawezi kumwita mkubwa au kumwamuru aje kwake. Pia vilevile, pamoja na masimulizi ya waathirika wenyewe wa matukio kuna taarifa zilizoandikwa na wavumbuzi wa kizungu karibu kabisa na kipindi ambacho hilo tukio lilitokea na maelezo yanafanana. Kwa hiyo hicho ulichokieleza 'Smile' siyo cha kweli maana hakina taarifa yenye nguvu inayokiunga mkono (yaani 'support'). Hata hivyo , ni kweli kwamba wakibosho walijiandaa kwa hilo tukio. Kwa mfano, walichimba mashimo katika njia mbalimbali zinazoweza kupitia kwenda Machame (siyo njia kuu ambayo waliitumia kujia Kibosho). Na wakafanya kama ulivyoeleza. Halafu, waliua panya wengi na hata wanyama wengine, wakawaweka kwa muda mrefu wakanuka na kuvunda. Waliwarundika kwenye boma la mangi Sina mwenyewe, na Sina akiwa ndani humo amejichifa kwenye hiyo harufu akiwa na bunduki yake. Hii ilikuwa kuwaaminisha kwamba alishakufa kweli na kuanza kunuka. Inasimuliwa kwamba hata hivyo, wanawake kadhaa wa kibosho kwa kuingiwa huruma na kilichokuwa kimepangwa (kumbuka hata Kibosho yenyewe waligawanyika kwa sababu wasingeweza kujua hatma ikiwa mpango huo ungeshindikana) waliweza kuwashitua baadhi ya wamachame waliokuja kwenye bomba la mangi Sina, kwa hiyo wapo walioweza kuingia mitini mapema. Kwa hiyo 'Smile' umepata taarifa nusunusu na baadhi zimechakachuliwa. Umefanya vyema hata hivyo kufanya angalau utafiti kidogo.
 
asante mkuu jones kwa masimulizi yako? je unaweza kunipa jibu kwanini kulikuwa na uadui kati ya kibosho na machame?
 
mwenye access na kitabu cha Sir Charles Dundas, Kilimanjaro and Its Peoples, 1924,akiweke hapa tafadhali,pia akiniPM nitafurahi zaidi.kitamaliza mgogoro huu
 
naomba mkifikia muafaka wa mgogoro huo nami nitoe historia ya wachaga na wapere,nikizingatia origin ya jina wapare na sababu ya utani uliopo
 
mwenye access na kitabu cha Sir Charles Dundas, Kilimanjaro and Its Peoples, 1924,akiweke hapa tafadhali,pia akiniPM nitafurahi zaidi.kitamaliza mgogoro huu

Snochet,

Sifahamu ni mgogoro gani huo unaouzungumzia labda utoe ufafanuzi. Kuhusu kitabu cha Kilimanjaro and its peoples, sina uhakika una maana gani kitamaliza mgogoro wakati hujakisoma bado. Vitabu vyote vilivyotajwa humu jamvini vitaweza kukusaidia kupata mwanga wa historia ya uchagani, hata hivyo vitabu, nyaraka, na majarida yanayoelezea habari za uchagani ni vingi mno. Kuna hata baadhi ya waandishi watafiti walifikia mahali wakadai kwamba wachaga ni kabila lilioandikwa habari zake kwa wingi kuliko hata makabila mengine yote ya Afrika. Labda hii haitokani tu na maarifa na maendeleo ya kifikra waliyoyaonyesha lakini pia ni kwa sababu ya kuwepo mlima Kilimanjaro kule. Kuhusu upatikanaji wa vitabu, vyote vinaweza kupatikana amazon.com ingawa ni vitabu vyenye bei ya juu mno. Kwenye maktaba muhimu Tanzania unaweza kuvipata pia nadhani, mfano kule Moshi, chuo kikuu cha Dar es Salaam, na makumbusho ya taifa. Sidhani hata hivyo kama vinaazimwa.

Smile, kuhusiana na uadui wa Kibosho na Machame, naona ni historia ndefu lakini kwa kiasi kikubwa imeshadokezwa kwenye blogu hii. Ukipata muda soma kuanzia no.1 taratibu mpaka uje ufike kwenye ukurasa huu (no.5) utaona vilivyoelezwa. Mengi tayari yameshajadiliwa hivyo jaribu kupitia tena usome masimulizi hayo kwenye kurasa mbalimbali za nyuma za mada hii.

Asango, karibu sana. Nitashukuru kufahamu hiyo historia ya wapare na wachaga. Ninafahamu kuna masimulizi ya aina aina, kwa hiyo nitashukuru kuona mrengo wako kama umejitikita kwenye utafiti zaidi. Naamini itasisimua na kuchangamsha.
 
asante mkuu
 
Back
Top Bottom