Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
Baada ya kuona swali la JMushi ambalo ni kilio cha kusikia kuwa Babu yake Mangi Sina alikuwa msaliti, kauli ambayo JMushi anasema ilitolewa na John Mnyika, nimeonelea nifungue hii thread ili wenye kumbukumbu za kihisoria kuhusu ujenzi wa Kabila la Wachaga, koo na himaya za Mangi kutokana na mgawanyiko wa Wachaga, iwe ni Machame kwa Shangali, Kibosho kwa Sina, Marangu kwa Mareale, iwe ni Mangi Rindi, Meli, Pfumba, Molelia na wengine.
Aidha kutokana na kuongezeka kwa tuhuma za ukabila na hasa kusemekeana Chadema ni cha Wachaga na kuna ubaguzi kati ya Wamachame ambako Mwenyekiti wa Chadema Mbowe anatoka, dhidi ya Wachaga wengine, Kibosho, Uru, Vunjo, Kilema, Rombo nk. ni muhimu tupitie historia ya wachaga kwa manufaa yetu sote, tuijue hii jamii, na ni jinsi gani ilivyoweza kuwa kubwa na kuwa na umahiri katika masuala ya biashara na elimu.
Natumaini JMushi atatumia fursa hii kujifunza kuhusu Kabila lake na historia yake pamoja na mahusiano kati ya makundi ya wachaga na hivyo kutoa majibu ya maswali aliyonayo hasa kuhusu uadui kati ya Mangi Meli na Mangi Sina.
Naomba kufunga ukumbi kwa majadiliano na kuelimishana.