Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,900
- 30,235
Mwanakijiji,true true.. inabidi Mzee Said aje atuambie majina yao ili waweze kuenziwa na kuheshimiwa.
Kama nilivyotanabaisha huko nyuma kuwa "advantage" yangu kubwa kukushindeni mimi ni mengi ambayo nyie hamna. Hilo la kuwaenzi mashujaa ndilo linalowapa shida kwa muda mrefu toka kitabu changu kitoke. Wanajiuliza tunaanzaje na Baba wa Taifa mwenyewe tulipata kumshauri afanye hivyo wakati alipotoa medali kuwaadhimisha wale walifanyia nchi makubwa na yeye akakataa? Soma hapa chini:
"Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa,[1] katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh abdallah Chaurembo. Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani." [1]
Nilipata kuzungumza na Zuberi Mtemvu kuhusu hili la Dossa. Mtemvu akasema kwa kwelli hata yeye kashangaa kwa Nyerere kutoa medali ka Dossa akawaacha wengie waliokuwa pamoja naDossa tena kaja kumpa medali hiyo peke yake baada ya wengine kutunukiwa. Akaendelea Mtemvu kusema lipi alofanya Dossa ambalo Abdulwahid hakufanya?Mwenyekiti wa kamati ile ya medali alimuuliza Nyerere mbona huwaadhimisi wale walikupokea Dar es Salaam?
Mwanakijiji nakupa changamoto nyingine mtafute nani alikuwa mwenyekiti wa kamati ya medali akupe jibu Nyerere alisema nini kuhusu wazalendo waliompokea Dar es Salaam.
Mohamed