Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,887
- 30,232
HISTORIA YA UDHALIMU IKIHIFADHIWA NI SILAHA KWA ALIYEDHULUMIWA NA HUWA FUNZO JEMA KWA DHALIMU
Mgahawa mpya ulitangazwa kuwa utafuguliwa tarehe kadhaa na ukawa unafanyiwa matangazo katika gazeti maarufu mjini Tel Aviv na tangazo likawa limetiwa kila aina ya maneno ya kuvutia wakisema, ‘’Watch This Page,’’ yaani usikose kuangalia ukurasa huu na tangazo lilikuwa na ukurasa mzima katikati ya gazeti sehemu ambayo msomaji hatakosa kufungua.
Ikawa hivyo kwa mwezi mzima na kila tangazo linawekewa nakshi, maandishi na picha za kuvutia huku siku zikihesaiwa kuwa leo zimebakia siku 5 mgahawa kufunguliwa siku ya pili tangazo litanadi zimebaki siku 4 mgahawa kufunguliwa na hivyo, hivyo tangazo likawa kila siku hadi ikabaki siku 1 na kuongezea, ‘’Kesho ndiyo siku yenyewe ya ufunguzi.’’
Hapo pakawekwa tangazo kuwa kwa watu 100 watakaopata kifungua kinywa hapo baina ya muda wa chai na chakula cha mchana mgawaha utakapofunguliwa watakula bure na watapewa zawadi ambayo haikutajwa na watapewa mwaliko maalum wa kuja kula chakula cha jioni na wake au waume zao.
Haya yote yatafanywa kwa ‘’rotary,’’ baina ya wakati wa chai asubuhi na chakula cha mchana.
Hata kabla hakujaanuka sawasawa muda wa kufungua mgahawa haujafika mtaa ukawa kama vile umevamiwa.
Pembeni ya mtaa karibu kabisa na mgahawa liliegesha gari la televisheni mtu wa camera akijaribu kupata picha zilizokuwa zinarushwa mubashara.
Jambo kama hili lilikuwa halijapata kutokea popote katika kumbukumbu za wakazi wa Tel Aviv.
Kweli kumekuwa na matangazo kama haya ya kuvutia biashara lakini hili lilikuwa limefurtu ada.
Kulikwa na uvumi kama kawaida ya miji mikubwa kuwa itatolewa zawadi ya dola za Marekani 10,000.00.
Muda wa kufungua mgahawa ukafika.
Mgahawa huu haukuwa umeelezwa jina lake.
Watu wakawa wamejipanga tayari kwa ufunguzi na kuingia ndani ya mgahawa.
Kabla ya kufungua milango mtangazaji akatawatangazia waliokuwapo kuwa watu wataingia baada ya kupachika bao lenye jina la mgahawa.
Mbele ya mlango palikuwa na wasichana warembo wamevaa vizuri wanasubiri kukaribisha watu.
Wakatokea watu wawili wamevaa nguo za wajenzi kichwani wana ‘’helmet,’’ yaani kofia ngumu na mabuti wakapanda zile ngazi kila upande wa mlango wamebeba bao limefunikwa kwa kitambaa cha hariri cheupe wakapanda ngazi zilizokuwa pembeni wakatundika bao na kwa haraka wakashuka chini.
Wakaja wasichana warembo wawili wakashika kamba huku na huku wakavuta na jina la mgahawa likaonekana likiwa katika maandishi ya makubwa meusi kwenye ubao mweupe.
Jina la mgawaha lilikuwa moja tu, ‘’Auschwitz.’’
Ulipigwa ukimya kwa sekunde ikawa kama vile wale waliofika pale wametokewa na zimwi mla watu anataka kuwatoa roho.
Wapiga picha walizubaa kwa sekunde chache kisha ghafla ikawajia kuwa wapo mbele ya tukio kubwa na kwa ghafla vilevile kama walivyoshtuka na kusita kupiga picha milio ya camera zikasika mianga ya camera ikikimbizana na kufanya kivuli na mwanga, kivuli na mwanga, kivuli na mwanga, camera zikatoka kwenye bao zikaelekezwa kwa watu wake kwa waume waliofika kwenye ufunguzi ule camera sasa zikiwa zimelengwa sura zao.
Wapigaji picha wale wenye uzoefu wa miaka na miaka wakijua kuwa tukio lile lote litabebwa na sura zilizopigwa na radi kali ya mshtuko wa yale yaliyokumbushwa na na yale waliofanyiwa wazee wao na Wajerumani Poland kwenye kambi iliyokuwa ’Auschwitz.’’
Milango ilikuwa wazi lakini hakuna aliyenyanyua mguu kuingia ndani ya mgahawa ule.
Kundi lile lililokuwa limejikusanya pale nje mbele ya mgahawa likawa sasa linarudi kinyume nyume, kimya kimya.
Ilichukua muda wa dakika mbili au tatu hivi kwa watu kurudi katika hali zao za kawaida.
Nyuma ikasikika sauti ya mtu akipiga ukelele, ‘’Vunja mgahawa huo, vunja!’’
Kama mashine ya saa inavyofanya kazi bao lilishushwa kwa haraka na mahali pale likapandishwa bao jingine kubwa mara mbili ya lile likiwa lineandikwa maneno haya, ‘’Hatujasahau!’’
Ikasikika sauti kutoka kipaza sauti kinapiga nyimbo maarufu ya Wayahudi, ‘Havanagila’’ na sauti ya msichana inaita,’’Karibuni ingieni ndani tunywe chai na tupongezane kwani tunastahili, baada ya miaka hii yote na vizazi kupita bado hatujasahau.’’
Taratibu watu wakawa wanaingia mgahawani na kabla hawajaingia ndani walikuwa wanafuta viatu vyao kwenye lile bao lililoandikwa, ’’Auschwitz.’’
Historia inayoishi kwa kukumbukwa ni silaha ya kuzuia dhulma ziliyofanywa na madhalimu kutorudiwa tena.