HISTORIA YA TANZANIA: Mkemanzi Lukamba aomba machifu waitwe wafalme

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Katika Mkutano wa wadau wa elimu kujadili somo la Historia ya Tanzania uliwakutanisha watawala wa kimila walioko nchini Tanzania ili kujadili vitu vya kujumuisha katika somo la Historia.

Kitukuu wa Kaitaba, Mkemanzi Lukamba amesema Machifu watambulike kama wafalme kwa kuwa neno chifu ni la kikoloni lililokuwa na nia ya kuwadunisha kiutawala watawala wa Kiafrika.

Aidha ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo inshughulika na #COVID19 ambayo imerudisha kwenye mila iliyokuwa ikitumiwa na wazee wa zamani, hasa suala la kujifukiza.

Katika maoni mengine ametaka suala la vita ya Kagera lifundishe kwa wanafunzi wa kidato cha tatu.

===

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania kukusanya maoni yote ya somo la historia yanayotolewa na kuyachambua bila kulala ili somo hilo liwe na mvuto wa kuongeza ari ya kulisoma kwa wanafunzi ili waipende nchi yao.

Ndalichako alisema jana alipokuwa akifungua mkutano wa wadau kuhusu kupokea maoni juu ya maudhui ya somo la historia Tanzania jijini Dar es Salaam.

Alisema baada ya kupokea maoni mbalimbali ya wadau Taasisi itayafanyia kazi na kuhakikisha kuwa yanaingizwa katika mihutasari na vitabu vya somo hilo.

“Kazi hii hakuna kulala mnapaswa kuifanya usiku na mchana ili mfanyie kazi maoni ya wadau.

“Ninasisitiza kuwa kazi ya kukamilisha uandishi wa vitabu ikamilike Mwezi wa Tatu kama ilivyopangwa ili uchapaji na usambazaji ukamilike kabla ya mwezi Julai ambapo somo hili litaanza kufundishwa rasmi. Mwenyekiti wa Baraza simamia utekelezaji wa ukamilishwaji wa kazi hii,” alisema.

Profesa Ndalichako alisema Taasisi hiyo tayari imekamilisha kazi ya kuandaa Rasimu za Mihtasari ya somo la Historia ya Tanzania itakayotumika kuanzia ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari hadi Kidato cha Sita.

“Kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa na Mheshimiwa Rais, lengo la kuanzishwa kwa somo la Historia ya Tanzania ni kuamsha na kujenga moyo wa uzalendo kwa kuwafanya Watanzania kuifahamu nchi yao, kuithamini, kuipenda, na kulinda rasilimali zake,” alisema.

Alisema historia ya Tanzania itasaidia pia wanafunzi kutambua harakati za kimaendeleo zinazoendelea nchini.

“Tanzania imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo, Uchumi wa Viwanda, Kilimo, Utalii, Biashara, Uvuvi, Usafiri na Usafirishaji, Nishati, Madini na Huduma za Jamii,” alisema.

Alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi yenye mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Afrika kwani kambi za wapigania uhuru wa Nchi za Afrika ya Kusini, Msumbiji na Namibia zilikuwa nchini wakati wa kudai uhuru hadi kupata Uhuru.

“Mpaka sasa Tanzania bado ipo mstari wa mbele katika kulinda uhuru wa nchi za Afrika. Ni vema wanafunzi wakaelewa nafasi ya Tanzania katika kulinda Uhuru wa nchi za Afrika na nchi yetu, na kwamba kukosekana kwa amani katika nchi za jirani kunahatarisha Uhuru wetu kama Taifa,” alisema.

Alisema katika mkutano huo viongozi wa jadi wamealikwa kutoka sehemu mbalimbali ili kukusanya taarifa kuhusu ulinzi wa Jamii za Jadi, vivutio vya Kihistoria ambavyo havijulikani katika maeneo waliyomo.

Pia historia yoyote katika maeneo yao ambayo haijawahi kuandikwa, watu mashuhuri katika maeneo yao walioshiriki katika harakati za ukombozi dhidi ya wavamizi wa kikoloni, na mbinu zilizotumika katika kupinga uvamizi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk. Aneth Komba alisema katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli, taasisi hiyo imekamilisha kazi ya uandishi wa rasimu za mihtasari.

Alitaja rasimu hizo ni muhtasari wa somo la historia ya Tanzania Elimu ya Awali na Msingi darasa la kwanza mpaka la saba.

Pia muhtasari wa somo la historia ya Tanzania elimu ya sekondari kidato cha kwanza mpaka cha nne na muhtasari wa somo la historia ya Tanzania Elimu ya sekondari kidato cha tano mpaka cha sita.

Alisema kwa sasa taasisi hiyo inaendelea kukamilisha kazi ya uandishi wa rasimu za vitabu na miongozo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza na kufundisha kazi ambayo itakamilika Machi 30 mwaka huu.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Machifu Msagati Fundikira alisema historia ya kweli wanayo machifu wan chi.

Alisema watatoa ushrikiano na historia ya kweli ya nchi ya Tanzania, pia aliomba machifu wapewe nafasi ya kufundisha mila na tamaduni.
 
Tanzania inautajiri mkubwa sana wa historia kupitia hawa Machifu wa kimila.Naunga mkono hoja kwamba ni vizuri kutumia vyanzo vyetu vya uhakika hasa vya oral trdition kutoka kwa warithi wa hawa Watawala wa kimila ili tuweze kuijua historia ya makabila na koo zetu kwa ukamilifu. Jambo hili wala sio aibu au kuendekeza ukabila maana ni muhimu kwa binaadamu yoyote kufahamu asili yake

Mwalimu Nyerere alifuta Uchifu kwa sababu ambazo pengine wakati ule zilikua na mashiko lakini kwa wakati huu hakuna tena tishio la kusema kwamba wanaweza wakaligawa taifa, bali kuwathamini viongozi hao wa jadi kunaweza kwa namna moja au nyingine kuliunganisha kwani watu watajua historia ya kweli na kufahamu mchango wa mila katika ukombozi na hata ujenzi wa Taifa na pia kuliponya Taifa na baadhi ya majanga. Tukumbuke kua mkataa asili ni mtumwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom