Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika: akili inapokataa kupokea elimu mpya

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,084
Akili inapozoea kitu kwa muda mrefu sana na kukiamini huwa inapata tabu kuamini elimu mpya inayokinzana na yale aliyofundishwa kwa muda
mrefu.

Nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes na ndani yake kuna historia ya wazalendo wengi sana ambao historia na michango yao katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika haikupata kufahamika.

Jana gazeti la Raia Mwema lilichapa makala iliyohimiza Mjii Mkuu Dodoma ihifadhi kama sehemu ya historia yake historia ya wazalendo wa mji wa Dodoma ambao waliasisi TANU na kupigani uhuru wa Tanganyika.

Nimepokea maswali mengi kuhusu historia ya wazalendo hawa na wengine,maswali ambayo si rahisi kuyajibu kwa sentensi hata kumi mtandaoni.

Lakini kinachojitokeza ni msomaji kupata mshtuko kwa kusoma historia ya wazalendo hawa kwa mara ya kwanza na linalowahangaisha wengi ni kule kuamini kutokana na kusomeshwa kwao, kuwa watu wale walikuwa si kitu chochote kama historia waliyosomeshwa ilivyowaweka.

Naweka hapa mfano mdogo wa jibu nililompa kijana mmoja aliyeniluza swali kuhusu Abdul Sykes akiwa kashangazwa na historia yake kama nguzo kuu katika kuasisi TANU:

Abdul Sykes Allah alimneemesha kwa mengi na alipendeza sana kwa wengi kwa ukarimu wake kiasi marafiki zake wakampa jina, "The Sweet Abdul Sykes," Vitani Burma (1942 - 1945) alikuwa Quarter Master Sergeant cheo cha mwisho kwa Mwafrika katika King's African Rifles (KAR), baada ya WWII Dar es Salaam akawa Secretary General Dar es Salaam Dockworkers Union (1948), Secretary TAA na mjumbe wa TAA Political Subcommittee (1950), Market Master, Acting President TAA (1951 - 1953), (Admitted to Princeton University, New Jersey 1953),Vice President TAA (1953) President Julius Nyerere, muasisi wa TANU kadi no. 3 (1954), mfadhili mkuu wa harakati za uhuru na mtu aliyempokea na kuishi na Mwalimu Nyerere nyumbani kwake (1955), Prison Superintendent (Bwana Jela) 1960...akiendesha Mercedes Benz 280 SE...

Kwa hakika kitabu cha maisha yake hakijapingwa na yeyote kuhusu ukweli wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika
na jinsi yeye alivyokuwa msaada mkubwa kwa Julius Nyerere kuingia katika siasa za TAA Dar es Salaam na kupanda kwake hadi kuwa Rais wa TANU na mwishowe kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika ulipopatikana uhuru mwaka wa 1961.

1080543


1080547


Mwandishi akifanya kipindi Azam TV Morning Trumpet akieleza historia
ya TANU na uhuru wa Tanganyika na mchango wa Abdul Sykes.
 
Hugo Sykes ana u special gani zaidi ya Watanganyika wote kwa pamoja?

Kwanini mtake kuwatukuza watu wachache mnawasahau wananchi waliosimama kwa pamoja kudai taifa na kufanya kaz?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom