Kumbe hata zamani kulikuwa na wapmbav.................Inaendelea.
- Nimekuwa natafiti pole pole kutafuta picha za pesa tulizowahi kutumia hapa kwetu, nikaona nizitundike hapa kukumbushana tulikotoka. Kuna sarafu ambazo nimeshindwa kupata picha zake, lakini hata hivyo nadhani nimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kukusanya ukweli kuhusu sarafu yetu. Najua kuwa hadithi hii ni ndefu sana, hata hivyo kama unataka kujua historia ya sarafu yetu jipe dakika kumi hivi kuisoma yote hapa; ni burudani ya aina yake.
Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo
Riyal
Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.
Maria Theresa Saler
Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:
1 Anna
1/4 rupee
1/2 rupee
1 rupee
Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.
Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.
- senti 20
senti 50
Shilingi 1
Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.
Shilingi 5
Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:
shilingi 25
Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.
senti 10
Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo
Shillingi 5
Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.
Na wewe pia asante kwa kutukumbushia uzi huu!!wengine hatukuwahi kuuona! Thanks man!Ubalikiwe kichungungu