Mwl. Prof Kichuguu,
Nashukuru sana kwa hiyo elimu.............nimeprint hiyo story na kuwapa wanangu wamefurahia sana
Once again thanks
Many thanks kichuguu for this.Hapana, sarafu ndogo kabisa kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa ya senti tano. Website ya benki kuu haina record nzuri ya kuonyesha historia ya sarafu yetu.
Nimeshindwa kupata baadhi ya sarafu kadhaa za kumbukumbu mbalimbali zilizotolewa nyakati za Nyerere na Mwinyi kwa mfano kumbukumbu ya mwaka wa mtoto wakati wa Nyerere, kumbukumbu ya kufunguliwa kwa jengo jipya benki kuu wakati huo n.k.
Nimeshakamilisha historia ya noti zetu; nitaipost baadaye nikipata muda wa kutosha, kwa hiyo wale wote wanaofurahia historia ya mambo ya nchi yetu kama mimi kaeni mkao wa kula tu.
Baada ya vita ya dunia mwaka 1919, Bara na Zanzibar pamoja na Kenya na Uganda zilikuwa chini ya himaya ya mwingereza ingawa kwa mikataba tofauti. Kuanzia hapo nchi hizo zilianza kutumia sarafu moja. Katika kipindi kifupi kuanzia mishoni mwaka 1919 hadi kati kati ya mwaka 1920, bara walitumia rupie za kijerumani pamoja na rupie za kiingereza zilizokuwa zikitumika nchini Kenya, Uganda na Zanzibar. Baada ya hapo, sarafu mpya ya Florin ya Afrika Mashariki iliingizwa kwenye mzunguko badala ya rupie na rupee. Kwa bahati mbaya sarafu hii ya Florin haikudumu muda mrefu na mwanzoni mwa mwaka 1921 ikabadilishwa na Shillingi ya Afrika ya Mashariki. Kwa hali hiyo kuna sarafu chache sana za Florin zilizotolewa katika kipindi hicho na sikufanikiwa kupata picha yake. Sarafu ya Shilingi ya Afrika Mashahariki ni kati ya sarafu imara sana zilizokaa kwenye mzunguko kwa muda mrefu bila kufanyiwa mabadiliko yoyote. Ilitolewa katika vipande vya senti 1, senti 5, senti 10, senti 50(nusu shillingi) na shilingi 1. Upande mmoka wa sarafu hizo ulionyesha jina la mtawala wa himaya ya uingereza, na upande wa pili ama ulikuwa na ama pembe za tembo au picha ya simba dume. Pembe za tembo zilikuwa kwenye sarafu za senti 1, senti 5 na senti 10 wakati simba dume alikuwa kwenye sarafu za senti hamsini na shilingi moja kama ifuatavyo
Nyuma ya sarafu
Upande ulioonyesha mtawala wa uingereza ulifanyiwa mabadiliko ya mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiutawala. Kuanzia mwaka 1921 mpaka mwanzoni mwa mwaka 1936 wakati wa utawala wa Mfalme George wa tano sarafu zilikuwa na sura ifuatayo.
Baada ya kifo cha Mfame George wa tano na utawala kuchukuliwa na Mfalme Edward wa nane, ni sarafu moja tu iliyobadilishwa kwa vile mfalme huyu alivuliwa madaraka baada ya muda mfupi tu kutokana na uamuzi wake wa kuoa mwanamke aliyekuwa ameachika Marekani. Sarafu iliyobadilika wakati huo ilikuwa ya senti tano tu, ambayo ilionekana kama ifuatavyo
senti 5
Mfalme George wa sita aliyekuwa mdogo wa mfalme Edward wa nane alichukua madaraka mwishoni mwa mwaka huo huo wa 1936. Sarafu zilizotengezwa wakati wa utawala wake zilikuwa na sura za aina mbili. Sura ya kwanza ilionyesha mfalme kama GEORGIVS VI. Sarafu za aina hii zilitolewa kati ya mwaka 1937 hadi mwaka 1946; zilikuwa na sura ifuatayo.
Sarafu za aina ya pili cghini ya Mfalme george wa sita silikuwa na maneno ya GEORGIVS SEXTVS REX. Hizi zilitolewa kati ya
mwaka 1949 hadi mwaka 1952 alipofariki. sarafu hizo zilionekana kama ifuatavyo.
Baada ya mfalme George wa sita kufariki, alirithiwa na binti yake Malkia Elizabeth wa pili mwaka 1952. Chini ya malkia huyu sarafu ziliokena kama ifuatavyo.
Sarafu hizi zilendelea kutumika hata baada ya kupata uhuru wetu. Kwa mafano sarafu zilizotolewa mwaka 1963 (baada ya uhuru)
zilionekana ifutavyo.
Ilipofika mwaka 1964, kukafanyika mabadiliko kidogo katika sura ya sarafu yetu kwa kuondoa maneno yanayoonyesha mtawala wa himaya ya kiingereza. Sarafu za senti tano na senti kumi zilizotolewa mwaka 1964 zilikuwa zinaonekana kama ifuatavyo.
Hata hivyo sarafu ya pamoja ya Afrika Mashariki ilifikia kikomo chake mwaka 1966 wakati Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki ilipovunjwa na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda. Sijaelewa sababu ya kuvunjika kwa bodi hiyo ya sarafu, bado ninafanya utafiti. Nikizpta nitawagawieni.
..........................Inaendelea
kweli jj picha hazionekani, sasa sijui tatizo liko wapi? mie nnaona kama ww
[h=2]Banknotes and Coins[/h] [h=3]Banknotes Series[/h] The Bank of Tanzania introduced a new series of banknotes in January 2011. The Banknotes series are in the denominations of Shillings 500, 1000, 2000, 5000 and 10000.
The previous series of banknotes issued in 2003 continues to circulate in parallel with the new issue. These will be withdrawn from circulation gradually until a date when they will be declared demonetized.
[h=3]Currently Circulating Coins[/h] The current coins in circulation are as follows: =/05, =/10, =/20, =/50, 1/=, 5/=, 10/=, 20/=, 50/=, 100/= and 200/=.
[h=3][/h]