Omary Zola
Member
- Mar 10, 2015
- 29
- 3
Duh!
Mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi Grade C ulikuwa ni Sh 60 na Grade A ulikuwa kati ya Sh 80 hadi 100; kulikuwa na waalimu wa daraja lililoitwa EO3 (Education Officer Grade 3) walikuwa wanapata mashara wa kat ya Sh 100 hadi Sh 120. Lakini angalia tena kuwa bei ya viatu vya ngozi Bata brand ilikuwa ni Sh10 wakati vile vya safari boot ilikuwa ni Sh 7. Bei ya suruali ya tetron ilikuwa Sh12 wakati ile ya Kakhi-Amerika ikiwa shillingi 9 na ile ya climpline (sijui kama nimepatia spelling) ilikuwa Sh 10. Mashati ya Gossage au Shikibo yalikuwa yanauzwa kati ya shilingi 7 -mikono mifupi, na Shilingi 8-mikono mirefu. Haya Mashati ya Gossage na Shikibo yalikuwa na quality kubwa sana kuliko haya ya Van Heusen leo.Hiyo noti ya Masai nilikuwa nasikia wakisema ni admu mtu kuwa nayo miaka hiyo ya 1969, maana mshahara wa mwalimu wa msi ngi ulikuwa haufiki shs 30/=.
Acha uboyaMshahara wa mwalimu wa shule ya msingi Grade C ulikuwa ni Sh 60 na Grade A ulikuwa kati ya Sh 80 hadi 100; kulikuwa na waalimu wa daraja lililoitwa EO3 (Education Officer Grade 3) walikuwa wanapata mashara wa kat ya Sh 100 hadi Sh 120. Lakini angalia tena kuwa bei ya viatu vya ngozi Bata brand ilikuwa ni Sh10 wakati vile vya safari boot ilikuwa ni Sh 7. Bei ya suruali ya tetron ilikuwa Sh12 wakati ile ya Kakhi-Amerika ikiwa shillingi 9 na ile ya climpline (sijui kama nimepatia spelling) ilikuwa Sh 10. Mashati ya Gossage au Shikibo yalikuwa yanauzwa kati ya shilingi 7 -mikono mifupi, na Shilingi 8-mikono mirefu. Haya Mashati ya Gossage na Shikibo yalikuwa na quality kubwa sana kuliko haya ya Van Heusen leo.
@@A A€-/-B SWiki chache zilizopita niliwaletea historia ya fedha ya sarafu hapa nchini kwetu nikaahidi kumalizia na historia ya noti. Kwa bahati mbaya majukumu yamenizidi nikashindwa kupata nafasi ya kuiandika ingawa nilikuwa nimeshaifanyia utafiti wa kutosha. Leo hii nimeamua kulivalia njuga ili niikamilishe, samahani sana kwa wanachama kwa vile historia hii ni ndefu kidogo kuliko ile ya sarafu kwa vile noti zilipitia mabadiliko mengi sana kuliko sarafu.
Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatasi zilianza kutumika mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolewa katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake
Rupie 5
Rupie 10
Rupie 50
Rupie 100
Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.
5 Zanzibari rupee
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake
1 Rupie
5 Rupien
10 Rupien
20 Rupien
50 Rupien
Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.
Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."
.....INAENDELEA