Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Dahh hongera sana kwa utafiti huu. Hii mada yako inathamani kubwa sana. Hongera sana sana sana
 
Hiyo noti ya Masai nilikuwa nasikia wakisema ni admu mtu kuwa nayo miaka hiyo ya 1969, maana mshahara wa mwalimu wa msi ngi ulikuwa haufiki shs 30/=.
Mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi Grade C ulikuwa ni Sh 60 na Grade A ulikuwa kati ya Sh 80 hadi 100; kulikuwa na waalimu wa daraja lililoitwa EO3 (Education Officer Grade 3) walikuwa wanapata mashara wa kat ya Sh 100 hadi Sh 120. Lakini angalia tena kuwa bei ya viatu vya ngozi Bata brand ilikuwa ni Sh10 wakati vile vya safari boot ilikuwa ni Sh 7. Bei ya suruali ya tetron ilikuwa Sh12 wakati ile ya Kakhi-Amerika ikiwa shillingi 9 na ile ya climpline (sijui kama nimepatia spelling) ilikuwa Sh 10. Mashati ya Gossage au Shikibo yalikuwa yanauzwa kati ya shilingi 7 -mikono mifupi, na Shilingi 8-mikono mirefu. Haya Mashati ya Gossage na Shikibo yalikuwa na quality kubwa sana kuliko haya ya Van Heusen leo.
 
Acha uboya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia nzuri ila umesema kuwa Sh.50, 100 na 200 za noti zilipigwa ban 1995 November Mimi niliuza korosho kilo kadha nikiwa mdogo 1997 nikapata noti kadhaa za sh. 200.
Basi itakuwa ziliondolewa mwishoni mwa mwaka.
 
Wiki chache zilizopita niliwaletea historia ya fedha ya sarafu hapa nchini kwetu nikaahidi kumalizia na historia ya noti. Kwa bahati mbaya majukumu yamenizidi nikashindwa kupata nafasi ya kuiandika ingawa nilikuwa nimeshaifanyia utafiti wa kutosha. Leo hii nimeamua kulivalia njuga ili niikamilishe, samahani sana kwa wanachama kwa vile historia hii ni ndefu kidogo kuliko ile ya sarafu kwa vile noti zilipitia mabadiliko mengi sana kuliko sarafu.

Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatasi zilianza kutumika mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolewa katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake

Rupie 5
doa_5rupien.jpg

Rupie 10
doa_10rupien.jpg

Rupie 50
doa_50rupien.jpg

Rupie 100
doa_100rupien.jpg

Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.

5 Zanzibari rupee

zz10.jpg

Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake

1 Rupie
doa_1rupiene_1.jpg

5 Rupien
doa_5rupiene.jpg

10 Rupien
doa_10rupiene.jpg

20 Rupien

doa_20rupiene.jpg

50 Rupien

doa_50rupiene.jpg

Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.

doa_1rupiene_3.jpg

Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."

.....INAENDELEA
@@A A€-/-B S
 
Ninayakumbuka mabadiliko ya 10,000 ya blue kuwa 10,000 nyekundu. Mr Blue aliimba mfukoni nitakuwa na blue blue. Pia nahisi 500 iliyokuwa inaitwa "Pajero" hilo jina ndilo lililofupishwa na kuitwa "Jero"
 
Back
Top Bottom