Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Hii pesa ilitesa sana enzi zake.

Kuna mshkaji alikuwa anaiweka mfuko wa juu wa shati jeupe la shule, halafu anakukuta wewe huna kitu unabaki kuwa mdogo tu.
 
Tulio tumia hizi note tunajua ubora wake, hakika zina ubora sana kuliko zilizopo, pia zinapendeza machoni na zinatangaza utalii wa nchi kwa upande mwingine,
 
Sababu kuu

Thamani ya pesa inatakiwa izidi gharama za matengenezo..hiyo pesa production yake ina thamani kuliko purchasing power yake so lazma waibadilishe

Mfano..
Tsh 100 material yake yangekua makubwa kuliko purchang power yake basi watu badala ya kuitumia kununulia vitu wangeiyeyusha kupata faida zaidi

Ufafanuzi zaid;fikilia hii mia tano ya coin itengenezwe na material yenye thamani ya Tsh. 1,000 watu wangeyeyusha kupata faida mala mbili
 
So kwa kifupi ile jero ya zamani thamani kuitengeneza ni kubwa kuliko vitu itakavyonunua
 
Wengi hatukujua kumbe Sarafu ya East Africa iliwahi kuwepo.wengi tulidhani kizazi hiki ndio kitakuwa waanzilishi.
 
Nashukuru sana kwa kupata historia hii ya matumizi ya noti Tanzania lakini noti tunazotumia sasa zimeshabadilishwa ndogo ikianzia mia tano lakini baada ya uchakavu kuzidi kwenye noti ya mia tano benki kuu ikaona iondoe kabisa mia tano ya noti na kuifanya ya sarafu.
Nahukuru tena.
 
Nashukuru sana kwa kupata historia hii ya matumizi ya noti Tanzania lakini noti tunazotumia sasa zimeshabadilishwa ndogo ikianzia mia tano lakini baada ya uchakavu kuzidi kwenye noti ya mia tano benki kuu ikaona iondoe kabisa mia tano ya noti na kuifanya ya sarafu.
Nahukuru tena.

Peruzi ipo nyingine ya Tsh. ni nzuri pia kufundishia watoto nyumbani hata shuleni.
 
Bora Mkapa hakuweka sura yake kwenye shilingi maana kila rais angekuwa anaweka sura yake katika uongozi wake.
 
MKJJ,

Picha na posts zote hizi hazina copyright protection yoyote ingawa acknowldegement ya jamboforums itakuwa appreciated. Unaweza kuzitumia kwa njia yoyote bila kuhitaji ruhusa ya mtu yeyote yule.

Nadhani kuna typos kadhaa kadhaa. Itakuwa vizuri kama utaweza kuidentify typos na kuniambia kusudi nizirekebisha kabla hujaweka kwenye PDF yako. Hii post ilikuwa ni extension ya historia ya sarafu ambayo nilipost wiki chache zilizopita kama alivyoonyesha Ogah. Nilikuwa motivated na efforts zinazoendelea kwa Afrika Mashariki kutumia sarafu moja.
Darasa halijafungwa bado!! Nnaombea hadi kizazi changu cha tano kiendelee kuelimika na kumbukumbu hii! Hongera Kichuguu (kama bado upo hapa)
 
Mwishoni mwa mwaka 1985 Nyerere alirudi kijijini kwake Butiama na kuiacha Ikulu mikononi mwa Mwinyi. Noti mpya zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 1986 zilikuwa sawa kabisa na zile zilizoacha na Nyerere isipokuwa zilikuwa na sura ya Mwinyi isipokuwa noti zile za Shillingi 100 ambazo ziliendelea kuwa na sura ya Nyerere kama Baba wa Taifa. Vile vile noti mpya ya shillingi 200 ilianzishwa ikiwa inajulika wakati huo kama "double cabin." Nyuma ya noti hizi za Shillingi 200 kulikuwa na wavuvi wanaodhaniwa kuwa walikuwa wa Zanzibar kwa vile kuna karafuu inayoonekana kwa pembeni.

20 Tz Shilling
tz_20shs_mwinyi_1.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_mwinyi1.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_1.jpg


Ilipofika mwaka 1988, kufuatia kushuka kwa thamani ya shilingi, ilikuwa ni muhimu kuwepo kwa noti zenye thamani kubwa zaidi ili kuwapunguzia watu mzigo wa pesa. Hivyo benki kuu ikaanzisha noti mpya za shillingi 500, ambao zilijulikana kama "Pajero." Noti hizi za shillingi 500 zilikuwa na sura tofauti kabisa na zile nyingine. Nembo ya Taifa ilikuwa ya rangi, halafu zilikuwa na nembo ya waziwazi ya Benki Kuu ya Tanzania. Nyuma yake zilionyesha akina mama wakivuna zao la kahawa au karafuu, sikumbuki tafsri ya picha hiyo vizuri.


500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_1.jpg

Kasi ya kupungua kwa thamani ya shilingi ilikuwa kali sana kiasi kuwa miaka miwili baadaye, Benki Kuu ililazimika kuingiza noti mpya ya Shillingi 1000 ambayo ilikuwa na sura kama ile ya Shillingi 500 isipokuwa ngao ya taifa haikuwa ya rangi. Vile vile ilikuwa na maandishi ya ndani kwa ndani kuonyesha 1000. Nyuma yake kulikuwa kiwanda cha nyama cha Tanganyika packers cha pale Kawe.

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_1.jpg

Noti zetu wakati huo zilikuwa pana sana na zilikuwa zinaongezeka upana kadiri thamani yake inavyopanda. Ilipofika mwaka 1992, Benki kuu ilifanya mabadiliko makubwa katika noti zetu. Kwanza zilipunguzwa sana upana halafu zote zikatengezwa upya kuwa na sura inayofanana. Noti ya shillingi 20 iliachisHwa na badala yake zikaongezwa noti mbili za Shillingi 5,000 na Shillingi 10,000 kama ifuatavyo:


50 Tz Shilling

tz_50shs_mwinyi2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_mwinyi_2.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_2.jpg

500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_2.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_2.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mwinyi_2.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mwinyi_2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumiwa hadi mwisho wa utawala wa Mwinyi mwaka 1995.

......INAENDELEA
Saluti babu
 
Baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti za kwanza zenye thamani hizo hizo za Shillingi 5, 10, 20 and Shillingi 100. Upande wa mbele wa noti hizi kulikuwa na sura ya Mwalimu Nyerere wakati wa kupata uhuru, na upende wa nyuma ulionyesha mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania. Noti ya Shillingi 5 ilikuwa na mlima Kilimanjaro, noti ya shilingi 10 ilikuwa na shamba la mkonge, wakati noti ya shilingi 20 ilikuwa inaonyesha mgodi wa almasi wa Mwadui. Noti ya shillingi mia moja ilikuwa inaonyesha morani wa kimasai akichunga ng'ombe wake.

5 Tz Shilling
tz_5shs_nyerere1.jpg

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere1.jpg


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere1.jpg


100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v1.jpg

Kwa waliotumia noti hizo wanakumbuka kuwa noti ya shilingi kumi ilikuwa inajulikana pia kama jani la katani, wakati ile ya 100 ilikuwa inajulikana pia kama Masai au Pink kutokana na rangi yake. Kwa muda mrefu noti ya shilingi ishirini imeendelea kujulikana kama paund au "mbao" kutokana na historia kuwa mwanzoni ilikuwa ina thamani ya Pound 1.

Hata hivyo sura ya masai kwenye noti ilileta mjadala kidogo kiasi kuwa benki kuu iliamua kuzibadilisha. Ilipofika mwaka 1969, wakatoA noti za shillingi 100 ambazo zilikuwa na wanyama katika mbuga ya serengeti kama ionekanavyo hapa chini

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 1978 zilipofanyiwa mabadiliko makubwa hasa ili kuondoa sura ya kitoto ya Nyerere na kuweka picha ya Nyerere akiwa mtu mzima. Noti mpya zote zilikuwa zimendikwa kwa kishwahili tu, na vile vile noti ya shillingi tano ilisimamishwa. Upande wa nyuma wa noti zote kulikuwa na ramani ya Tanzania pamoja na sura mbalimbali zihusuzo Tanzania. Noti ya shillingi 10 ulikuwa na mlima Kilimanjaro, kinyago cha kimakonde na mnara wa Azimio la Arusha; noti ya shillingi ishirini 20 ilikuwa na kiwanda cha nguo kuashiria kuwa nchi ilikuwa inasonga mbele kiviwanda, na ile noti ya shillingi 100 ilikuwa tasisi za elimu kuanzia shule za msingi na vyuo vikuu kuashiria juhudi za nchi kupambana na adui ujinga. Vile vile shughuli za elimu ya kujitegemea zimeonyeshwa kwa wanafunzi kulima kwa jembe la mkono!!

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere_2.jpg

20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_2.jpg

Miaka saba baadaye, mwaka 1985 (muda mfupi sana kabla Nyerere hajastaafu) noti zilifanyiwa mabadiliko tena kwa kuondoa noti ya shillingi 10 na kuwekwa kwa noti ya shillingi 50. Noti hizi zilikuwa na sura ya Nyerere akiwa ameanza kuzeeka, na zilitumia rangi nyingi sana kuliko zilizotangulia. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, noti ya shillingi mia moja ilibadilishwa rangi kutoka "pink" na kuwa ya bluu. Noti ya shilingi ishirini ilionyesha shughuli mbalimbali za baadhi ya viwanda vyetu, wakati shilingi 50 ilionyesha shughuli za kujitolea kujenga mashule. Noti ya shillingi 100 ilionyesha wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama na baadhi ya majengo ya chuo hico. Nadhani ilikuwa pia kuonyesha kuwa nchi imepiga hatua katika upande wa elimu ya juu.


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere3.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_nyerere.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg



.... INAENDELEA
Hiyo noti ya Masai nilikuwa nasikia wakisema ni admu mtu kuwa nayo miaka hiyo ya 1969, maana mshahara wa mwalimu wa msi ngi ulikuwa haufiki shs 30/=.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom