Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Asante mkuu kichuguu heshima kubwa sana kwako huu uzi wako utadumu milele na milele autakuja kuchuja
 
Safi sana, hii ni hazina..

Halafu kuna mamtu yanataka kufungia JF nzima kwa sababu ya Jukwaa moja tu.
Umeona eeh?
Huwa hawapekui na kupata maarifa na historia kama hii kwanza, wanakimbilia kutaka kutuziba midomo. Nyambafu zao
 
hiz
Baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti za kwanza zenye thamani hizo hizo za Shillingi 5, 10, 20 and Shillingi 100. Upande wa mbele wa noti hizi kulikuwa na sura ya Mwalimu Nyerere wakati wa kupata uhuru, na upende wa nyuma ulionyesha mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania. Noti ya Shillingi 5 ilikuwa na mlima Kilimanjaro, noti ya shilingi 10 ilikuwa na shamba la mkonge, wakati noti ya shilingi 20 ilikuwa inaonyesha mgodi wa almasi wa Mwadui. Noti ya shillingi mia moja ilikuwa inaonyesha morani wa kimasai akichunga ng'ombe wake.

5 Tz Shilling (hii enzi hizo ukienda nayo shule ya msingi we ni tajiri wa kutosha)
tz_5shs_nyerere1.jpg

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere1.jpg


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere1.jpg


100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v1.jpg

Kwa waliotumia noti hizo wanakumbuka kuwa noti ya shilingi kumi ilikuwa inajulikana pia kama jani la katani, wakati ile ya 100 ilikuwa inajulikana pia kama Masai au Pink kutokana na rangi yake. Kwa muda mrefu noti ya shilingi ishirini imeendelea kujulikana kama paund au "mbao" kutokana na historia kuwa mwanzoni ilikuwa ina thamani ya Pound 1.

Hata hivyo sura ya masai kwenye noti ilileta mjadala kidogo kiasi kuwa benki kuu iliamua kuzibadilisha. Ilipofika mwaka 1969, wakatoA noti za shillingi 100 ambazo zilikuwa na wanyama katika mbuga ya serengeti kama ionekanavyo hapa chini

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 1978 zilipofanyiwa mabadiliko makubwa hasa ili kuondoa sura ya kitoto ya Nyerere na kuweka picha ya Nyerere akiwa mtu mzima. Noti mpya zote zilikuwa zimendikwa kwa kishwahili tu, na vile vile noti ya shillingi tano ilisimamishwa. Upande wa nyuma wa noti zote kulikuwa na ramani ya Tanzania pamoja na sura mbalimbali zihusuzo Tanzania. Noti ya shillingi 10 ulikuwa na mlima Kilimanjaro, kinyago cha kimakonde na mnara wa Azimio la Arusha; noti ya shillingi ishirini 20 ilikuwa na kiwanda cha nguo kuashiria kuwa nchi ilikuwa inasonga mbele kiviwanda, na ile noti ya shillingi 100 ilikuwa tasisi za elimu kuanzia shule za msingi na vyuo vikuu kuashiria juhudi za nchi kupambana na adui ujinga. Vile vile shughuli za elimu ya kujitegemea zimeonyeshwa kwa wanafunzi kulima kwa jembe la mkono!!

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere_2.jpg

20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_2.jpg

Miaka saba baadaye, mwaka 1985 (muda mfupi sana kabla Nyerere hajastaafu) noti zilifanyiwa mabadiliko tena kwa kuondoa noti ya shillingi 10 na kuwekwa kwa noti ya shillingi 50. Noti hizi zilikuwa na sura ya Nyerere akiwa ameanza kuzeeka, na zilitumia rangi nyingi sana kuliko zilizotangulia. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, noti ya shillingi mia moja ilibadilishwa rangi kutoka "pink" na kuwa ya bluu. Noti ya shilingi ishirini ilionyesha shughuli mbalimbali za baadhi ya viwanda vyetu, wakati shilingi 50 ilionyesha shughuli za kujitolea kujenga mashule. Noti ya shillingi 100 ilionyesha wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama na baadhi ya majengo ya chuo hico. Nadhani ilikuwa pia kuonyesha kuwa nchi imepiga hatua katika upande wa elimu ya juu.


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere3.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_nyerere.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg



.... INAENDELEA
hizi na mimi nilipata bahati ya kusitumia nikiwa shule ya primary(early 1980s) na secondary (late 1980s)

H






0
 
Mwishoni mwa mwaka 1985 Nyerere alirudi kijijini kwake Butiama na kuiacha Ikulu mikononi mwa Mwinyi. Noti mpya zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 1986 zilikuwa sawa kabisa na zile zilizoacha na Nyerere isipokuwa zilikuwa na sura ya Mwinyi isipokuwa noti zile za Shillingi 100 ambazo ziliendelea kuwa na sura ya Nyerere kama Baba wa Taifa. Vile vile noti mpya ya shillingi 200 ilianzishwa ikiwa inajulika wakati huo kama "double cabin." Nyuma ya noti hizi za Shillingi 200 kulikuwa na wavuvi wanaodhaniwa kuwa walikuwa wa Zanzibar kwa vile kuna karafuu inayoonekana kwa pembeni.

20 Tz Shilling
tz_20shs_mwinyi_1.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_mwinyi1.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_1.jpg


Ilipofika mwaka 1988, kufuatia kushuka kwa thamani ya shilingi, ilikuwa ni muhimu kuwepo kwa noti zenye thamani kubwa zaidi ili kuwapunguzia watu mzigo wa pesa. Hivyo benki kuu ikaanzisha noti mpya za shillingi 500, ambao zilijulikana kama "Pajero." Noti hizi za shillingi 500 zilikuwa na sura tofauti kabisa na zile nyingine. Nembo ya Taifa ilikuwa ya rangi, halafu zilikuwa na nembo ya waziwazi ya Benki Kuu ya Tanzania. Nyuma yake zilionyesha akina mama wakivuna zao la kahawa au karafuu, sikumbuki tafsri ya picha hiyo vizuri.


500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_1.jpg

Kasi ya kupungua kwa thamani ya shilingi ilikuwa kali sana kiasi kuwa miaka miwili baadaye, Benki Kuu ililazimika kuingiza noti mpya ya Shillingi 1000 ambayo ilikuwa na sura kama ile ya Shillingi 500 isipokuwa ngao ya taifa haikuwa ya rangi. Vile vile ilikuwa na maandishi ya ndani kwa ndani kuonyesha 1000. Nyuma yake kulikuwa kiwanda cha nyama cha Tanganyika packers cha pale Kawe.

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_1.jpg

Noti zetu wakati huo zilikuwa pana sana na zilikuwa zinaongezeka upana kadiri thamani yake inavyopanda. Ilipofika mwaka 1992, Benki kuu ilifanya mabadiliko makubwa katika noti zetu. Kwanza zilipunguzwa sana upana halafu zote zikatengezwa upya kuwa na sura inayofanana. Noti ya shillingi 20 iliachisHwa na badala yake zikaongezwa noti mbili za Shillingi 5,000 na Shillingi 10,000 kama ifuatavyo:


50 Tz Shilling

tz_50shs_mwinyi2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_mwinyi_2.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_2.jpg

500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_2.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_2.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mwinyi_2.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mwinyi_2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumiwa hadi mwisho wa utawala wa Mwinyi mwaka 1995.

......INAENDELEA
Asante kwa darasa mkuu....nimekumbuka mbali sana yaani mimi nilianza kuiona 200 hii such a good memories

Sent from my Iphone 7 plus using JamiiForums app
 
Ilikiwa na mstari wa siri wenye maneno,benki kuu ya Tanzania.

Maandishi madogo sana,yakiwashinda kabisa jamaa wazee wa kopy.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom