Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

mkuu m nna noti za shilling 20 na 100 vp naweza kuzirudisha benki kuu


Kichuguu
Zitunze za kumbukumbu tu; sheria ni kuwa kuna siku ya mwisho ya kubadilisha hel, ukichelewa basi unabaki nazo kama makaratasi tu. Mabadiliko ya noti yalaiyofanywa mwaka 1985 yalifanyika kwa muda mfupi sana ili watu waliokuwa wameficha fedha za uhujumu wakwame kuzibadilisha na hivyo kuziondoa kwenye mzunguko. Kuna watu walilia sana
 
1000tzn money is 0 bob kenyan money
This is due to misunderstanding the difference between the value of money, its decimalization and the exchange rate. When a country devalues its currency, basically it changes its decimalization, but that does not technically mean that the value has decreased; in fact it can increase the value of that currency depending on the local economy. That is why China is blamed for devaluing its currency frequently. The value of any currency is determined by its demand in the world; if the Kenyan currency has high demand in the world markets, then its value increases irrespective of the exchange rate. For now although the exchange rate between the Japanese Yen and the Kenyan Shilling is almost 1:1, the Japanese Yen has higher value than the Kenyan shilling because of the Japanese economy.

Of course this principle does not apply to failed economies like Zimbabawe.
 
Baada ya kuusoma huu Uzi nikaenda kufumua makabrasha ya mzee wangu...hizi noti zote zipo kuanzia hizo za muingereza za mwishoni mwa miaka60 na kuja mpaka hizo za nyerere kabla ya kubadilishwa na mzee Mkapa..
Inshort hizo fedha (noti)mzee wangu anazo amezihifadhi Ila kwa Sasa sijui zitakua na thamani ya kiasi gani ningependa kulijua Hilo...na je naweza kuzipeleka Bot kuzibadilisha!
Ahsante kwa Uzi mzuri Sana!
 
Baada ya kuusoma huu Uzi nikaenda kufumua makabrasha ya mzee wangu...hizi noti zote zipo kuanzia hizo za muingereza za mwishoni mwa miaka60 na kuja mpaka hizo za nyerere kabla ya kubadilishwa na mzee Mkapa..
Inshort hizo fedha (noti)mzee wangu anazo amezihifadhi Ila kwa Sasa sijui zitakua na thamani ya kiasi gani ningependa kulijua Hilo...na je naweza kuzipeleka Bot kuzibadilisha!
Ahsante kwa Uzi mzuri Sana!
Nasubiri majibu ya wadau
 
Andiko zuri sana hili. nimelipenda. Keep the move.




Only Sky and not Shy is the limit. provided the universe is one. Things will go backforward to backfuture our developments.


Let give Support to this regime to prove to world why they should be granted to rerun in 2025 AGain MoRe.



Rgds,



GaK*!
 
Wakati Mkapa alipochukua usukani wa kuongoza nchi, aliamua kusitisha matumizi ya sura za viongozi kwenye noti. Kwa hiyo noti zote zilizotolewa mwaka 1997 chini ya utawala wake hazikuwa na sura ya kiongozi yeyote. Badala yake zilikuwa na kichwa cha Twiga ambaye ni kihistoria ndiye mnyama wa taifa. Wakati huo pia, noti za shillingi 50, 100 na shillingi 200 zilisimamishwa.

500 Tz Shilling
tz_500shs_mkapa_1.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_1.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mkapa_1.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mkapa_1.jpg

Hata hivyo baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999, iliamuliwa kuwa sura yake iwe ya kudumu kwenye noti ya Shillingi 1000, hivyo noti hiyo ilisanifiwa upya na kuwa kama ifuatavyo

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_1_-v2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 2003 zilipofanyiwa mabadiliko ya kuongeza usalama zaidi. Vile vile kutokana na manunguniko ya kichinichini kutokea zanzibar kuhusiana na mtumizi ya Twiga ambaye alikuwa mnyama wa Tanganyika, iliamuliwa kutotumia twiga tena. Badala yake sura za wanyama wakubwa mbalimbali wa Tanzania zilitumika ingawa sura ya Nyerere iliendelea kubaki kwenye noti za Shillingi 1000. Vile vile noti mpya ya Shillingi 2000 ilianzishwa. Upande wa nyuma wa noti hizi ulionyesha shughuli mbalimbali za uchumi, sehemu za kihistoria na harakati za kukuza elimu . Kwa mara nyingine tena kuanzia mwaka 1978, noti hizi ziliandikwa kwa Kiingereza na Kishwahili tena. Noti hizi ndizo zinazotumika hadi leo, sura zake ni kama ifuatavyo

500 Tz Shilling
tz_500shs_mkapa_2.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_2.jpg

2000 Tz Shilling
tz_2000shs_mkapa.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mkapa_2.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mkapa_2.jpg



TAMATI
Kweli umefanya jambo la maana sana. It is very rare kukutana na kumbukumbu kama hii. Umeniongezea kitu in life
 
Hivi kwanini viongozi wetu kutoka awamu ya nne,tano na sasa ya sita hawataki kuchapisha noti mpya zenye nyuso zao? Kuna nini nyuma ya pazia!??

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwanini viongozi wetu kutoka awamu ya nne,tano na sasa ya sita hawataki kuchapisha noti mpya zenye nyuso zao? Kuna nini nyuma ya pazia!??

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Nchi zilizo nyingi, kwenye noti zinachapwa picha za waasisi wa taifa ama alama muhimu za Taifa. Kwenye dola ya Marekani kuna picha ya George Washington, kwenye Rand ya Afrika Kusini wamemweka Mandela, Uingereza walimweka Malkia, nk. wenye uelewa zaidi watafafanua
 
Hata hivyo mwaka 1958, noti hizo zilitengezwa upya katika mtindo tofauti na zile zilizokuwapo mwanzo. Noti mpya zilikuwa na rangi nyingi huku zikionyesha mazao mbali mbali ya uchumi yaliyokuwapo Afrika ya Mashariki. Noti ya shillingi 5 ilionyesha pamba na karafuu; noti ya shillingi 10 ilionyesha mkonge na chai; noti ya shillingi 20 ilionyesha kahawa na alizeti, na mwisho noti ya shillingi 100 ilionyesha minazi, miwese na pareto. Inaelekea kuwa kuanzia hapo, shillingi ya Afrika mashariki iliacha kubebeshwa kwenye pound kwa vile noti mpya hazikuwa na thamani ya pound tena.


5 EA Shilling
ea_5shselizabeth2_2.jpg

10 EA Shilling
ea_10shselizabeth2_2.jpg

20 EA Shilling
ea_20shselizabeth2_2.jpg

100 EA Shilling
ea_100shselizabeth2_2.jpg


Noti hizi ziliendelea hadi baada ya uhuru ingawa mwaka 1961 zilifanyiwa marekebsihao madogo kwenye sura ya mbele ili kuweza kuonyesha sahihi sita za wajumbe wa bodi ya fedha ya afrika mashariki ambapo wakati huo walikuwa wameongezeka na kuwa sita kutoka watano waliokuwapo mwaka 1958. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo


5 EA Shilling
ea_5shselizabeth_2_3.jpg

10 EA Shilling
ea_10shselizabeth2_3.jpg

20 EA Shilling
ea_20shselizabeth2_3.jpg


100 EA Shilling
ea_100shselizabeth2_3.jpg



Baada ya nchi zote za Afrika ya Mashariki kuwa huru, noti za kwanza zilizotolewa mwaka 1964 zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana. Kwanza, noti hizi zilikuwa zimeandikwa katika kiingereza, kiarabu na kishwahili; halafu sura ya mtawala wa uingereza iliondolewa na badala yake kuwekwa mashua. Sikuweza kufahamu mara moja kwa nini waliamua kutumia mashua. Sura za nyuma za noti ziliendelea kuonyesha mazao mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ingawa kwa mpangilio tofauti kama inonekanavyo katika picha hizi.


5 EA Shilling
ea_5shs.jpg

10 EA Shilling
ea_10shs.jpg

20 EA Shilling
ea_20shs.jpg

100 EA Shilling
ea_100shs.jpg


..... INAENDELEA
 
Back
Top Bottom