Historia ya neno Msela na Baharia

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,926
12,472
Miaka ya nyuma watu walikuwa wakijiita masela kutokana na kuwaiga watu waliokuwa wamepanda meli na kwenda ulaya.

Sailor "msela" ni mfanyakazi wa meli ambaye sio ofisa au baharia wa kawaida.
Huyu ni mtu ambaye alikuwa amesafiri sana na meli kipindi hicho.

Ambapo walikuwa wakirudi Tanzania wanakuja na vitu vya thamani kama cheni,saa,viatu na nguo. Pia walipenda kuninginiza cheni na miondoko yao ilikuwa ni ya kutembea kwa kudunda kutokana na kuishi kwenye meli ambapo muda mwingi walikuwa wakivaa safety booty kubwa na ile hali ya chombo kuyumba kutokana na wimbi.

Kipindi cha sasa vijana wengi wanajiita "Baharia" hii ni kutokana na mabaharia kuwa watu wa kusafiri kila eneo, kusaidiana,kuweka kambi popote na kwenye mahusiano baharia kuwa na mahusiano ya kimapenzi kila sehemu atayofika ambapo kipindi cha nyuma walikuwa wakitumia msemo wa "New Port, New Wife".

Hii imepelekea sasa vijana wengi mtaani na kwenye kada mbalimbali kutumia neno la baharia au kujiita baharia.

Impressment-of-sailors-3000-3x2gty-58b60eca5f9b586046563592.jpg
 
Msela = Sailor

Hilo lilitokana na meli na majahazi ya zamani ya mizigo na abiria kutumia matanga "sailing". Mfanyakazi wa hizo meli na jahazi za matanga ndio "sailor" kwa Kiswahili wakamuita "msela",

Baharia = Seaman

Meli na majahazi ziliposita kutumia matanga na kutumia nishati zingine mbadala ndiyo ikawa hao wafanyakazi humo huitwa mabaharia au Seaman kwa kuwa hawa "sail" tena.
 
Meli na majahazi ziliposita kutumia matanga na kutumia nishati zingine mbafala ndiyi ikawa hao wafanyakazi humo huitwa mabaharia au Seaman kwa kuwa hawa "sail" tena.
Kama hawajaelewa basi tena DMI hoyeeee
 
Msela = Sailor

Hilo lilitokana na meli na majahazi ya zamani ya mizigo na abiria kutumia matanga "sailing". Mfanyakazi wa hizo meli na jahazi za matanga ndio "sailor" kwa Kiswahili wakamuita "msela",

Baharia = Seaman

Meli na majahazi ziliposita kutumia matanga na kutumia nishati zingine mbadala ndiyo ikawa hao wafanyakazi humo huitwa mabaharia au Seaman kwa kuwa hawa "sail" tena.
Kwa maana nyingine huyu mleta mada tunaweza mwita "offshore baharia"
 
Msela = Sailor

Hilo lilitokana na meli na majahazi ya zamani ya mizigo na abiria kutumia matanga "sailing". Mfanyakazi wa hizo meli na jahazi za matanga ndio "sailor" kwa Kiswahili wakamuita "msela",

Baharia = Seaman

Meli na majahazi ziliposita kutumia matanga na kutumia nishati zingine mbadala ndiyo ikawa hao wafanyakazi humo huitwa mabaharia au Seaman kwa kuwa hawa "sail" tena.
Uko sahihi, ila teknolojia ya matanga sasa inatumika kama mbadala kwenye meli zinazotumia mafuta ili kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama za uendeshaji.
 
Wakuu saiv ni bora kuwa Baharia kuliko kuwa na stress ndani unang,aramikia matatizo na unakuja kuishi nayo ndani
World is change in generally ,? Waendelee ktaka usawa na kufagilia mfumo dume
Wanawake 99 percent na hopeless wanaiga life stlye na kupretend maisha we can't move on
Vichwa vya kuku kamwe hakibebi mzigo
UVUMILIVU WA KUSHINDA UKWELI UTASHINDA LEO KAMA SI KESHO
Mwanume we will remain best and ever coz God create us as leader in this world so women is our helpers
 
Nimepata taabu sana kuelewa ulichoandika, ila pole inaonekana umefanyiwa unyama wa kihisia.
 
Back
Top Bottom