Historia ya mtandao wa kifisadi baina ya william ngeleja, rostam aziz, pius msekwa

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Ndugu Wana JF,

Napenda kutoa mwanga na historia ya waziri wa Nishati na madini Bwana William Ngeleja na mtandao wa kifisadi wa Rostam Aziz na Pius Mswekwa. Bwana Ngeleja aliwekwa na mafisadi kama mwanasheria wa VODACOM (T) LTD mpaka mwaka 2005, chini ya wakurugenzi wake akiwamo ROSTAM AZIZ, PIUS MSEKWA kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Peter Noni kama wakurugenzi wazalendo wa VODACOM.

Mwaka 2005, mtandao wa kifisadi uliweka azimio wa kuandaa vijana wa kazi ambao wataweza kuendeleza kazi ya kulinda maslahi yao, na ROSTAM AZIZ kama key player wa mtandao huo alimshawishi bwana william Ngeleja kwenda sengerema kugombea ubunge na mtandao utakuwa nyuma yake kumwezesha kwa hali na mali ili aweze kupata ubunge na hatimae kuingia bungeni kuongeza nguvu ya mafisadi.

Bwana William Ngeleja alikwisha nunuliwa na mtandao wa mabosi wake wa zamani pale VODACOM alipokuwa mwanasheria wa VODACOM, hivyo basi kwa watu wasio mfahamu vizuri William Ngeleja wanafikiri kuwa amekuwa waziri wa Nishati na madini kwa bahati mbaya, hiyo ni calculated move ya mtandao wa mafisadi ambao amekuwa nao karibu na kufanya nao kazi mda mrefu.

Hivyo kitendo cha Ngeleja kuwa Waziri wa nishati na madini na kuendelea kukingia kifua deal za mafisadi kama anavyo endelea kufanya hivi sasa kwenye deal ya DOWANS na kufanya jitihada kubwa kuzika mapendekezo ya kamati ya bunge ya Kashfa ya RICHMOND ili kuwalinda ma GODFATHER wake waliomweka hapo alipo.

Mimi binafsi nilikwisha fanya kazi na William Ngeleja ni mtu ambae hawezi kuwa na independent mind na kufanya decision zenye maslahi ya taifa, ni mtu anaependa kujipendekeza na kunyenyekea bila kuwa na reasoning na independent decision.

Hivyo mafisadi wataendelea kutusumbua kwa sababu JK alikwisha tengeneza mtandao mkubwa sana kwa kila sector ya uchumi wa nchi hii, tulimwajibisha Nazir Kalamagi, msabaha na Lowassa walioletwa ni vijana wao wa kazi wakina William Ngeleja, Matayo David, Adam Malima, Lawrence masha na wengine wengi wengi.
 
Mkuu haya yanajulikana, nilitegemea unakuja na kitu kipya kabisa, anyway wenye data wataweka,
 
Kweli kabisa, wengine tulikuwa hatujui hili! Ametufumbua macho na kuweka tafakuri kwenye akili zetu!
 
Kabla ya kugombea ubunge waziri wa Nishati na Madini alikuwa mwanasheria wa Vodacom akiwa chini ya Ndgugu Godwin Ngwilimi,wakati huo Muiran Rostam akiwa mmiliki mkuu wa Vodacom,

Du full connection;
 
oyi hapo jombaa nchi hii na mora sasa tuamue kuandamana je nani atachukua nini mimi hawa majamaa wananikera kama vile nchi ni yao peke yao
 
Kila mmoja kujua hakutoshi, ni muhimu sana kukumbushana. Wengine wamesahau au hawakusikia kabisa, hivyo hii ni nzuri sana. Zaidi mafisadi watapenda tusahau
 
jamani baharini usiseme twafa sema nafa , hapa sema najua usiseme wote wanajua , mimi ndiyo kwanza nayaona leo acha nikugongee thanx
 
Back
Top Bottom