historia ya miaka 50:Viongozi wa kiafrika na jinsi ya kuwagawa kimakundi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

historia ya miaka 50:Viongozi wa kiafrika na jinsi ya kuwagawa kimakundi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Oct 27, 2011.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Matatizo ya kiuongozi siyo mageni hapa barani Afrika na ikiwa nchi nyingi zinasheherekea na zitasherehekea miaka 50 ya uhuru,(nyingi zilipata uhuru miaka ya 60) basi ningependa tuwachambue wale wale viongozi waliziongoza na tujaribu kuwaweka katika makundi mahsusi kutokana na sifa zao binafsi na zile za kiuongozi

  Predators/ kama wanyama

  Jean Bokassa wa Afrika ya Kati (kujifanya mfalme na kutumia hazina yote ya nchi kwenye sherehe hizo, kufunga chuo kikuu, kurushia watu kwenye mamba wake wa kufuga, kuoa wanawake kila anapoenda na kula watu)
  Idi Amin (tunamuelewa vizuri)
  Francias Macias Nguema wa Equatorial Guinea) (kujifanya ni mchawi ili aogopwe na watu wake, kufunga shule na vyuo vyote na kuhamisisha wananchi wake wasipate elimu kwani ni mbaya, kuchukua pesa zote benki kuu na kuzihamishia kijijini kwake, kuua watu, kuwala ikiwemo mawaziri wake)

  Criminals/wahalifu
  Teodoro Nguema wa Equtorial Guinea(ndugu wa Nguema mwingine hapo juu)-mhalifu anayechukua pato lote la taifa yeye na familia yake, kujaza wanafamilia kwenye sehemu zote nyeti za serikali, mauaji ya wapizani
  Paul Biya wa Cameroon-kugawanya nchi katika sehemu mbili za kusini na kaskazini ili aongoze vizuri, wizi uliokubuhu, hulka ya kukaa Ufaransa hata miezi 3 bila ya kurudi nyumbani, kuhamasisha uhalifu nchi nzima
  Sani Abacha wa Nigeria-aliiongoza nigeria kwa miaka 4 tu lakini inasemekana alikufa akaacha $4 bil, alikua hatoki ikulu wala kukutana na wanahabari, kuleta wanawake wa kumburudisha toka Ulaya na Asia n.k
  Samuel Doe wa Liberia-kucheza bao siku nzima, kula nyama ya mtu anayempinga ili apate nguvu zake, kutumia fedha zote za misaada kibinafsi
  Omar Bongo wa Gabon-kubadilisha dini ili aoe wake wengi, kutaka kubaka miss mmoja toka nchi za kilatin Amerika aliyemualika katika hafla ikulu, kusaini mikataba ambayo hela za mafuta zinapitia katika akaunti yake binafsi
  Mobutu Sesseko-tunamjua vizuri
  Charles Taylor- nafikiri tunamjua
  Gnassibe Eyadema wa Togo-muuaji wa sylvanus Olympio, kurithisha kiti cha urais kwa mwanae, uzinzi uliokufuru na wizi wa waziwazi
  Isaias Afewerki wa Eritrea-mhalifu anayeleta matatizo nchi za jirani ili aendelee kunyanyasa watu wake
  hapa list ni ndefu sana akina Gaddafi, Meles Zenawi(ethiopia), Nguesso sassou (congo-brazaville),Omar al Bashir (sudan) etc

  Hustlers/wazee wa mipango mjini
  comrade Mugabe nimemsamehe kumuweka hapa nafikiri anafaa kukaa hapo juu na criminals wenzake kwa kile anachowafanyia wananchi wake na kwa mauaji ya halaiki kule Bulawayo miaka ya 80. Kwa sasa Bob amekua mzee wa mjini piga dili hapa na pale kutumia mke wake
  Jomo Kenyatta-aliwahusstle wenzake akina Jaramogi Odinga, na kumdhuru Tom Mboya waliopigania nae uhuru akawa mzee wa mali na familia yake kupitia mke wake Ngina na kakikundi chake cha kikabila. nimemuonea huruma ya ujirani ukichukulia mauaji ya JM Kariuki ingefaa akae na criminals hapo juu
  Ben Mkapa-na mengi ya kusema hapa? labda moja kuupaisha ufisadi hadi kua tatizo la kitaifa
  Yoweri Museveni-tunamjua
  Mswati III- mzee wa totoz, ameifilisi nchi kwa kutumia kigezo cha tamaduni za kifalme
  D. Arap Moi-aliiba akaiharibu Kenya na mwisho kwa sababu alikua anawazidi ujanja akwaambia naachia urais ila nisiguswe na familia yangu wakamkubalia akawasainisha akaacha.hii ni Phd ya usanii
  JK-huyu bwana tunamuangalia tunaweza tukampandisha hapo juu hospitali zikishiwa madawa na watu wakianza kufa wakati yeye anasafiri kila siku
  Jacob Zuma-kama Jk tu ana bahati kauchumi kule kako imara kidogo, ushikaji mwingi, totoz luluki, kazi hakuna, ANC haishi migogoro, nk
  na wengineo wengi wa namna hii

  Saints/wazalendo wa ukweli

  JK nyerere-sina mengi ya kumuongelea
  Mandela-pia huyu sina mengi
  Thomas Sankara-Nyerere wa Burkina Faso
  Sir Quett Masire-kainyanyua Botswana toka ilipokua nchi maskini hadi hapo ilipo kiuchumi na kidemokrasia, mzalendo wa kweli angeweza kujipa utajiri wa almasi lakini aliweka nchi mbele kwanza

  Kagame yuko njiani kuingia katika kundi hili kama ukabila ukipungua (inasemekana ameupunguza kwa kiasi kizuri) na uchumi ukiendelea kukua huku taratibu akianza kuruhusu dekokrasia na media

  Tunataka rais wa awamu ya 5 ajifikirie kua saint wa African politics and leadership
   
Loading...