Historia ya Mgogoro kati ya Wilaya ya Ngara kati ya Wakulima na Wafugaji(Wanyarwanda) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia ya Mgogoro kati ya Wilaya ya Ngara kati ya Wakulima na Wafugaji(Wanyarwanda)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by QUALITY, Jun 21, 2011.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  habari toka Ngara: Historia ya Mgogoro kati ya Wilaya ya Ngara kati ya Wakulima na Wafugaji(Wanyarwanda)

  Watanzania wanapokuwa watumwa katika nchi yao……….

  Mnamo mwaka 2008 Wilaya ya Ngara ilianza kuvamiwa na wafugaji maarufu kama Wahima waliotoka Wilaya ya jirani ya Karagwe baada ya kufukuzwa na Serikali na baadhi walitoka nchi ya jirani ya Rwanda.
  Mnamo mwaka 2009 mifugo ya wafugaji ilizidi kuongezeka na maeneo ya malisho yakawa finyu ndipo wafugaji wakaanza kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima kwa ubabe na kiburi huku wakiwatishia wakulima kuwa hawana lolote la kuwafanya watawapiga na kuwauwa kwani wao wanamifugo mingi ya kuwahonga viongozi wa serikali.
  Mgogoro huu ulipelekea wananchi wawili (2) kuuwawa kifo cha kinyama cha kipigwa na mawe baada ya kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mauaji haya yalifanyika katika kitongoji cha Ngoma Kijiji cha Kasulo Novemba 2009. Kati ya wananchi hao, mmoja baada ya kupigwa sana na kutokufariki alichomwa mkuki wa kifuani mpaka mauti yake. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mgogoro kati ya Wakulima wa Kitanzania na Wafugaji wa Kinyarwanda.

  Wananchi waliripoti mauji hayo kituo cha polisi na kwa Mkuu wa Wilaya lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa wafugaji hao. Kutokana Serikali kutokuchukua hatua yoyote kiliwakasilisha wananchi na kuamua kujichukulia hatua ya kuwasaka Wanyarwanda popote waliopo na kukata kata mifugo yao kwa mapanga. Wanyarwanda wakaripoti tukio hilo kituo cha polisi, msako mkari ulifanywa na jeshi la polisi kuwatafuta wakulima waliokata kata mifugo ya wanyarwanda. Hii ililetezea wananchi wa kitongoji cha Ngoma kuandamana kulekea kituo cha polisi kwa kile walichokua wanadai pindi wakiripoti mauji yafanywayo na wafugaji wa Kinyarwanda hakuna hatua zozote zinazochukuliwa lakini wanyarwanda wakiripoti juu ya kukatwa katwa kwa mifugo yao hatua kali zinachuliwa na Jeshi la Polisi. Madai makuu yakiwa kipi bora kati ya uhai wa mnyama au uhai wa mwanadamu?. Maandamano hayo yalichukua muda wa masaa sita kama kawaida ya Jeshi la polisi la Tanzania maandamao yale yalivunjwa kwa mabomu ya machozi na risasi baridi na kukamwatwa kwa baadhi ya wananchi waliondamana.
  Mgogoro huu ulitatuliwa na RPC wa Mkoa wa Kagera Mr. Endrew Salewi kwa kuwakutanisha wakulina na wafugaji na kuwaachia wanachi waliowekwa rumande, Mgogoro huu uliendeleza chuki zaidi kati ya Wakulima na Wafugaji.

  Mwaka 2010 katika kitongoji kashabula kijiji cha Kasulo, wafugaji wa Kinyarwanda walimuua mwanachi mmoja. Mgogoro ulikuwa mkubwa sana wananchi wakidai wanyarwanda watoke nchini kutokana na mwendelezo wa mauaji wanayoyafanya na kitendo chao cha kulisha mifugo katika mazao yao, kunywesha ngombe zao katika visima vya wanachi wavitumiavyo kwa maji ya kunywa na matumizi mengine, pia kauli mbovu wanazozitoa wafugaji wa Kinyarwanda kwa wananchi kua wao wanawasilina na Ikulu sio wao. Mnamo mwezi wa March 2010 wa kijiji cha kasulo waliamua kuandamana tena kuelekea kwa mkuu wa Wilaya ili kuwasilisha kilio chao na kutoa notisi ya siku 20 Wanyarwanda wote walio katika Wilaya ya Ngara waondoke mara moja. Katibu Tarafa wa Nyamihaga alizima maandamano hayo na kuwaomba wananchi wawaongezee muda wa notisi ya kuondoka kwa wanyarwanda hadi mwezi mmoja.

  Taarifa ambazo hazijathibitishwa, wananchi waliaandaa mishale, mikuki na mapanga ili muda wa notisi ukifika kama serikali haitachukua hatua yoyote wao wachukue jukumu la kuwaodoa kwa nguvu na kukatakata mifugo yao. Taarifa hizo ziliwafikia wanyarwanda nao wakaingia msituni na vijana 28 kuwafundisha mbinu za kivita ili wapambane na wananchi kwani hawako tayari mifugo yao iuwawe ni bora watanzania wafe.
  Taarifa hizi za kiintelejensia ziliifikia kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ambayo mwenyekiti wake ni mkuu wa Wilaya. Mnamo tarehe 7/5/2010 Mkuu wa Wilaya aliamua kuitisha mkutano kati ya wakulima na wafugaji ili kutatua mgogoro huu. Kabla ya mkutano huu, ulifanyika mkutano wa ndani kati ya viongozi wa wilaya, viongozi wa serikali ya kijiji cha Kasulo na wajumbe wake. Katika mkutano huo mkuu wa Wilaya aliwafukuza wajumbe wa serikali ya kijiji na kuwaalika wafugaji wa Kinyarwanda wapatao nane (8). Inasemekana katika Mkutano huo wa ndani Mkuu wa Wilaya alipewa fedha (milioni 300 na kuahidiwa million 150 baada ya mkutano wa hadhara) na Wanyarwanda ili kuzima mgogoro huo, kitendo hiki kiliwakasilisha sana wananchi na kuapa kuwa watapambana nacho.

  Baada ya mkutano huo wa ndani Mkuu wa Wilaya alimwita Mwenyekiti wa Kijiji na kumpa vitisho vingi sana ili awaache Wanyarwanda waendelee kuchunga mifugo yao katika ardhi ya Tanzania,Mwenyekiti wa Kijiji alimjibu Mkuu wa Wilaya kuwa yeye hana uwezo wa kumjibu lolote ila kama anataka hayo maneno akawaambie wanachi yeye mwenyewe. Baada ya majibizano hayo Mkuu wa Wilaya aliitisha mkutano wa wananchi ikiwa na lengo kuu la kuwaponda na kuwapa vitisho wananchi waache kuwafuatilia Wafugaji wa Kinyarwanda. Katika mkutano huo alihudhuria mwakilishi wa ITV/Radio one, Mkuu wa Wilaya baada ya kuona kuna mwandishi wa habari akaogopa kuhutubia na kuwatuma OCS na mwenyekiti wa kijiji wamuondoe katika mkutano huo. Mwandishi aliwakatalia kuondoka akidai huo ulikua ni mkutano wa hadhara hivyo anaruhusiwa kuhudhuria kama mwanachi pia kama mwandishi. Baada ya kuwajibu hivyo wakamplekea taarifa Mkuu wa Wilaya, kwa jazba akasimama na kumualisha aondoke na kuwauliza wananchi “Nataka huyu aondoke”wananchi wakamjibu kama ukimuondoa huyo nasi tunaondoka. Kwa jazba tena akasimama na kuwaambia wananchi anayetaka kunisikiliza mimi akae chini na anetaka kuondoka anyanyuke haraka aondoke. Zaidi ya wananchi 700 wakaondoka wakimfuta mwadishi wa habari na mkutano ule ukavunjika. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mwandishi wa habari wa ITV Ngara kuandamwa na kesi zisizoisha dhidi ya Jamuhuri kuwa yeye si raia na kwamba anatakiwa kuondoka wilayani hapo.

  Tarehe 11/5/2010 taarifa ile ilitoka katika kituo cha ITV ilielezea sakata zima na wananchi wakitoa malalamiko yao jinsi wanavyoonewa na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na Serikali. Mnamo tarehe 12/5/2010 ikiwa ni siku moja baada ya taarifa ile kutoka mwandishi wa ITV/Radio one alipokea barua toka Idara ya Uhamiaji wilaya ya Ngara ikimwambia kuwa yeye sio Mtanzania, wale wananchi sita (6) walioonekana kwenye ITV wakihojiwa wakabambikiwa kesi ya kukutwa na gongo, bangi na uwizi mpaka sasa kesi ziko mahakamani.
  Kutokana na kubambikiwa kesi kwa wananchi walioonekana katika kituo cha ITV na mwandishi wa habari kuhojiwa na Idara ya uhamiaji, wananchi wa kijiji cha kasulo wakapata woga mkubwa na kuacha kuhoji tena kuhusu uvamizi wa Wanyarwanda na kuishi kwa wasiwasi wakiogopa kumbambikiwa kesi.
  Kwa upande wa pili Wanyarwanda waliongeza kiburi na kuanza kuwaita wafugaji wenzao katika Wilaya za Misenyi, Muleba, Biharamulo, na wengine toka nchi ya Rwanda. Hii ililetezea kuongezeka mifugo kwa wingi zaidi katika Wilaya ya Ngara kuliko uwezo wake. Kwa taarifa ambazo hazijathibitishwa kadri mifugo ilivyokua inaongezeka ndivyo viongozi wa serikali hasa Mkuu wa Wilaya alivyozidi kupewa rushwa zaidi ili kumzima mdomo na kuwakingia kifua wafugaji.
  Maeneo ya kulima kwa wakulima yakazidi kupungua zaidi kutokana na serikali kugawa maeneo hovyo bila utaratibu wowote kwa wafugaji na kuwaacha wakulima wakikosa maeneo yao ya asili kwa ajili ya kilimo. Maeneo yaliyoathirika zaidi na kuvamiwa kwa wafugaji ni katika kata za Rusumo, Murusagamba, Keza, Mganza, Bugarama na kata zote zilizo pembezoni na zenye malisho mazuri.
  Mauji ya Murusagamba:
  Baada ya uvamizi wa tembo katika vijiji vya Murugamba na Mkalinzi wananchi walisimama kulima maeneo hayo kutokana na mazao yao kuliwa na tembo. Waliitwa wanyama pori ili kuwafukuza tembo hao. Baada ya zoezi hilo kukamilika wafugaji wa Kinyarwanda wakapewa kinyemela maeneo hayo na serikali. Wananchi wakaanza kulalamika ili warudishiwe maeneo yao ya kulima. Alitwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili atatue mgogoro huo, mkutano wa hadhara ulipangwa kufanyika tarehe 19/5/2011. Mkutano huo haukufanyika kutokana na ujio wa Naibu Waziri wa Maji na Umwailiaji. Wananchi wakaamua kujitwalia maeneo yao ya zamani ili waanze kuyandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo.
  Mnaomo tarehe 30/5/2011 muda wa usiku ndipo wanyarwanda wakawavamia wananchi sita (6) na kuwafunga mikononi na miguuni na kuanza kuwapiga mpaka kuwauwa, mwishowe walitoa macho maiti hizo kwa kweli kilikua ni kifo cha kinyama sana. Siku ya mauaji kulikuwa na wanachi nane (8), wawili walifanikiwa kutoroka.
  Baada ya mauaji viongozi wa polisi walikuja ili kufanya upelelezi wao, wanyarwanda kadhaa walikamatwa. Bado wanachi wanakinyongo na serikali yao kwa kufumbia mauji ya mara kwa mara wayafanyayo wanayrwanda.
  Mnamo tarehe 11/6/2011 kamishina wa Chama Cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Kagera Mr. Mshenyela alitaja orodha ya mafisadi kumi na moja (11) wa Wilaya ya Ngara wanaopokea rushwa kutoka kwa Wafugaji wa Kinyarwanda na kuwatetea. Kinara wa upokeaji wa rushwa hizo kwa mujibu wa Kamishina huyo ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mr.Salumu Nyakonje. Taarifa zilizopatikana kutoka Wilayani zinadai tume toka Wizarani imeshatua Wialaya ya Ngara ili kuchunguza migogoro inayoendelea
  Swali loangu kwa serikali: Haya yote yanatokea wakati wahusika bado wanaendelea kuwepo madarakani. je serikali imeenda likizo?
   
Loading...