Historia ya Mbowe isitumike kubaka Democrasia CHADEMA

Kada Deya

Senior Member
Nov 8, 2011
152
195
MBOWE ATAKA HISTORIA YAKE ITUMIKE KUHALALISHA YEYE KUBAKI MADARAKANI KWA MABAVU KWA KISINGIZIO CHA KULINDA CHAMA

Mbowe anadhani historia yake binafsi katika chadema inaweza kutumika kufunika vitendo vya ubakaji wa democrasia katika chama ikiwa ni pamoja na yeye kunyofoa kifungu cha ukomo wa uongozi wa chama kwenye katiba ya chadema. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mbowe kwa wanafunzi jana wakati akifungua Kanda maalum ya cdm vyuo vikuu kanda ya ziwa angalia kama kuna element yoyote ya kujenga democrasia katika chama, angalia kama hotuba hii inakijenga maslahi ya chama au inajenga maslahi binafsi ya Mbowe?.

Kutokana na hofu ya kufukuzwa na wananchi ulinzi ni wa kutisha mpaka kwenye paa za nyumba. Vijana walikuwa redbrigade walikuwa na hofu sijapata kuona!

Mbowe anaanza hotuba yake akisema wakati wa TANU hakukuwa na computer za kupotosha umma kwenye mitandao.

Anasema alishinikiza Dr Slaa awe katibu mkuu wa chama na akashinikiza kufanya mabadiriko makubwa kabla ya kukubali kuwa mwenyekiti.

Anasema alimulipia nauli Kabuoru nauli toka Marekani na alipokuja alilipwa mshahara na yeye na Ndesemburo

Anatoa siri kwamba siri ya Chadema kutosimamisha wagombea urais, ni kwa sababu Makani na Mtei waligombania kugombea urais mwaka 1995 chama kikaamua kuwatosa!

Anasema wanaosema anataka uongozi ni mpuuzi na mmbea, kazi ya kuongoza chama hiki ni ngumu kwani kifungo ni chako, risasi ni zako na kufirisika!

Anasema ameshambuliwa Arusha kwa bomu la kivita, bunduki za kivita na bastora. Anayesema hatavumiliwa mtu yoyote anayetaka kutoboa mtungi uliyotengenezwa kwa miaka 25 mfululizo.

Anasema Chadema wana msiba Ccm wanalia kuliko Chadema wenyewe. Anasema Chadema iko imara na anayefikiria vinginevyo apime ataona!

Anasema atasimamia nidhamu kwa gharama yoyote. Anasema Mbowe hana kundi wala hana njaa! Hatuwezi kugombania vyeo wakati huu kwani wakipewa nchi watatoana meno.

Ametangaza kwamba chama kitafanya kazi kubwa ya kujenga chama kwa akina mama mwaka 2014. Amemaliza hotuba na anazindua kanda maalum ya vyuo vikuu.

Mpambe wa Mbowe bw. Wenje alipata fursa ya kuongea akasama hivi: Natoa taarifa kuwa jmanne kitaumana bungeni kwani kwani wanataka kujua haki iliyovunjwa ya meye wa Ilemela. Anasema yeye Zitto, Mdee na Mnyika ni product ya Mbowe (ona ujinga wa huyu jamaa product ya mbowe in what context?)

Kuna watu kama mandela ambao wamefanya mambo makubwa kwa nchi zao, kwa Afrika na kwa dunia lakini hawakuwa wabinafsi kama Mbowe. Na viongozi wazuri ni wale wanaojali democrasia si wale wanaobaka democrasia kwa maslahi binafsi.

View attachment 126820
 
lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
637
500
Ukiangalia kwa jicho la mbali bila unafiki,kwa kweli bora tuendelee kuongozwa na ccm kuliko watu hawa,hawana lolote!!ok now mnatuambia ugomvi wa makan na mtei 1995,kipi kilichokuwepo nyuma ya pazia?masilahi binafsi,na ni hayo hayo ndio mbowe unayoyapigania,wadanganyeni watanzania wote,i will b the last kuwa na imani na uongozi wa cdm wa sasa!!shame on you mbowe!!!ni bora ufe kabisa.
 
taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
1,195

Hivi adui wa CCM na watawala wake ni CHADEMA yenyewe ama ni watu fulani hususan Mbowe na Dr. Slaa?. Kwa nini kila mara watawala na chama chao wanatumia kibwagizo cha DEMOKRASIA kama silaha ya kuwashambulia Mbowe na wengineo na sio kujikita katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza makumi ya ahadi walizowaahidi wananchi wa Tanzania?.
 
Kada Deya

Senior Member
Nov 8, 2011
152
195
Hivi adui wa CCM na watawala wake ni CHADEMA yenyewe ama ni watu fulani hususan Mbowe na Dr. Slaa?. Kwa nini kila mara watawala na chama chao wanatumia kibwagizo cha DEMOKRASIA kama silaha ya kuwashambulia Mbowe na wengineo na sio kujikita katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza makumi ya ahadi walizowaahidi wananchi wa Tanzania?.

Mbowe na Slaa wanamaslahi binafsi na chadema na hali hii ndio inakitafuna na kukimaliza chama. Wasipoangalia 2015 huenda cdm ikawa na wabunge wasiozidi wa 2.
 
lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
637
500
Hivi adui wa CCM na watawala wake ni CHADEMA yenyewe ama ni watu fulani hususan Mbowe na Dr. Slaa?. Kwa nini kila mara watawala na chama chao wanatumia kibwagizo cha DEMOKRASIA kama silaha ya kuwashambulia akina Mbowe na Dr. Slaa.Mpendwa,mimi cjui adui wa ccm ni Chadema au la!!nilichoongelea ni kwamba chadema kama taasisi ina misingi imara tu,tatizo ni uongozi.Migogoro yote iliyowahi tokea chadema imemhusisha Mbowe moja kwa moja,na mara zote yeye amekuwa akibaki salama,ckatai yawezekana kabisa yupo sahihi katika maamuzi yake kwenye hiyo migogoro.
Ila ukitizama kwa mbali ukifungua kichwa chako utaona hata anapobainisha historia yake ndani ya chama utaona kuna harufu fulani ya kuonyesha namna alivyogharamika kukifikisha chama hapo kilipo pamoja na wakina Ndesamburo!!
Na hilo limefanya kila kunapokuwepo na migogoro ni lazima yeye awe sahihi na kwa sababu usalama wako CDM unategemea jinsi gani mawazo yako yanaendana na Mbowe,then asilimia kubwa ni wa kumuunga mkono wazi wazi au wanabaki neutral kama wakina Baregu,Prof Safari na wengineo.Narudia tena sababu watanzania tumeichoka ccm na tunahitaji mabadiliko,Mwenyezi Mungu aondoe huo uongozi wa mbowe na Slaa,kwa style yeyote,ikibidi Israel awatembelee tu then hapo ndio cdm ishike dola otherwise ni kudanganyana tu,tutajuta na kusaga meno.
 
mkereketwa89

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
278
250
I believe in change!!na hawa majamaa watatuongoza kwenye mapinduzi ya ukweli..adui wa ccm ni ss watu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Tutawaongezea Mbowe na Dr Slaa miaka kumi halafu baada ya hapo Tutamkabidhi Chama Tundu Lissu kama Mwenyekiti na Mnyika Katibu Mkuu.
 
mwanza_kwetu

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
687
195
Ndio maana akina kambona wakitupwa ni kawaida nyerere usingemtoa ktk msingi kwa kisingizio cha demokrasia pia esp kama unaonekana we w e mamluki
 
lukatony

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
637
500
Tutawaongezea Mbowe na Dr Slaa miaka kumi halafu baada ya hapo Tutamkabidhi Chama Tundu Lissu kama Mwenyekiti na Mnyika Katibu Mkuu.Zungumza kidemokrasia ndugu,acha uzushi!!Kama upo kijana nakwambia cdm chini ya mbowe kamwe haitakamata dola!!!Mnyika it is ok,Lissu no may be ........................
 
kigu

Senior Member
May 27, 2012
183
195
chadema ni chama kidhaifu sana!! hakina viongozi wenye uoni wa mbali na wenye mawazo mbadala wa kuleta mabadiliko ya kweli ktk nchi yetu!!

mbowe '' sijamuona wa kumkabidhi uenyekiti chadema"
Dr Slaa "tukiingia madarakani tutahakikisha gongo inauzwa hadharani na kutengezwa na sido"

halafu kuna wasomi wanawatetea kwa hayo mambo wanayo ya sema
 
MZABIBUASILI

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
287
195
Cjaona maslahi binafsi ya mbowe ila ninachojua amegombea mara 2 tu na akashinda kikatiba kabisa! Na huu ndio muda wake wa mwisho katika uongozi.sasa nashindwa kuelewa hii sympath ya ccm inatoka wapi? Maana jk kagombea mara 2 na akashinda kwa mujibu wa katiba sasa mbona cwasikii mkimwita dictator au ana maslahi binafsi?kiukweli siwaelewi kabisa labda njooni na hoja kuntu kwa kuainisha uhalisia na c porojo za humu jamvini.
 
Usidanganye watu, mbowe hajawahi kugombea, marazote amekuwa akipita bila kupingwa, kila anayeonesha dalili ya kugombea naye anapigwa vita na kupewa majina kama Msaliti, Mhaini , mamluki, anatumiwa na ccm etc
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000
MBOWE ATAKA HISTORIA YAKE ITUMIKE KUHALALISHA YEYE KUBAKI MADARAKANI KWA MABAVU KWA KISINGIZIO CHA KULINDA CHAMA
Usiwapotoshe watanzania alichokisema Mbowe ni hiki hapa watanzania naomba m-download hotumba zima ya Mbowe na makamanda wengine Jana akiwa Mwanza.. Moderator naomba speech hii ya Mbowe iwekwe kwenye Thread ili watu walinganishe na upotoshaji unaofanywa na vibaraka wa CCM.
 
Attachments

  • File size
    9.4 MB
    Views
    65

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000
Cjaona maslahi binafsi ya mbowe ila ninachojua amegombea mara 2 tu na akashinda kikatiba kabisa! Na huu ndio muda wake wa mwisho katika uongozi.sasa nashindwa kuelewa hii sympath ya ccm inatoka wapi? Maana jk kagombea mara 2 na akashinda kwa mujibu wa katiba sasa mbona cwasikii mkimwita dictator au ana maslahi binafsi?kiukweli siwaelewi kabisa labda njooni na hoja kuntu kwa kuainisha uhalisia na c porojo za humu jamvini.
Wewe mnafiki nisome hapo juu...
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,225
waachemi CDM na Mbowe wao, CCM mnahangaika sana, mmeshinwdwa kumhonga avuruge chama, sasa mnona ni tatizo?
 
joely

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,053
2,000
Aaah zitto yeye anaposema ameanza chadema akiwa16yrs old, kwa hiyo.hata akisaliti hamna noma hamsemi
 
Dotto C. Rangimoto

Verified Member
Nov 22, 2012
1,993
2,000
Ukiangalia kwa jicho la mbali bila unafiki,kwa kweli bora tuendelee kuongozwa na ccm kuliko watu hawa,hawana lolote!!ok now mnatuambia ugomvi wa makan na mtei 1995,kipi kilichokuwepo nyuma ya pazia?masilahi binafsi,na ni hayo hayo ndio mbowe unayoyapigania,wadanganyeni watanzania wote,i will b the last kuwa na imani na uongozi wa cdm wa sasa!!shame on you mbowe!!!ni bora ufe kabisa.

acha hizo...kama wanaCHADEMA watakubali mbowe ataongoza tena,,,ingawa mimi siungi mkono kwa hilo,,,ila maamuzi ya chama hufanywa na wengi si mtu mmoja, na wengi wakiamua hivyo hakuna namna.
 
Gracious

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
1,843
2,000
Mpendwa,mimi cjui adui wa ccm ni Chadema au la!!nilichoongelea ni kwamba chadema kama taasisi ina misingi imara tu,tatizo ni uongozi.Migogoro yote iliyowahi tokea chadema imemhusisha Mbowe moja kwa moja,na mara zote yeye amekuwa akibaki salama,ckatai yawezekana kabisa yupo sahihi katika maamuzi yake kwenye hiyo migogoro.
Ila ukitizama kwa mbali ukifungua kichwa chako utaona hata anapobainisha historia yake ndani ya chama utaona kuna harufu fulani ya kuonyesha namna alivyogharamika kukifikisha chama hapo kilipo pamoja na wakina Ndesamburo!!
Na hilo limefanya kila kunapokuwepo na migogoro ni lazima yeye awe sahihi na kwa sababu usalama wako CDM unategemea jinsi gani mawazo yako yanaendana na Mbowe,then asilimia kubwa ni wa kumuunga mkono wazi wazi au wanabaki neutral kama wakina Baregu,Prof Safari na wengineo.Narudia tena sababu watanzania tumeichoka ccm na tunahitaji mabadiliko,Mwenyezi Mungu aondoe huo uongozi wa mbowe na Slaa,kwa style yeyote,ikibidi Israel awatembelee tu then hapo ndio cdm ishike dola otherwise ni kudanganyana tu,tutajuta na kusaga meno.

Mbona huwasemi wale wanajinasibu wameijenga CHADEMA na CHADEMA ina damu yao tangu miaka 16? Ukweli ni kwamba Mbowe kaitoa CHADEMA mbali sana kuliko huyo mtu wenu
 
Kada Deya

Senior Member
Nov 8, 2011
152
195
Usiwapotoshe watanzania alichokisema Mbowe ni hiki hapa watanzania naomba m-download hotumba zima ya Mbowe na makamanda wengine Jana akiwa Mwanza.. Moderator naomba speech hii ya Mbowe iwekwe kwenye Thread ili watu walinganishe na upotoshaji unaofanywa na vibaraka wa CCM.

Hiyo sehemu ya hotuba ni kwamujibu wa Magreth Makange ambaye alikuwepo eneo la tukio jana na clip yake tunayo. Nilidhani unapinga maneno hayo ya mbowe kama issue ni Hotuba nzima uko sahihi hotuba ikliyowekwa hapa ni sehemu tu ya hotuba nzima.
 
REX

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
331
195
Cjaona maslahi binafsi ya mbowe ila ninachojua amegombea mara 2 tu na akashinda kikatiba kabisa! Na huu ndio muda wake wa mwisho katika uongozi.sasa nashindwa kuelewa hii sympath ya ccm inatoka wapi? Maana jk kagombea mara 2 na akashinda kwa mujibu wa katiba sasa mbona cwasikii mkimwita dictator au ana maslahi binafsi?kiukweli siwaelewi kabisa labda njooni na hoja kuntu kwa kuainisha uhalisia na c porojo za humu jamvini.

ya wezekana na wewe umezibwa macho usione, mbowe hafai kuaminiwa hata kidogo watu kama nyie mnamfagilia ndio maana anaendeleza madudu yake, fuatilia mkasa wa chacha wangwe na hii ya zito kabwe, ukitaka kuwa salama cdm usimpinge sasa hayo ndo mabadiliko tunayoyahubiri majukwaani? Kunapokuwa na hoja zinazokizana ndipo tunajenga mbinu mpya za kuleta maendeleo kichama. mbowe ndio cha matatizo yote ndan ya chama na kama kuna mchawi wa cdm bas ni mbowe na kuliko kiipa dola chadema chin ya uongoz wa mbowe na slaa bora CCM waendelee wanaweza kuwa na uzalendo na nchi. Kama bado unatetea yanayofanyika ndan ya cdm bas na wewe una chochote unachopata huko, kama ni raia kama mim hupaswi kujibama hivyo kufikiri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom