Historia ya mapendekezo ya Katiba ya Gavana Edward Twining 1950 (Sehemu ya Kwanza)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,851
30,195
HISTORIA YA MAPENDEKEZO YA KATIBA YA GAVANA EDWARD FRANCIS TWINING 1950 (SEHEMU YA KWANZA)

Juma Mwapachu mtoto wa Hamza Mwapachu miaka mingi nyuma katika mazungumzo wakati natafiti historia ya TANU aliniambia kuwa katika vitu vyote ambavyo baba yake alikuwa akijivunia katika maisha yake ya kutafuta uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni kushiriki kwake katika kuandika katiba ya Tanganyika wito uliotolewa na Gavana Edward Francis Twining kupitia kamati aliyoiunda iliyokuwa ikijulikana kama Constitutional Development Committee.

Uzito wa maneno ya Hamza Mwapachu kwa mwanae Juma nilikuja kuufahamu baadae sana baada ya kumsoma Cranford Pratt, ‘’Critical Phase in Tanzania 1945 – 1968,’’ (1976) kwani alisifia mapendekezo yake.

Mapendekezo haya yaliandikwa na Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia wakiwa wajumbe wa TAA Political Subcommittee iliyoundwa mwaka wa 1950.

Lakini kuna kitu Juma Mwapachu alinificha na nina hakika aliogopa kuniambia kwa kuchukua tahadhari kwani miaka ile historia ya uhuru wa Tanganyika ilikuwa jambo nyeti sana.

Juma Mwapachu atakuja kulisema lile alilonificha miaka mingi baadae tena kwa kuliandika kwenye mtandao kwa dunia nzima kusoma.

In Shaa Allah nitaeleza nini alisema huko mbele ya safari.

Lakini kabla sijaondoka hapa katika haya mapendekezo aliyoyasifia Pratt nilikuja kujifunza mambo mengine mazito ndani ya waraka huo.

Huu waraka nikaukuta katika Nyaraka za Sykes wakati huo niko katikati ya utafiti wangu na Ally Sykes amenifungulia nyaraka zao zote nizipitie.

Waraka huu ulijadiliwa mwaka wa 1954 katika mkutano wa mwaka wa TAA uliounda TANU na mwaka wa 1955 Julius Nyerere alipokwenda UNO safari ya kwanza ulikuwa sehemu ya hotuba yake mbele ya Kamati ya Udhamini. Mazungumzo haya yangu na Juma Mwapachu niliyafikisha kwa Kleist Sykes mtoto wa Abdul Sykes.

(Baba zao marafiki ndugu na watoto halikadhalika na wote baba zao walikuwa rafiki wa Julius Nyerere, viongozi wa TAA, waasisi wa TANU na hawakuufaidi uhuru walioupigania kwani walikufa katika umri mdogo). Siku hii sitaisahau naikumbuka kama jana vile.

Kleist alikuwa amekuja likizo kutoka Geneva alikokuwa akifanya kazi na UNHCR na ilikuwa kawaida yetu kila anapokuja likizo tutakutana kwa mazungumzo angalau mara moja kwa yale mazungumzo ya ‘’one on one.’’

Tumekaa ukumbini kwake tunazungumza mimi nikamueleza maneno yale aliyoniambia Juma Mwapachu.

Kleist akaniambia kuwa suala la katiba ya Tanganyika kwa uongozi wa TAA lilikuwa jambo kubwa na muhimu sana na yeye akaniambia kuwa baba yake ndivyo alivyomweleza.

Hii ndiyo siku Kleist akanitajia jina la Earle Edward Seaton na kunifahamisha kuwa alikuwa rafiki wa baba yake na akanieleza kuwa baba yake alimweleza kuwa Earle Seaton ndiye aliyekua mshauri wa TAA katika mambo ya sheria na katiba.

Kleist akanieleza kuwa Earle Seaton alisaidia sana katika kutayarisha mapendendekezo yaliyowasilishwa kwa Constitutional Development Committee ya Gavana Twining.

Ushahidi wa historia hii nikaja uona kwa macho yangu baadae sana vilevile kwanza katika Nyaraka za Sykes kisha katika kitabu cha Judith Listowel, ‘’The Making of Tanganyika, ‘’ (1965) na baadae nikasoma aliyoeleza Dr. Vedasto Kyaruzi katika mswada wake ambao bado haujachapwa, ‘’The Muhaya Doctor,’’ (1961).

PICHA: Juma Mwapachu na Julius Nyerere, Kleist Sykes na Mwandishi, Dr. Vedasto Kyaruzi katika siku zake za za uzeeni na picha ya mwisho wakati wa ujana wake.

JUMA MWAPACHU NA JULIUS NYERERE.jpg

KLEIST ABDUL SYKES NA MOHAMED SAID.jpg


DR. VEDASTO KYARUZI.jpg
1627330989197.png
 
Shule halisi,endelea kutujuza kwani historia rasmi imepotishwa Kwa faida ya genge fulani.
 
Shule halisi,endelea kutujuza kwani historia rasmi imepotishwa Kwa faida ya genge fulani.

Nnangale,
Hapana haja ya lugha kali ndugu yangu.
Tusome, tujadili na tujifunze kwa pamoja na katika staha.

Ukifanya hivyo na mimi unanitia moyo wa kuisomesha historia hii ambayo huenda walioandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika hawakupata kuijua kwa kuwa hawakuwako wala hawakuhusika na harakati zile.
 
Nnangale,
Hapana haja ya lugha kali ndugu yangu.
Tusome, tujadili na tujifunze kwa pamoja na katika staha.

Ukifanya hivyo na mimi unanitia moyo wa kuisomesha historia hii ambayo huenda walioandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika hawakupata kuijua kwa kuwa hawakuwako wala hawakuhusika na harakati zile.
kaka mi niko huku Ng'wamitilwa mkoani geita kiswahili nacho shida mie nilifikiri ni lugha ya kawaida tu, kumbe lugha kali samahani sana.
 
kaka mi niko huku Ng'wamitilwa mkoani geita kiswahili nacho shida mie nilifikiri ni lugha ya kawaida tu, kumbe lugha kali samahani sana.
Nnangale,
Nimekuelewa.

Hii historia inamuhusu sana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tutake tusitake lazima tutamgusa.

Mwalimu ni kiongozi mkubwa inatakiwa tumuwekee heshima.
 
Back
Top Bottom