Historia ya Kabila la Wahaya

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
Mzungu wa kwanza kukanyaga Bukoba alikuwa ni Mjerumani Emin Pasha aliyewasili tarehe 31 Oktoba, 1890, ingawa miaka 30 kabla ya hapo Waingereza wawili, T.H. Speke na T.A Grant waliwahi kufika Karagwe na kukutana na Omukama Rumanyika l (Rugundu). Gavana wa kwanza wa kijerumani ni Julius von Soden (1891-1893) na wa mwisho ni Heinrich Schnee (1912-1916).

Gavana wa kwanza wa kiingereza ni Sir Horace Byatt (1916-1924) na wa mwisho ni Sir Richard Turnbull (1958-1961). Wahaya (wakiwemo Wanyambo) wanajulikana kama Western Interlacustrine Bantu. Walihama kutoka Uganda Magharibi katika karne za 15 na 16, hasa kutoka Bunyoro na Ankole. Koo nyingi asili yao ni Bunyoro na chache kama abamiilo/abagabo asili yao ni Ankole.

Kihanja, Ihangiro na Bukara Bakama wao ni Bahinda wakati wale wa Kiamutwara na Bugabo ni Bankango waliowaasi Bahinda na kujitangazia uhuru yapata mwaka 1820 wakati Mukama Kalemera II alipofariki. Uasi huu uliongozwa na Kitekere na baadaye kuimarishwa na mtoto wake Omukama Kaitaba (1860-1888).

Kiziba Rulers (title Omukama)
.... - .... Bike
.... - .... Kiziba Kizindo
.... - .... Ntumwa
.... - .... Kanyamaishwa
.... - .... Kibi I Nyakiiru Kaganda
.... - .... Ishamura-Njobe "elya Kiziba, elingome"
.... - .... Ishamura-Nyakabinga "elya Bunyoro"
.... - .... Wanumi
.... - .... Bwanamba
.... - .... Matwi
.... - .... Magembe I (1st time)
.... - .... Kashumba (regent?)
.... - .... Magembe I (2nd time)
.... - .... Muzinga
.... - .... Mwigara
.... - .... Burungu I
.... - .... Magembe II
.... - .... Mboneko I
.... - .... Nyarwangu
.... - .... Mulimpuzi -Regent
.... - .... Ruhangarazi I
.... - .... Nyarwangu II
.... - .... Rutajwaha
.... - .... Burungu II Kakinda
.... - .... Kibi II Rutahirwa
.... - 1870 Ruhangarazi II (d. 1870)
1870 - 1903 Mutatembwa
1898 - 1900 Rweshabura (in rebellion)
1903 - 1916 Mutahangarwa Karutasigwa
1916 - 1927 Edward George Mboneko II
1927 - 1937 William Mutakubwa
3 May 1937 - 6 Nov 1962 Nestor Lutinwa wa mwisho kusimikwa (kutendekwa)

Bakama wa Kiziba ukoo wao ni Baziba/Babiito. Baada ya kifo cha Mukama Burungu II (1800-1835) walipendelea kuitwa Abayobya. Sababu ni kwamba wanatokana na Omulangila Luyobya, mtoto wa Mukama Ruhangarazi I. Kutokana na ukatili uliopitiliza wa Burungu II, baba yake mdogo, Omulangila Luyobya, alishindwa kumvumilia na hivyo akaanzisha vita ya kumng’oa. Katika vita hii alisaidiwa sana na mtoto wake aliyeitwa Rutahilwa. Luyobya kwake kulikuwa ni Bukwali, Kanyigo.

Burungu II alijikuta katika hali ngumu ya kushambuliwa kutoka ndani na nje, kwani Bahyoza walikuwa pia wanamshambulia. Baada ya Burungu kuuawa na maadui mwaka 1835, Rutahilwa, mtoto wa Ruyobya alitawala na akapewa jina Kibi II. Baada ya Kibi II, alitawala mtoto wake Rugangarazi II (1858-1865), halafu Mutatembwa (1865-1903), aliyefuatiwa Mutahangarwa (1903-1916), kisha Mboneko II (1916-1926), halafu Mutakubwa (1926-1937), halafu Lutinwa (1937-1974).

Mutakubwa aliondolewa na wakoloni mwaka 1937 na hakuwa na mtoto. Hivyo ndugu yake Mboneko aitwaye Nestor Lutinwa alichaguliwa kumrithi, na akatawala mpaka Nyerere alipofutilia mbali utawala wa Bakama.

Sababu ya kuondolewa kwa Mutakubwa ni inadaiwa ni ufuska uliokithiri, ukiwemo ule wa kulazimisha mama yake Muchureza alijaribu kumkanya lakini hakusikia. Hivyo alikwenda kumuomba DC wa Kikoloni amsaidie kumkanya. Badala ya kumkanya DC alimfukuza, kwani kwa mzungu kubaka ni dhambi isiyosameheka. Lakini DC hakuelewa kuwa Mukama hawezi kuwa na hatia ya kumbaka mwanamke au kufanya uasherati, kwani kwa mila zetu wanawake wote ni mali ya Mukama. Hivyo watu wakawa wanamuimba Muchureza kuwa ni “kilimi nyakwelega ayagambiile omujungu ati Omukama nasiyana”. Maana yake, wimbo ulikuwa unamsuta Muchureza kwa kujichongea (okwelega) bila sababu ya msingi.

Mutakubwa, baada ya kufukuzwa, alimalizia maisha yake pale Kigarama, kwa Edward Kasano, kwani baba yake Edward alikuwa tumbo moja na Mutakubwa, wote wakiwa ni watoto wa Muchureza. Alifariki mwaka 1948 na kuzikwa pale Kigarama.

Jambo la ajabu ni kwamba wazee pale kijijini waliendelea kumpa heshima kama Mukama wakimwamkia Habuka Izoba, Habuka Rugaba, Habuka Nyakusinga, nk. Inadaiwa mtu akishasimikwa kama Mukama anakuwa na namna ya uungu (semi-divine). Hivyo ukimnyima heshima yake unaweza ukapatwa na mabaya.

7B80A181-39AA-4F0B-9ABB-8DAB071E232A.jpeg

Mavazi ya Asili ya Wahaya (Olubugo)

4B8B8304-7A87-49EA-B9F9-D7C06D83A415.jpeg

Nyumba za asili za wahaya

861CD2A6-FF5A-49D0-A46A-5D9C0A773438.jpeg
 
Nina kitabu cha historia na utamaduni wao, nitakitafuta nikuwekee dondoo, ila kuna nadharia fulani nimeisikia ikanigusa, kuhusu asili ya wahaya kuvaa kanzu na kofia kama vazi la kiutamaduni. Hii hutokea sana kwenye harusi. Nasikia ni urithi wa kikoloni.
 
Wasoga wa Uganda ,wanawasikia vizuri sana Wahaya wakiongea.Majina mengi ya Kihaya yako vilevile Uganda!eg Mujuzi etc
 
Title ya hicho kitabu ni nini? mtunzi? asenti

Kitabu kizuri cha kuanzia kujua historia ya Buhaya ni "The making of karagwe kingdom' kilichoandikwa na marehemu Israel katoke. Hiki kitabu ninacho lakini hadimu sana na nafikiri ni out of print( si unajua watanzania hatuna utamaduni wa kusoma)

Kingine, hiki nafikiri unaweza kukipata catholic bookshop ya Dar kimeandikwa na method Kilaini kama phd thesis kinaitwa kama sikosei historia ya kanisa buhaya (ninacho lakini kiko mbali kwenye maboksi sasa hivi)

Kingine nimesahau mtunzi kwa sasa(kipo kwenye maboksi yangu inabidi nifute vumbi nikitafute, hiki kina information sana kama sikosei kinaitwa ' economic history of the bahaya'.

Nimekuwa busy kidogo lakini very soon nitaanza kutandika historia ya bahaya pamoja na titles za vitabu muhimu.

naomba subira kidogo.
 
Sasa tuendelee na historia ya Wahaya.Ningependa niandike kwa kiswahili kitupu, nitajitahidi, lakini nitaanza kwa kiingereza.Ieleweke kuwa mimi sio professional historian, nina passion tu ya historia(shukrani kwa mwalimu Mutabingwa pale muhimbili primary school enzi zile aliyenipa mapenzi ya somo hili!) kwa hiyo yoyote atakayetaka kunikosoa anakaribishwa sana!!!

The coming of the Bantu speaking people

The Bahaya like many (but not all) Tanzanian tribes speak the Bantu language which is a member of the Niger-Congo language family. The reason that this language family is called Niger-Congo is because linguists have hypothesized that this language family originates around river niger – congo border.The Bahaya may have distant genetic and linguistic relationships with other Bantu speaking tribes further east of Tanzania from the wasukuma to waswahili and they were probably one section of these great migrations of Bantu speaking people during the aforementioned periods. To show how the Bahaya have distant relationship even with the coastal tribes i.e Waswahili, similarities in the words below show this sufficiently:

Oruhaya:Omuntu, Kiswahili:Mtu
Oruhaya :Okurya, Kiswahili :Kula
Oruhaya: Amaizi , Kiswahili:Maji
Oruhaya:Amaino, Kiswahili:Meno
Oruhaya:Ndetela, Kiswahili:Niletee


Historians agree that the first Bantu speaking people settled in Buhaya between the fifth and the tenth century AD. It is also generally agreed that the Bahaya settled first in Bunyoro Kitara (Present day Uganda) before continuing southwards towards Buhaya. Bunyoro -Kitara should therefore be understood as the cradle of Buhaya history, and as it would be showed later Buhaya and especially Bunyoro share many cultural traits.

Kuweza Kuelewa historia ya Buhaya( na sio buhaya tu na hata historia ya karibu makabila yote ya Uganda) inabidi kwanza tuijue angalau kidogo historia Ufalme wa Zamani wa Bunyoro-Kitara.Hii ndio maada nitakayoiongelea baadae kidogo.

Munyegere, mnakaribishwa!
 
Hiki ni kitabu, titled "Historia fupi ya utawala wa Bankango, Kyamtwala - Bukoba." Kimeandikwa na mwanahistoria Francis J. Rwegoshora.

Nimefurahi kuona na kusoma historia ya watu wa nchi yetu katika kitabu hiki, kwani maelezo yaliyomo yanahusu tawala zilizokuwepo tangia miaka ya 1700!

(c) Omulangira FJ Rwegoshora
 
Katoma,

Ahsante sana kwa kuweka kitabu hiki, mimi bado sijakisoma,kitatuongezea ujuzi wa suala hili, Ahsante sana.

Kwa wale wanaouliza, reference nilizotumia/ninazotumia ni hizi.

1) The making of karagwe kingdom( by marehemu Israel katoke)
2) Economic revolutions in Bahaya history( By CM Tibazarwa)
3) Historia ya kanisa katoliki bukoba- Kagera ( By Method Kilaini)

Pamoja na mahojiano na wazee/ wafalme wa Buhaya.Hasa mkama wa Kianja.

Haya sasa ngoja niendelee kuanika historia.
 
Waitu nimekuwa kimya kidogo kutokana na shughuri za hapa na pale naomba mnisamehe.


Sasa nitaongelea Bunyoro Kitara.

Kama nilivyoeleza mwanzoni, kuna ushadi wa kutosha kuwa wahaya, walikuja kagera kutoka kaskazini /magharibi ya a frika wakipitia Bunyoro Kitara, uganda.Vilevile, walipofika Bunyoro walikaa kidogo wakatengeneza crucible au chungu cha mapishi b ambacho kina define wahaya mpaka leo.

Sasa tuangalie how was Bunyoro kitara formed?

Bunyoro kitara was an ancient kingdom which is now located in the Northwest of Uganda. The rulers of this once mighty kingdom were known as the Bachwezi and at its peak it is said to have extended up to Tabora in Tanzania..Inasemekana hawa wachwezi walikuwa kama miungu watu na walikuwa watu wenye busara sana kama miungu vile!. From the migrations of the Bantus during the fifth century to the fourteen century, Buhaya was mostly ruled by local clans. ( I will speak about Buhaya local clans later) According to oral traditions, the demise Bunyoro kitara kingdom brought about the bahinda/babito invasion of Buhaya resulting in the conquest of the Buhaya original clans.

Nihaongelea baadae kuhusu bahinda/babito.

Sasa wazee wa Buhaya na wanahistoria hawajui kwa uhakika mambo mengi kuhusu Bunyoro kitara.Katika mashairi ya kale ya Buhaya, wachwezi wanasemwa sana lakini hakuna mtu aliyeisha hakikisha kisayansi kuwa hawa watu walikuwa wa aina gani. Lakini kuna ushahidi wa ki archeology unaohakikisha kua hawa watu walikuwepo kweli, na inawezekana kabisa kuwa wachwezi ndio wabantu wa kwanza maeneo ya great lakes, wapo watu wengine wanaowausisha wachwezi na watusi au wafugaji wa Buhaya wa leo hii. Lakini hii kubuni tu, hamna mtu mwenye uhakika.

Nitaendelea na Bunyoro kitara...

Sasa kabla ya kuja kwa watawala kutoka Bunyoro Kitara sio kwamba Buhaya ilikuwa tupu haina watu na watawala.Buhaya ilikuwa na koo, ambazo mpaka sasa bado zipo.Kila koo (Oruganda) ilikuwa na mkuu wa ukoo(o'mkulu wo'Oruganda) ambaye alikuwa kama mfalme/ mzee wa hekima wa ukoo.Huyu alikuwa kama Supreme Judge,yaani tatizo la mwisho yeye ndiye aliyekuwa mtatuaji.Kuna baadhi za koo zilikuwa na nguvu au influence kuliko nyingine, lakini cha muhimu hapa ni kwamba hizi koo ziliongea lugha zinazoelewana, yaani lugha zinazofanana na kihaya cha sasa.Hizi koo zilikuwa hazijaungana, yaani zilikuwa zimetapakaa ingawa zilishirikiana kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ndoa.Kwa kuwa wahaya hawawezi kuoka katika koo zao wenyewe, yaani kwa mfano kama mtu anatoka ukoo wa abarwani hawezi kumuoa mnyarwani mwenzake inabidi atafute msichana anayetoka kwenye koo nyingine mfano Omuzigaba n.k

Mwenendo huu wa ndoa ulisaidia kuongeza na kuunganisha jamii ya wahaya na ndio maana mpaka leo unakuta koo zilizoko buhaya unazikuta mpaka rwanda na hata Kongo!!

Sasa ni mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu Buhaya kabla ya karne ya 14(yaani wakati wa koo hizi) lakini muda hauniruhusu kusema hayo yote, nimeruka kidogo topic labda sasa niendelee kidogo na utawala wa wachwezi.

PS:ieleweke kwamba enzi zile kulikuwa hakuna mipaka ya nchi kama iliyopo sasa hivi.Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa majority ya watu wa Rwanda, Burundi, Uganda na hata mashariki ya Kongo walikuwa wanaelewana kabisa kilugha na kimila na ndio maana mpaka sasa hivi mhaya na mnyankole/mnyoro na mpaka munyamurenge wanaelewana ingawa wakati mwingine kwa maneno machache.

Sasa nitaendelea.

Hivi leo ukienda kwenye ekikale au ikulu ya mkama wa kianja Peter Nyarubamba(pale kanazi) , atakuonyesha jinsi dini ya kale ya buhaya ilivyo.Hii dini bado ipo mpaka leo na Nyarubamba ndio mrithi au high priest wadini yetu hii ambayo ilishambuliwa sana na wakoloni ingawa tenents zake ni very aunthentic and spiritual.

Sasa Mukama Nyarubamba kazi yake ni kufanya rituals fulani wakati fulani wa kuonekana kwa mwezi.(sasa unaona similarities na waisilamu ambao wanasherekea sikukuu zao kutokana na kuonekana kwa wakati fulani kwa mwezi-ingawa la hasha wahaya hawakucopy kutoka wa waisilamu ).

Katika sala zake, Mukama, hasahau kuwaomba wahenga hasa Ruhinda mwanzilishi wa koo ya kifalme ya abahinda( ukoo anaotoka mfalme) ambayo ilitawala sehemu kubwa Buhaya. Je huko Bunyoro wahinda waliingiaje kabla ya kutawala buhaya?
 
ni vyema ukawa unaaweka na attachment, ya uanchoandika ili mtu akipenda ana download the entire story with each update
 
HISTORIA YA KIOBYA KYA MIHIGO
Daudi Brett

UTANGULIZI:-

Katika ukoo mzima wa Abarwani nimeamua kuandika historia ya mtu mmoja tu KIOBYA kutokana na umuhimu aliokuwa nao katika uzao mzima wa Mugarula. Hadhi yake ilijengwa na nafasi aliyokuwanayo wakati wa utawala wa Omukama Kahigi II na Omukama kalemera III wa kihanja, nafasi ambayo aliitumia kuuweka ukoo wa Abarwani juu hakuitumia kwa faida yake na familia yake binafsi ndio maana nimesukumwa na dhamira yake nzuri kuandika historia yake.

MAISHA YA KIOBYA

Kiobya Baitwa ni mtoto kati ya watoto 17 wa Mihigo inakisiwa alizaliwa kati ya mwaka 1847 na 1850 alizaliwa katika kitongoji cha Busiko kijiji cha Ruhanga Kamachumu Kianja. Ukoo wake ni wa Abarwani kutoka katika kijiji cha Katembe na Mulongo huko Bugabo. Mama yake aliitwa Kyelesile wa ukoo wa Basimba kutoka katika kijiji cha Busingo Kamachumu Kihanja.

Babu yake aliitwa Kaweshela alihama toka kijiji cha Kizilu Kibale Bugabo pamoja na ndugu zake sita, walihamia Kihanja kutafuta makao mapya walipata ardhi Ruhanga wakalima mashamba Busiko.Baada ya kifo cha Kaweshela shamba lake alipewa jamaa yake aliyeitwa Kikoito na Kikoito alipohama akapewa Jeremia Njaza, sasa anakaa Rooza Mukabaihukya wote ni wa ukoo wa Abarwani.

Kaweshela alipokufa aliacha watoto 14 kabuli lake halijulikani lilipo Mihigo alipokufa aliacha watoto kumi na saba wafuatao:- Kiobya, Itimaa, Kobalyenda na Ntambara Watoto hawa wanne mama yao ni mmoja haijulikani nani wa kwanza kuzaliwa na nani wa mwisho.Tegambwage, Matunu na Kuzara hawa watatu nao mama yao ni mmoja haijulikani wa kwanza nani na wa mwisho nani.Baitira na Kabakenga inaaminika nao mama yao ni mmoja. Watoto waliobaki kila mmoja alikuwa na mama yake wajukuu zake wakubwa kwa umri walikuwa Bajumuzi na Kakana.Mihigo alipokufa alizikwa katika shamba analokaa sasa mwanae Matunu. Matunu hakuwa mrithi wake mrithi alikuwa Ntambara.

Kiobya hakujua kusoma wala kuandika elimu hiyo ilionekana kama elimu ya kigeni iliyoletwa na wazungu ingawa alipenda watoto wake waipate hivyo aliwapeleka watoto wake wote wa kiume shule zama hizo mtoto wa kike alikuwa hafikiriwi kwa lolote la maendeleo hakuna mtoto wake wa kike hata mmoja aliyepelekwa shule.

Kiobya hakuwa mfuasi wa dhehebu lolote la dini kwa maana nyingine hakuwa na dini hata hivyo hakuwazuia watoto wake wa kike na kiume kuwa wafuasi wa dhehebu lolote la dini wapendalo pia sikumbuki kuwepo kwa yeyote miongoni mwa wake zake aliyekuwa mfuasi wa dini yoyote.

Upande wa michezo Kiobya alikuwa mpenzi mkubwa sana wa mchezo wa BAO (Olwesho) wachezaji wenzake wakubwa wakati akiwa Kanazi alikuwa Kataikile Bwohe na Shedrack Kikaibi na alipokuwa Kyanguge alikuwa Rwakitanga Kasigwa na walikuwepo wachezaji wengine wa siku moja moja, bao alilolitumia bado lipo huko Kyanguge hadi sasa.
KUHAMIA KANAZI

Mnamo mwaka 1895 Omukama Kahigi wa II wa Kihanja alihamisha kikale chake toka Bulembo kihanja kwenda kanazi ili aweze kuitawala vizuri sehemu ya nchi aliyomegewa na utawala wa Wadachi toka katika utawala wa Kyamtwara na Bukara Maruku. Miongoni mwa watu aliohama nao ni Kiobya walipokuwa Kanazi alipewa shamba lenye ukubwa wa ekari kumi, baadae akapewa shamba jingine Kyanguge lenye ukubwa wa ekari kumi na mbili na akaifanya Kyanguge kuwa makao yake makuu.

Shamba hili la Kyanguge lilikuwa la Kailembo Byanjweli.Kailembo alihama na kuliacha shamba hili akaamua kurudi kyamtwara alikotoka kwa sababu hakupenda kutawaliwa na Omukama Kahigi. Kailembo Byanjweli alikuwa Omukungu (mtawala wa Kijiji) alifuatana na Omukama Mkotani wa Kyamtwara kwenda Karagwe na baadae Buganda (Uganda) huko ndiko alikokwenda kuomba hifadhi. Kailembo Byanjweli, Kiobya na Mashaija wa Kabale waote ni ukoo mmoja, Kiobya zaidi ya kupewa shamba alipewa Obukungu badala ya Kailembo.

Mnamo mwaka 1897 alipewa shamba jingine Bugera Kanyangereko lenye ukubwa wa ekari 20 na wakati wa utawala wa Omukama Kalemera alipewa shamba jingine la Kasomoro Kanazi lenye ukubwa wa ekari 25. Shamba lake la urithi la Busiko Ruhanga alimpa mwanae Mustafa Nyangasha.Katika kila shamba alilima kilimo cha mazao mchanganyiko kama migomba, mibuni, nk. Ndani ya kila shamba alifuga Ngombe na wakati wote walikuwepo sio chini ya Ngombe wanane waliokuwa wakikamuliwa maziwa, katika shamba la kanazi alijenga nyumba za kisasa zilizojengwa kwa kutumia matofali ya kuchoma, mawe, ziliezekwa kwa bati na zilipigwa rangi kwa kutumia chokaa, pia alifanya hivyo hivyo kwenye shamba la Kyanguge.

KUWA NAIBU (REGENT) WA OMUKAMA
KAHIGI II
Mnamo mwaka 1908 Omukama Ntare VII wa Karagwe aliondolewa madarakani na Wadachi, nchi yake ikawekwa chini ya himaya ya Omukama Kahigi ailinde. Omukama Kahigi II alimteua Kiobya kya Mihigo kwenda kuitawala Karagwe kwa niaba yake. Katika kitabu kiitwacho Tanganyika under German Rule 1905-1912 kilichoandikwa na John IIiffe uk 173 imeandikwa hivi some what later the Germans abandoned their attempt to prop up the ruling house of Karagwe,weakened by succession of child Rulers and natural disaster and installed Kahigis brother in-law KIOBYA as Regent.

Katika kitabu cha historia ya wilaya ya Bukoba kilichoandikwa na Hans Cory ukurasa 126 anasema Ntare alipopata makamo mnamo mwaka 1908 mara moja akaonyesha tabia zilezile za Babu zake Wadachi wakamuondoa Karagwe ikawekwa chini ya utawala wa Kahigi Mukama wa Kihanja ambaye wakati huo alikuwa rafiki na akipendwa sana na Wadachi. Kahigi akamchagua Kiobya Shemeji yake aitawale Karagwe kwa niaba yake.

Omukama Ntare kwanza aliachwa akae Karagwe lakini baadae aliondolewa akapelekwa Kanazi makao makuu ya Omukama Kahigi baada ya vita kuu ya Dunia ya kwanza kutokea alijaribu kuandikiana na waingereza wa Uganda akashitakiwa na Kahigi na Kiobya akanyongwa na Wadachi kwa uasi.Kiobya akaendelea kuitawala karagwe.

Ijapokuwa Kiobya alijitahidi kuitawala Karagwe vizuri yeye kwa kuwa alikuwa mgeni alichukiwa zaidi kuliko watawala wabovu na katili wa jamaa ya haki ya utawala waliomtangulia. Mnamo mwaka 1916 ikawa lazima aondolwe na Daudi Rumanyika mtoto wa Omukama Ntare akapewa mamlaka ya kuitawala karagwe chini ya ulinzi wa Isaac huyu alikuwa Mganda kwa kuwa Daudi alikuwa ni mtoto mdogo wa umri wa miaka 11 na wakati huohuo akapelekwa Uganda kuelimishwa.

Omukama Kahigi II alikufa tarehe 4-9-1916 wakati wa Kifo chake Kiobya alikuwa bado Karagwe alitumiwa ujumbe kumwarifu juu ya kifo cha Omukama akaondoka Karagwe kurudi Kihanja kuhani msiba na tangia hapo hakurudi tena Karagwe. Aliwatuma wanae Mustafa Nyangasha, Ab-Bakari Munema na Anatori Balimunsi kuchukua mali zake na jamaa zake aliokuwa amewaacha huko na utawala wa Wadachi Ukamtawaza rasmi Daudi Rumanyika Kuwa Omukama wa Karagwe.


KILIMO CHA KAHAWA
KARAGWE

Kiobya alikaa Karagwe tangu mwaka 1908 hadi mwaka 1916 makao yake makuu aliyaweka Kishao Bugene, kile kikale cha Omukama Ntare kilikuwa Nyakahanga. Katika utawala wake alipokuwa Karagwe aliwahimiza na kuwasimamia Banyambo kulima kilimo cha Mibuni na Pilipili ili kujiletea maendeleo kwa kuwa kwa wakati huo ndio yalikuwa mazao makuu ya biashara, hadi wakati huu kahawa ilikuwa haijaanza kuvunwa kwa wingi Karagwe, ilikuwepo mibuni michache tu na kwa watu wachache kahawa iliyovunwa ilipikwa na kukaushwa kwa moshi kwa matumizi ya kutafuna tu.

Ili kuonyesha mfano na kuleta mapinduzi katika matumizi ya zao la kahawa Kiobya mwenyewe alilima na kupanda mibuni mingi sana katika shamba lake la Bugene, Banyambo nao wakashawishika wakaanza kupanda mibuni mingi katika mashamba yao. Shamba na nyumba yake ya Bugene vilidumu hadi miaka ya 1960. Mnamo mwaka 1950 vyama vya ushika vya msingi vya ununuzi wa zao la kahawa vilipoanzishwa katika wilaya ya Bukoba nyumba yake ya Bugene ndiyo iliyofanywa ofisi ya kwanza ya chama cha ushirika wa ununuzi wa zao la kahawa (Bugene Native Farmers Co-operative Society Ltd).

Profesa Israel Katoke kwa ajili ya chuki zake za kikabila za Banyambo kwa Kiobya zilizojengwa kwa kuwatawala akiwa mgeni katika kitabu chake cha The Making of Karagwe Kingdom ameandika matusi mengi sana dhidi ya Kiobya lakini hata hivyo historia itabaki palepale kwamba Banyambo maendeleo waliyonayo sasa Karagwe yanatokana na zao la kahawa ambalo Kiobya alihimiza na kusimamia kupandwa kama sio hivyo maendeleo waliyonayo leo wasingekuwa nayo kwa hilo Banyambo wanapaswa kumshukuru na kumkumbuka Kiobya.


SAFARI ZAKE ZA KUTOKA KIHANJA
KWENDA KARAGWE
Katika safari zake zote za kutoka Kanazi Kihanja kwenda Karagwe na kutoka Karagwe kurudi Kihanja zilikuwa ni za kutembea kwa miguu, njia yake kuu aliyopita mara nyingi ilikuwa ni kutoka Kanazi >Ibwera>Nyakigando>Kabirizi>Ndama Lushanje hapa ni mpakani mwa Kihanja na Karagwe anaingia Kikula anafika Bugene. Enzi hizo sehemu kubwa ya njia hii yalikuwa ni mapori yenye aina mbalimbli ya wanyama Simba, Chui, Faru, Tembo, Twiga na wanyama wengineo walikuwa wakipatikana kwenye misitu hiyo.
Msafara wake wakati wa safari zake ulikuwa haupungui chini ya watu 40 na safari ya kwenda au kurudi ilikuwa inachukua kati ya siku tatu hadi nne, wakati wa safari zake Kiobya hakupenda kuipa nchi yake ya Kihanja kisogo hivyo katika safari zake za kutoka kihanja kwenda Karagwe alikaa kwenye machela akitazama alikotokea yaani akiiangalia Kihanja zama hizo wakuu katika utawala katika safari zao walibebwa juu ya machela.

KIOBYA NA UTAWALA WA
OMKUKAMA KALEMERA
Kama tulivyokwishaona huko juu baada ya kifo cha Omukama Kahigi mwanae Benjamin Mtembei ndiye aliyepaswa kurithi kiti cha Baba yake wakati huo alikuwa ni mtoto mdogo wa umri wa miaka 8 wazee wa ukoo wa Omukama walio wengi hawakupendezwa na mtoto mdogo wa umri kama huo kutawala wakaona ni vyema wamtawaze mtoto mkubwa serikali ikawaunga mkono miongoni mwa watoto wakubwa wa Omukama Kahigi akachaguliwa Alfred Rutabingwa kushika mamlaka akatawazwa akaitwa Omukama Kalemera III.

Mama wa Omukama Kalemera aliitwa Kabalyenda ambaye alikuwa ni dada yake Kiobya kwa kutawazwa mwanae yeye akawa Omukama Omukulu akaitwa Kabibi (Mpanzi), kabalyenda alifariki mwaka 1927alifia Ntungamo Muhutwe baada ya kifo chake mtoto wake Kiobya aliyeitwa Evangelina Kiiza akaitwa jina lilelile la Kabibi.

Kiobya katika tawala zote mbili Utawala wa Omukama Kahigi na Utawala wa Omukama Kalemera alikuwa katika baraza la wazee wa kumshauri Omukama ni wakati wa utawala wa Omukama Kalemera Kiobya alijipatia majina ya tambo na majigambo ya "Rwakaijanangoma", "Rwakaijanante" na "Ituro lya Rumambo"

Abahinda watu wa ukoo wa utawala walimwamkia Kiobya "shumalaamu zama hizo ilikuwa ni mwiko kabisa kwa Muhinda (ukoo wa Omukama) kumwamkia Mwiru (koo za watawaliwa). Kwa upande wa Omukama binafsi Kiobya licha ya kuwa mtawaliwa alikuwa hamwamkii Omukama (kumulamya) kama ilivyokuwa ikifanywa na watawaliwa wengine isipokuwa yeye wakati wa kwenda kumwamkia alimpa chochote ambacho angekuwa ameshika mkononi kati ya Fimbo, Muhoro au Mkuki na Omukama alikigusa kitu hicho kama ishara ya kukubali salamu hiyo. Kwa mujibu wa mila Omukama hamwamkii mtu yeyote isipokuwa mama yake mzazi tu.

KIFO CHAKE
"Narudi Kyanguge lakini sijui kama nitakuja Kanazi tena."Haya ni maneno aliyoyatamka Kiobya wakati akiwaaga ndugu, jamaa na marafiki zake wa kanazi wakati akitoka huko kurudi nyumbani kwake Kyanguge. Kanazi palikuwa mahali pa "Ikulatiro" alikaa kwa muda tu alipokwenda kumtembelea Omukama au kama Omukama alimuhitaji. Hakuwa na mke yoyote aliyekaa kanazi isipokuwa alikuwa akienda na baadhi ya wake zake ambao waliungana na wake wenzao ambao walikuwa wanakaa Kanazi Kasomoro.

Wakati akitoka Kanazi Kurudi Kyanguge akikaribia kufika katika uga wa nyumba yake alikuwa akipiga risasi moja hewani ishara ya kuwaarifu ndugu, jamaa na marafiki zake kwamba alikuwa amerudi nyumbani kutoka kanazi, na huku nyumbani nako alijibiwa kwa kupigwa ngoma yake iliyoitwa "katonda" aliyekuwa akipiga ngoma hii alikuwa anaitwa Kasamitara Kyangura wakati anapiga ngoma hii alikuwa anatamka maneno yafuatayo "Ekiita ni Katonda" na waliobaki wanabwagiza "Omukama ni Rugaju" baada ya hapo ilipigwa panda aliyekuwa akipiga panda alikuwa anaitwa Banyeza baba yake Simioni Myaka.

Baada ya siku mbili tangu atoke Kanazi aliugua na siku ya tatu kama alivyojitabiria mwenyewe akafariki dunia ilikuwa tarehe 18-1-1935 majira ya kama saa sita hivi usiku. Mtu muhimu katika ukoo wa Abarwani akawa ameiaga dunia akiwa amezungukwa na ndugu jamaa na marafiki zake. Waliokuwemo ndani ya chumba chake wakati huo ni wake zake Mukasheruzi, Nagayo, Mukafumu, Nagayo Anna, Tibyakushemera, Mukabahaya na Tibashemelelwa. Nduguye aliyekuwepo ni Omwani Nyamaishwa pia walikuwemo wanae Mustafa Nyangasha,Coroneli Bushongore na Willbard Kwelengera katika chumba jirani walikuwemo wanae Tryphone Samson, Daud Brett, Ferdinand silingi, Esteria Mukatesi, Nyangoma, Mathias Balingilaki na Feliciani Binamungu, sebuleni huko kulijaa watu wengi sana. ambao siwezi hata kuwakumbuka.

Manamo tarehe 20-1-1935 majira ya saa 10 jioni Kiobya akazikwa katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba katika moja ya vyumba vya nyumba yake ya Kyanguge japo ametutoka jina lake limebaki na litaendelea kuwepo kwa vizazi na vizazi. Mungu amrehemu amfutie madhambi yake na ampuzishe kwa amani AMIN.

URITIHI
Mnamo tarehe 21.1.1935 siku moja baada ya mazishi ya Kiobya Omukama Kalemera alituma ujumbe Kyanguge kwa ukoo wa Ambarwani kuwaomba waahirishe zoezi la kumrithisha mtoto atakaye chukua kiti chake mpaka hapo baadaye, kwa mila na desturi za Bahaya siku mbili baada ya mazishi ya marehemu mtoto atakayemrithi na kuwa kiongozi wa familia hukalia kiti cha marehemu.

Kufuatia ombi la Omukama Kalemera utaratibu wa kumsimika kwenye kiti mrithi wa Kiobya ulisimamishwa na aliyepasawa kumrithi alikuwa ni mwanae Koroneli Bushongore na dada yake katika urithi alipaswa kuwa Esteria Mukatesi maana hao ndio walioosha mwili wa marehemu "kugabura".

Baada ya wiki mbili Omukama Kalemera alituma ujumbe wa pili Kyanguge kwa ukoo wa Abarwani ukiwa na pendekezo la Omukama la kuwaomba kumsimika Petro Tibaijuka kuwa mrithi wa kiobya badala ya Koroneli Bushongero. Barwani waliridhia haja ya Omukama zoezi la urithi lililokuwa limesimama likaendelea Petro Tibaijuka akasimikwa kwenye kiti akawa mritihi kiongozi wa familia na dada yake katika urithi akawa Nyangoma.

Petro Tibaijuka alikuwa anafanya kazi Mwanza alifika Kyanguge siku tano baada ya mazishi ya baba yake.Watoto wa kiume ambao hawakuwa na mashamba walilirithishwa mashamba, na kila mtoto wa kiume alipewa "Batwarwa wa Nyarubanja" kulingana na uwiano wa umri wa kuzaliwa walipewa fedha na ng'ombe kwa kufuata uwiano huohuo. Watoto wote wa kike kila mmoja aliwekwa chini ya uangalizi wa mtoto wa kiume wa kumlinda kwa mila za Bahaya watoto wa kike hawawezi kurithi mashamba. Baada ya miezi sita Banyaruganda walivunja Matanga na kusambaa kuendelea na maisha ya kawaida (kushohora)

Sababu za Omukama Kalemera kumpedekeza Petro Tibaijuka kuwa mrithi wa kiobya ni kwa kuwa alikuwa msomi akijua kiingereza vizuri na akifanya kazi bomani Mwanza kama karani mkuu chini ya District Officer (D.C) sifa ambazo Omukama aliziona zina manufaa katika utawala wake kwa kuwa zilikuwa zinaendana na wakati.

UZAO WA KIOBYA
Inaaminika Kiobya alizaa watoto zaidi ya mia moja na alioa wanawake wengi kwa idadi kama hiyo au pungufu kidogo ya mia moja, hapa chini ni orodha ya wanae ambao wakati anakufa walikuwa hai pamoja na mama zao.
1. Ab- Bakari Munema
2. Anatoli Balimunsi
3. Alphonce Ndyakohasi
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Banyangoi wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Bwigula Kihanja.

1. Koloneri Bushongore
2. Tereza Mukaite
3. Willbard Kwelengera
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Bagane wa ukoo wa Abayego mzaliwa wa katoke Kihanja.

1. Paskazia Mukabengesi
2. Daudi Brett kilyekaija
3. Esteria Mukatesi
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Anna Nagayo Bagoka wa ukoo wa Abende mzaliwa wa Bugene Karagwe.

1. Joseph Kandabila
2. Fulgence Tibamanywa
3. Feliciani Binamungu
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Tibyakushemera wa ukoo wa Abayango mzaliwa wa Ihembe Karagwe.

1. Amina Amulungi
2. Fideli Katto
3. Tadeo Rwiza
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Mukomutanda wa ukoo wa Abende wa Bugene Karagwe.
1. Stephano Bashaija
2. Angerbert Ambele
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Bagelize wa ukoo wa Abahuga mzaliwa wa Rwayango Mabira Karagwe.

1. Paulo Katabaro
2. Ferdinand Silingi
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Mukafumu wa ukoo wa Abayozi mzaliwa wa Itoju Kihanja.

1. Shuzali Ngaiza
2. Gervazi Babili
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Kalungi Kahigi wa Ukoo wa Bahinda

1. Mustafa Nyangasha
2. Malifedha Kyabago
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Kagulila

1. Raphael kiboga
2. Jeremid Lukomwa
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Tereza wa ukoo wa Abasingo

Tryphone Samson: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mukasheruzi wa
ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Karagwe.

Amisa Kwezi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Lyagwage mzaliwa wa Karagwe

Domitina Tikyakweba: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kemisingo wa ukoo wa Abashasha mzaliwa wa karagwe.

Paskazia Mukalangira: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mukabahaya wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Karagwe.

Maria Kasoli: mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kyetoba Rwiza wa ukoo wa Abashozi mzaliwa wa Kigarama Rwagati Kihanja.

Hamisi Babu: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kyantumile wa ukoo wa Abanyuma mzaliwa wa Maruku Bukara.

Yohana Maria Mapenzi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kitundila wa ukoo wa Abagaya mzaliwa wa Kyanjoju Kihanja.

Nyangoma: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kansiga mzaliwa wa Karagwe.

Petro Tibaijuka: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Tinkunilwa wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Mugaza Kyanguge Kihanja.

Paulina Kabalebe: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Nkubuye mzaliwa wa Rwanda.

Ameria Kamashsmba: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mpongwa mzaliwa wa mabira Karagwe.

Martina Tibela: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kaigane wa ukoo wa Abasaizi mzaliwa wa Karagwe.

Evanjelina Kiiza: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Rooza Nyanjala wa ukoo wa Abamiila mzaliwa wa Ankole Rukiga Uganda.

Kashumuni: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Tindyebwa wa ukoo wa Ababango mzaliwa wa Kyanguge Kihanja.

Zelida Mukajuna: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Suzana Kyobendaga wa ukoo wa Abamiilo mzaliwa wa Rukinga Ankole Uganda.

Mathias Balingilaki: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Bashemere wa Ukoo wa Abasaizi mzaliwa wa Ankole Uganda

Fredrick Kabinyagira: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Nzine mzaliwa wa Karagwe.

Anastazia Tibikinena: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abaihuzi wa Bugera Kanyangereko.

Asmini Bikale: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abaihuzi wa Bugera Kanyangereko.

Shella Kinuzile: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abayango mzaliwa wa Rwazi Kanyangereko.

Tereza Mukagilage: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......mzaliwa wa Karagwe.

Mathayo Mushongi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......mzaliwa wa Karagwe.

Mikaili Katabazi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa Ukoo wa Abazigu mzaliwa wa Karagwe.

Watoto wa Kiobya Rooza Kemilembe na Zainabu Twahilwa sina kumbukubu za wasifu wa Mama zao.
Hadi Kiobya anachukuliwa na umauti aliacha watoto hai 49 ambao nilikuwa ninawafahamu na aliacha wake hai niliokuwa ninawafahamu 40 kati ya wanawake hao arobaini aliokuwa bado anaishi nao ndani ya nyumba yake ni wake nane tu kati ya hawa wake 8 wawili kati yao hakujaaliwa kupata nao watoto, wake hawa wawili ambao hakuzaa nao ni Nagayo Bwikiza na Tibashemerelwa.Wake ambao alikuwa haishi nao ama alikuwa amewaacha au walikuwa wanaishi na watoto wao baada ya "kugungwa" kutoendelea kushirikiana nao kama wake kwa muda mrefu sana.
Mke wa kwanza wa Kiobya kuoa (Kwebohora au Kwoga) alikuwa anaitwa Nobileki ambaye alizaa nae mtoto mmoja tu aliyeitwa Laurent Byakugira mtoto huyu alikufa miezi michache kabla ya kifo cha baba yake alikufa bila kuzaa (Buchweke) pia binti wa kwanza wa kiobya Kyenchwere nae alikufa bila kuzaa (Bugumba).Kati ya wake zake aliyekufa wa Mwisho ni Anna Nagayo Bagoka alikufa tarehe 19 December 1985. Watoto walioko hai hadi ninapoandika kitabu hiki ni kumi na nne tu ambao ni hawa wafuatao:-
1. Willbard Kwerengera
2. Stephano Bashaija
3. Angelbert Ambele
4. Thadeo Rwiza
5. Amina Amulungi
6. Paskazia Mukabengesi
7. Yohanamaria Mapenzi
8. Rooza Milembe
9. Zainabu Twahilwa
10. Anastazia Tibikinena
11. Domitina Tikyakweba
12. Shuzari Ngaiza
13. Feliciani Binamungu
14. Daudi Brett.
(Ninapochapisha kitabu hiki mwaka 2009 kati ya watoto hao kumi na nne wa kiobya wamebaki watoto wawili tu Shuzari Ngaiza na Paskazia Mukabengesi mungu aendelee kuwapa uhai -Mukhsin Kiobya)[/h]
 
hongera sana kuwa mwandishi wa kitabu wewe ndo unayehitaji ka hapa tanzania
tumechoka na magazeti ya udaku bora watz waanze kufunguka macho na kusoma
historia ya makabila yao endelea na utunzi na ufike mbali kama akina
ngungi wa thiongo
Kitabu kizuri cha kuanzia kujua historia ya Buhaya ni "The making of karagwe kingdom' kilichoandikwa na marehemu Israel katoke. Hiki kitabu ninacho lakini hadimu sana na nafikiri ni out of print( si unajua watanzania hatuna utamaduni wa kusoma)

Kingine, hiki nafikiri unaweza kukipata catholic bookshop ya Dar kimeandikwa na method Kilaini kama phd thesis kinaitwa kama sikosei historia ya kanisa buhaya (ninacho lakini kiko mbali kwenye maboksi sasa hivi)

Kingine nimesahau mtunzi kwa sasa(kipo kwenye maboksi yangu inabidi nifute vumbi nikitafute, hiki kina information sana kama sikosei kinaitwa ' economic history of the bahaya'.

Nimekuwa busy kidogo lakini very soon nitaanza kutandika historia ya bahaya pamoja na titles za vitabu muhimu.

naomba subira kidogo.
 
hongera sana kuwa mwandishi wa kitabu wewe ndo unayehitaji ka hapa tanzania
tumechoka na magazeti ya udaku bora watz waanze kufunguka macho na kusoma
historia ya makabila yao endelea na utunzi na ufike mbali kama akina
ngungi wa thiongo

Kweli dada Waandishi wa historia wanahitajika sana.
 
Ntare alikuwa katili vp rubabi umesimulia utawala wa kihanja tu au kwasababu nikwenu vp kyamutwara bugabo maruku kiziba misenyi ihangilo.
 
Wasoga wa Uganda ,wanawasikia vizuri sana Wahaya wakiongea.Majina mengi ya Kihaya yako vilevile Uganda!eg Mujuzi etc

sio kweli wale watu nimewahi kuishi nao ila,mhaya huwez kuwaelewa,bora hata wanyankole na wachiga na watolo!!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom