Historia ya maisha ya siasa ya Freeman Mbowe na mafanikio yake ndani ya CHADEMA

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
FREEMAN AIKAEL MBOWE na CHADEMA

Kwa Hisani ya Martin MM

Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14.09.1961 katika wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro.

Freeman Aikaeli Mbowe alisoma elimu ya msingi katika shule ya Msingi Lambo na kufanikiwa kufaulu kwenda shule ya Sekondari Kibaha mkoa wa Pwani.

Alipohitimu kidato cha 4 Kibaha Sekondari, alifanikiwa kujiunga na kidato cha 5 IHUNGO Sekondari Manispaa ya Bukoba. Baadae alielekea nchini Uingereza kwa masomo zaidi. Uingereza alisoma programu inaitwa PPE (Politics, Philosophy, and Economics).

Ni programu ambayo ilianzishwa na Uingereza kwa ajili ya watumishi serikalini. Baadaye nchi nyingine kama US na RSA zimeshaanzisha programu hiyo. Kwa UK inatolewa kama first degree tu. Mbowe akamalizia MBA in Leadership & Sustainability kutoka Chuo Kikuu cha Cumbria, UK.

Freeman Mbowe ni miongoni mwa Watu waliofanya kazi katika Bank kuu ya Tanzania kama Afisa wa Bank Kuu (BoT) huko ndipo alipofifanikiwa kukutana na Mzee Edwin Mtei, Mzee Bob Makani.

Katika harakati za kisiasa, Freeman Aikael Mbowe aliingia rasmi katika siasa mwaka 1992.

Freeman Aikaeli Mbowe ni miongoni wa WAASISI au waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chama ambacho kilisajiliwa usajili wa kudumu mwaka 1993 kwa namba 0000003 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 katika dawati la msajili

Freeman Aikaeli Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya vijana ya CHADEMA chini ya uenyekiti wa Edwin Mtei. Waasisi wengine wa CHADEMA kutaja majina yao kwa uchache ni Pamoja na;Freeman Aikaeli Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya vijana ya CHADEMA chini ya uenyekiti wa Edwin Mtei. Waasisi wengine wa CHADEMA kutaja majina yao kwa uchache ni Pamoja na;

1. EDWINI MTEI - ARUSHA

2. BOB MAKANI - SHINYANGA

3. FREEMAN MBOWE - KILIMANJARO

4. BROWN NGWILUPIPI - IRINGA

5. EDWARD BARONGO - KAGERA

6. WASIRA-MARA

7. MENRAD MTUNGI - KAGERA

8. MARRY KABIGI - MBEYA

9. EVARIST MAEMBE - MOROGORO

10. COSTA SHIGANYA - KIGOMA

Wakati wa kusaka wanachama wa CHADEMA ili kupata usajili wa muda (Provisional registration) kwa mujibu wa sheria ya vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 na usajili wa kudumu (full registration) kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(b)

kinachotaka chama cha siasa Ili kupata usajili wa kudumu ni lazima kiwe na wanachama mia mbili katika mikoa kumi (10) huku mikoa miwili ikiwa mmoja Pemba na mwingine Unguja, CHADEMA iliasisi hatua hiyo kama SAFARI YA TRENI KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA.

Dhana “SAFARI YA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA” ilimaanisha kwamba, katika dhamira ya kutafuta mabadiliko ya kweli na kuunda serikali kwa kushinda uchaguzi, wapo watakaonunuliwa, watakaoamua kuacha siasa, watakaohama chama, watakaoachana na CCM na kupanda Treni popote!

Freeman Mbowe na waasisi wenzake waliipa safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma kwamba kufika Kigoma ni CHADEMA kushinda uchaguzi na kuunda serikali. Waliamini kwamba katika safari, wengine watashukia Kibaha, wengine watapanda, wengine watapanda Treni Morogoro

Wengine watashuka, wengine watapanda Dodoma wengine watashuka. Hivyo walimaanisha kwamba, katika safari ndefu ya kufika kigoma (kipindi hicho safari ya Treni kutoka DSM kwenda Kigoma ilikua ni ya shida, mateso na maumivu. Ilichukua siku 3 hadi 5 kutoka DSM kufika Kigoma)

Hivyo Mateso waliyoyapata Waasisi kuijenga CHADEMA walifananisha na safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma. Mfano, viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Edwin Mtei, Bob Makani, Freeman Mbowe, Mary Kabongo na Evarist Maembe walipigwa mawe na kufukuzwa na wananchi Morogoro.

Waliambiwa kwamba “CHADEMA ndio nini? Kwa nini mnampinga chama chetu kilichotukomboa Kutoka kwa utumwa wa wakoloni. Kwa nini mnapinga chama cha Mwalimu Nyerere baba wa taifa? Kwa nini mnapinga chama cha wanyonge CCM chama chenye matumaini kwa wakulima na wafanyakazi?”

Walipigwa mawe, kufukuzwa maeneo mbalimbali, kutukanwa, kudhalilishwa na kudhihakiwa. Kuzungumza siasa za upinzani ilionekana ni usaliti na uhaini, walivumilia. Wengine walikata tamaa, wengine waliamua kurudi CCM, wengine waliamua kulinda vyeo vyao na maslahi yao na kurudi CCM

Mwaka 1995 Edwin Mtei na Bob Makani wote wawili walichukua Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote walionekana kuwa na nguvu. Mapambano huo ulileta sitofahamu kubwa ndani ya CHADEMA.

Freeman Mbowe kama kijana alitoa ushauri kwa chama kwamba CHADEMA isisisimamishe mgombea urais ili kuepusha mpasuko ndani ya chama na badala yake CHADEMA imuunge mkono mgombea wa urais kupitia NCCR MAGEUZI, Augustine Lyatonga Mrema.

Ushauri huu wa FREEMAN Mbowe uliungwa mkono na wanachama na Viongozi. Edwin Mtei na Bob Makani waliacha mchakato huo na CHADEMA ilimuunga mkono mgombea urais wa NCCR-MAGEUZI, Augustine Lyatonga Mrema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.

Freeman Mbowe alichukua fomu kugombea ubunge jimbo la Hai mwaka 1995. Freeman Mbowe wakati wa kampeni jimbo la Hai , aliombwa kugharamia mkutano wa mgombea urais Augustine Lyatonga Mrema na aliahidiwa kwamba Mrema atamnadi jukwaani. Mbowe kwa kuwa alikua na Fedha na uchumi mzuri.

aligharamia mkutano huo ulioandaliwa na FREEMAN Mbowe ikiwa ni pamoja na malazi ya timu ya kampeni ya Mrema nk. Lakini Augustine Mrema alipofika Jukwaani alimpuuza Freeman Mbowe wa CHADEMA na kumnadi mgombea wa NCCR MAGEUZI aliyeitwa Mwinyihamisi Mushi.

Katika uchaguzi huo mgombea wa NCCR MAGEUZI Mwanahamisi Mushi alishinda uchafu kwa kupata kura 29,046 (52.0%) huku Freeman Mbowe akiambulia kura 15,995 (28.6%). Freeman Mbowe hakukata tamaa, aliendelea kuweka nadhiri ya kuwa mbunge wa Hai lakini kupitia CHADEMA (sio vinginevyo)

Mwaka 2000, ukafanyika uchaguzi mkuu nwingine tena. Freeman Aikael Mbowe aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata ushindi wa kura 64.5% dhidi ya mpinzani wake wa NCCR MAGEUZI ambaye alikula mweleka kutokana na chama chake kuwa na mvurugiko mkubwa,

Mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya Mabere Nyaucho Marando na Agustine Lyatonga Mrema uliifanya NCCR-MAGEUZI kuyumbana sana na kuanza kupoteza mvuto wake kwa umma. Viongozi wake wakaanza kujiondoa katika chama hicho. Freeman Mbowe aliongoza jimbo la Hai mpaka mwaka 2005.

Katika nafasi ya Urais, FREEMAN Mbowe na CHADEMA kwa ujumla walikubaliana kwamba CHADEMA isisimamishe mgombea yeyote bali chama kimuunge mkono mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Haruna Lipumba. Lakini makubaliano hayo hayakufanikiwa. Freeman Mbowe akagombea Urais.

Uchaguzi wa urais na ubunge ulifanyika mnamo 4 Desemba 2005. Mapema ulikuwa ulipangiwa kufanyika mnamo 30 Oktoba lakini ukahairishwa kutokana na kifo cha mgombea kiti cha Makamu wa Rais (mgombea mwenza wa CHADEMA), Jumbe Rajab Jumbe.

Mwaka 2004, Freeman Mbowe aligombea uenyekiti wa CHADEMA TAIFA na kushinda akimpokea Bob Makani ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1999. Mbowe baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alifanya mabadiliko makubwa sana ndani ya chama.

Baada ya kuchaguliwa, Freeman Mbowe alifanya mabadiliko makubwa sana ndani ya CHADEMA. Ni kipindi hiki Mbowe alianza kutembelea vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania, kufuatilia wanasiasa mbalimbali kutoka CCM, NCCR MAGEUZI, CUF, TLP na vyama vinginevyo. Mifano iko mingi.

John Mnyika ambaye alikua mwanaharakati wa kutetea haki za wanafunzi na watu mbalimbali na pia akiwa mtangazaji wa Radio One Stereo, Freeman Mbowe alimshawishi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuungana na wanamabadiliko wengine.

Hata hivyo, uwezo mkubwa wa John Mnyika ambao aliuonesha katika ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (ingawa yeye alikua akisoma masomo ya jioni) alisimama na kupinga sera ya uchangiaji wa masomo elimu ya Juu (cost sharing) na kusababisha wanafunzi kuanza Mgomo chuoni

John Mnyika akiwa Morogoro, aliombwa kutuliza hali hiyo na alipofika chuoni, aliita wanafunzi na kuwaambia mambo kadhaa ili kupima ujasiri wao. Alimuomba rafiki yake kurusha jiwe katikati ya kusanyiko kubwa la wanafunzi wenye hasira nyingi, eneo la Mabibo Hostel
 
Siku akitoa kitabu cha kuelezea uhalisia wa maisha yake ya kweli, sijui mleta mada utaficha wapi sura yako, au na ww utabadili tena ID yako?
 
FREEMAN AIKAEL MBOWE na CHADEMA

Kwa Hisani ya Martin MM

Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14.09.1961 katika wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro.

Freeman Aikaeli Mbowe alisoma elimu ya msingi katika shule ya Msingi Lambo na kufanikiwa kufaulu kwenda shule ya Sekondari Kibaha mkoa wa Pwani.

Alipohitimu kidato cha 4 Kibaha Sekondari, alifanikiwa kujiunga na kidato cha 5 IHUNGO Sekondari Manispaa ya Bukoba. Baadae alielekea nchini Uingereza kwa masomo zaidi. Uingereza alisoma programu inaitwa PPE (Politics, Philosophy, and Economics).

Ni programu ambayo ilianzishwa na Uingereza kwa ajili ya watumishi serikalini. Baadaye nchi nyingine kama US na RSA zimeshaanzisha programu hiyo. Kwa UK inatolewa kama first degree tu. Mbowe akamalizia MBA in Leadership & Sustainability kutoka Chuo Kikuu cha Cumbria, UK.
Hapo kwenye Programme ya PPEya Uingeeza na MBA in Leadership ya Cumbria umechapia. Ungemuacha na hiyo elimu ya Kibaha Sec na Ihungo ingetosha. Hivyo vingine ni sawa na vyeti vya Amazon College ya Buguruni au Paradigm College ya Gongo la Mboto. Not accredired at all

Kama hujaingia miaka 3-5 mfululizo darasani kwa ajili ya bachelors degree jihesabu tu huna degree.

Kama manampenda Mbowe mwambie aji enroll kwenye eveing degree programs zipo hapa Dar es Salaam kama UDSM, Tumaini, Kampala Uni, CBE na IFM
 
Back
Top Bottom