Historia ya kuanzishwa kwa Kampuni ya Google

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Mwaka 1996 vijana watatu Larry Page, Sergey Brin na Hassan Scott wakiwa wanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) ya Sayansi ya Kompyuta (Computer science) Chuo Kikuu cha Stanford, Carlifonia nchini Marekani walifanya utafiti kuhusu matumizi ya intaneti katika kutafuta taarifa ama takwimu ambapo mtu angeweza kuingiza kitu anachokitafuta kisha taarifa zikaja kutoka vyanzo mbalimbali.

Walipohitimu masomo yao waliamua kuufanyia kazi utafiti wao. Lakini Hassan yeye akaachana na mpango huo na akatumia taaluma yake kwenda kuanzisha kampuni ya kutengeneza maroboti. Larry na Sergey wakaendelea na mpango wao na September 4 mwaka 1998 wakafanikiwa kusajili kampuni yao kwa jina la Google wakisaidiwa na wahadhiri wao waliowafundisha Chuo Kikuu Stanford.

Lakini pamoja na kusajili kampuni bado hawakuwa na uwezo wa kupangisha ofisi. Hivyo walilazimika kuomba nafasi nyumbani kwa mwanafunzi mwezao Susan Wojicki. Lakini nyumba ya Susan haikuwa na nafasi ya kutosha ofisi hivyo akawapa eneo la karakana ya magari (garage). Kwahiyo ofisi ya kwanza ya Google ikawa kwenye karakana ya nyumbani kwa kina Susan.

Kufikia mwaka 1999 mambo yakaenda mrama. Biashara haikuwa vizuri kama walivyotarajia na wakaamua kuiuza kampuni yao kwa $1M sawa na TZS 2Bil. Lakini hawakufanikiwa kupata mteja hivyo wakashusha bei hadi $750,000. Kampuni ya Excite iliyokuwa ikiongozwa na George Bell ikatoa offer ya $500,000. Excite ni ni kampuni ya teknolojia kama ilivyo Google.

Akina Larry wakakubali offer hiyo kwa masharti kwamba nao wawe sehemu ya menejimenti ya Excite lakini pia mfumo wote wa Excite ubadilishwe na utumike wa Google. George Bell akakataa, wakashindwana hivyo biashara ikafa.

Baada ya mpango huo kufeli ikabidi akina Larry waandike muswada wa kuomba ufadhili wa fedha kutoka sehemu mbalimbali ili kuinusuru kampuni yao isife. Walipata fedha kutoka kwa Jeff Bezos (mmiliki wa Amazon). Pia kutoka kampuni ya Klainer Peerkins na Sequoia ambazo ni kampuni maarufu kwa kutoa ufadhili kwa biashara zinazochipukia.

Kufikia mwaka 2000 kampuni ya Google ilikuwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha $25M kutoka kwa wawekezaji mbalimbali. Mwaka 2004 ikawa imejiimarisha na kuanza kuuza hisa zake katika soko la hisa la New York, kwa bei ya $85 kwa hisa moja. Ikafanikiwa kupata dola $16Bil (sawa na Trilioni 35 za Kitanzania) na hivyo kukuza mtaji wake na kufikia dola$23Bil kwa wakati huo. Hii ilifanya Google kuwa moja ya makampuni yenye thamani kubwa duniani.

Kwa sasa Google inamiliki makampuni tanzu kadhaa ikiwemo Youtube na Gmail ambazo walizinunua. Na Susan Wojcicki aliyewapa garage yake watumie kama ofisi wamemchukua na ndiye boss wa YouTube kwa sasa. Mtaji wa Google kwa sasa umefikia $280Bil, sawa na Trilioni 620 za Kitanzania (kama bajeti yetu ya nchi kwa miaka 20 ijayo under ceteris paribus).

Larry na Sergey kwa pamoja wanamiliki hisa zenye thamani ya $167Bil (sawa na Trilioni 390 za Kitanzania) na kuwafanya kuwa moja ya Mabilionea wakubwa nchini Marekani. Mbali na hisa hizo pia Larry na Sergey wana utajiri binafsi usiopungua $50Bil (zaidi ya TZS Trilioni 100) kila mmoja.

Kutokana na ukuaji wa haraka wa Google ilipofika mwaka 2015 akina Larry waliona inaweza kushindwa kujiendesha kwa siku za baadae. Hivyo wakaunda kampuni mama (parent company) iitwayo Alphabet Inc ambayo kazi yake ni kuongoza Google na makampuni tanzu yaliyopo chini yake.

Kampuni ya Excite ambayo ilikataa kuinunua Google iliporomoka katika soko la hisa mwaka 2008 na mtaji wake kufikia $23Bil kutoka $46Bil. Hata hivyo imeendelea kuporomoka na mwaka jana ilitajwa kuwa na mtaji wa $6Bil tu. Hii ni sawa na kusema kwamba Kampuni ya Google ina mtaji mkubwa mara 50 ya Excite kwa sasa.

Hata hivyo aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Excite, George Bell anasema hajutii uamuzi wa kukataa kuinunua Google kwa sababu ulikuwa ni uamnuzi sahihi kwa wakati ule.

"Suala halikua pesa. Tungeweza kuwapa $750,000 walizokuwa wanahitaji. Lakini tatizo ni kwamba walitaka kubadilisha utaratibu mzima wa kampuni na kufunga mitambo yao. Hiyo ingeathiri kwa kiasi kikubwa mwenendo wa kampuni (Organizational culture)’ alisema Bell alipohojiwa na CNBC mwaka 2015.



Credit: G.Malisa
 
Yaani ndani ya miaka 20 ndio hali imegeuka kuwa bora zaidi.
Inatia hamasa sana katika utafutaji kwenye kuamini na kuimarisha kile unachokifanya.

But, mtengeneza maroboti anaendekeaje?
 
Back
Top Bottom